Hamisa Mabetto: Natafuta mume miaka 45+ mgane aliyeachwa mzungu

Hamisa Mabetto: Natafuta mume miaka 45+ mgane aliyeachwa mzungu

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,117
Reaction score
1,966
Mwanamitindo Hamisa Mobetto ameamua kuweka wazi mwanaume ambaye anataka kuishi naye kwa sasa, ambapo amedai kuwa anataka mwanaume wa kizungu ambaye alishawahi kuachika na mwenye watoto.

Akizungumzia vigezo vya mwanaume anayemtaka, Hamisa amesema kuwa kwa sasa hapendi kuolewa na vijana na anatafuta Mzungu mwenye umri mkubwa kuanzia miaka 45.

“Mimi hapa nataka labda mzungu au mtu mzima, awe alishawaki kuachwa au Mgane kwa hiyo ndio hivyo, yaani nikisema kijana dah hapana. Awe angalau miaka 45 kwa sababu mimi mwenyewe nina watoto sasa ukisema kijana yeye mwenyewe bado anakua atawezaje kulea watoto wangu,“amesema Hamisa Mobetto kupitia EATV.

Hamisa Mobetto tayari ameshazaa watoto wawili na wanaume wawili tofauti tofauti, ambao ni Diamond Platnumz na Majizzo na amesema kwa sasa hawezi kurudiana na yeyote kati yao.

Kwa upande mwingine, Hamisa Mobetto amekiri kuwa sauti iliyosambaa mitandaoni wiki mbili zilizopita akiongea na Mganga wa kienyeji ilikuwa ni ya kwake.
 
POLEPOLE JAMANI TUNAMALIZIA MAOMBOLEZO YA KITAIFA.
Hayo masuala ya mume mzungu anayajua yeye na nafsi yake
 
Akili za mange hizi.....na hivi ndiyo marafiki kwa sasa bila shaka
 
Hamisa anahitaji uangalizi wa karibu sana
Aliwahi kukaririwa kuwa haaamini katika kuolewa na anafurahi kuzini mpaka.kupata watoto
Kutangaza kutaka mzungu mwenye 45+,anaonesha kabisa kwamba ni Gold Digger!
Akipata kizee anakiroga sawa sawa mpaka.kinamjengea au kumnunulia nyumba
Hamisa hana akili ya kukomaa.kuuza shumizi zake mpaka.afanikiwe,anataka njia za mkato
 
Back
Top Bottom