Hamisa Mobetto amepoteza mwelekeo wa maisha

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
MWISHONI mwa wiki iliyopita, mwanadada Hamisa Mobetto kwa mara nyingine ali-make headline kwenye mitandao ya kijamii, baada ya kuanza kuvujishwa kwa taarifa zake za ndani na mmoja kati ya wasiri wake.

Kwa wapekuzi wa mitandao ya kijamii, watakuwa wanaelewa namaanisha nini lakini kwa kifupi ni kwamba taarifa zilizokuwa zinavujishwa mitandaoni, zimefunua upande wa pili wa maisha ya msanii na mwanamitindo huyu, ambao pengine wengi walikuwa hawaujui.

Naelewa kwamba wakati mwingine mtu asiyekupenda anaweza kuamua kutumia mitandao ya kijamii kukuchafua na kukufanya uonekane si lolote si chochote mbele ya jamii! Najua pia kwamba wapo baadhi ya watu ambao ni mahodari wa kutengeneza habari za uongo kuhusu watu fulani kwa sababu wanazozijua wao wenyewe.

Lakini pia Waswahili wanasema lisemwalo lipo, kama halipo basi laja! Yamezungumzwa mambo mengi kuhusu Hamisa lakini kubwa nataka nizungumze na mwanadada huyu kuhusu suala la uhusiano wake wa kimapenzi na picha anayoijenga kwenye jamii.

Hamisa amepoteza utulivu katika mapenzi, kila kukicha anaibuka na skendo mpya kuhusu mapenzi, leo ukisikia hili basi ujue kesho linakuja zito zaidi ya lile la jana. Nakukumbusha kwamba Hamisa ni mama wa watoto wawili.

Wa kwanza ni yule aliyezaa na bosi mmoja wa redio maarufu Bongo, walikuwa kwenye uhusiano ‘siriasi’ na pengine wengi walianza kumjua Hamisa Mobeto kipindi hiki.

Baadaye sijui ikawaje, penzi hilo likafa lakini mara zikaanza kuibuka tetesi kwamba anatoka kimapenzi na Diamond Platnumz, kila mtu akawa anakanusha lakini mwisho wa siku, uhusiano huo umesababisha kupatikana na mtoto mwingine.

Kwa hiyo unapomzungumzia Hamisa, elewa kwamba unamzungumzia mama wa watoto wawili! Hakuna namna yeyote mama wa watoto wawili anaweza kuwa bado hajakomaa kiakili, Hamisa hana utoto wowote wa kujificha anapofanya haya madudu yake.

Hebu turudi kwenye pointi, katika chating zinazosambaa, inaonesha kwamba kumbe ile safari ya mwanadada Hamisa Mobeto kwenda nchini Marekani, haikuwa ya kikazi kama mwenyewe alivyotaka kuwaaminisha Wabongo.

Ilikuwa ni safari ya mapenzi, ambayo iliratibiwa kwa sura ya kufanya ionekane kwamba mwimbaji huyo wa Madam Hero anakwenda kutangaza kazi zake kimataifa, kumbe wapi!

Mwanaume anayetambulishwa kwa jina la Mr Champagne, msanii wa muziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ndiye anayetajwa kuwa nyuma ya mchongo mzima.

Achana na madudu mengine kibao yanayotajwa kufanyika katika ziara hiyo ya Hamisa, wiki chache zilizopita ni Hamisa huyuhuyu aliingia kwenye skendo nyingine ya kudaiwa kukwapua mwanaume wa mwanadada mwingine aitwaye Tahiya.

Skendo ikawa kubwa kwelikweli na kusambaa kila kona, huku Hamisa naye akishupaza shingo mithili ya anayesema ‘kwani tatizo liko wapi?’ Mambo anayoyafanya Hamisa, hayafanani kufanywa na mama wa watoto wawili!

Inaonesha kuna kitu hakipo sawa kwenye kichwa cha Mobeto, pengine aliyoyapitia yamemuathiri kisaikolojia kiasi cha kumfanya asielewe tena nini anataka kwenye maisha yake. Anahitaji kusaidiwa huyu. Haya ni maneno dawa ambayo akijitafakari na kuyafanyia kazi, yanaweza kumfaa.
 
Achana naye, si umesema ni mama wa watoto wawili?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... maisha binafsi ya mtu mwachie mwenyewe!
 
Kwa hiyo unatuletea maisha ya Hamisa Mobetto sisi wana JF ili tufanyeje? Pambana na hali yako acha kufuatilia ya wengine.
 
Kweli kabisaa...Hamisa anapita alimopita Wema!!hata hajali yeye anaona watu tunamuonea tunavyomsema

Na mamayake na yeye ndio kahaba aliyezeeka..muhuni wa Zamani wala hana cha kumshauri Misa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Champions League wakuu! 4 hours to go.
 
Naona Umekoleza Tu, Umeshauri Kipi? Kazi Ya Hamisa Inayomuingizia Kipato Unaijua? Yeye Hajapotea Ila Wewe, Think Twice,!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…