Je huo mkataba mmependekeza imeshindikana? Sabbu kumbukeni wana simba sio nyinyi peke yenu wanasimba wao wengi sana hata hao mnaosigana nao ni wanasimba kama nyinyi, kama wao wanaona kuna jema wakifanya hivyo kwa maslahi ya Club kwanini nanyi msione ni jambo jema?
Kuna faida gani ya kukaa na majengo yaliyo chakaa, ambayo si faida kwa club wala wanachama na kuna faida gani ya kuwa na jina kubwa la Simba lakini timu haina mafanikio ya maana ndani na Nje ya Nchi?
mi nilidhani suala ingekuwa mzee kilomoni na timu yake upande ambao wana hizo nyaraka wanazokatalia wangeweka masharti yao mezani kwa niaba ya upande wao je wanataka kitu gani kwa kushikilia hizo hati?, na waseme hivyo mbele ya wanasheria na waandishi wa habari huenda hoja zao zina mashiko..kwa faida ya club ya leo na kesho.
Kisha upande wa Bodi ya Simba(muwekezaji) nao watoe malengo yao na nia yao kwa kuhitaji hizo hati kisha muafaka kwa maslahi ya club ufikiwe sio kwa matumbo ya watu fulani ni wajinga wajinga ambao mpaka leo wanaamini katika uchawi na ushirikina..