Hamisi Mandi (B 12) rasmi E FM kutoka Clouds FM

Hamisi Mandi (B 12) rasmi E FM kutoka Clouds FM

Ina maana hujui kuwa JF ni ya kila MTU. Jinsia zote na hadi wenzako kina James delicious WAPO humu ndio maana na wewe upon, unatukana ila tunakuvumilia
 
CMG sio rahisi kudorola kwa mfanyakazi mmoja tu kuondoka

Ni kweli kabisa kipindi Kama kipindi kinaweza ku shake kidogo na hii ni kwa muda mfupi sana

Tuangalie coverage Kwanza. Efm na Clouds ni redio gani ina coverage kubwa kuliko nyingine? Utagundua ni Clouds

Turudi kwenye XXL, huyo the Navigator hicho kipindi alikuwa peke yake? Jibu ni hapana. Kama ni hapana, ana nini cha ziada? Jibu ni ana kipaji, ameshajijenga hivyo ana ushawishi kwa jamii ya vijana na wanamuziki. Sawa, hapa unajiuliza je, ni rahisi kuhama na mashabiki wake wote? Hapa jibu ni hapana kwasababu hata XXL yenyewe watu wanapenda segment ya mwisho ambayo inakuwa mseto ikiongozwa na Mchumvo

Kwa hiyo utagundua huenda na yeye akakutwa na waliyokutana nayo kina Gardener walivyoondoka na baadae wakarudi

Clouds imeji establish sana kiasi kwamba mtangazaji mmoja sio rahisi kuua kipindi akiondoka. Nadhani aliyebuni utaratibu wa kuwaweka wengi aliona mbali

Kazi kubwa naiona kwake kuanza kuwashawishi shabiki zake wahamie alikohamia ikiwa ni pamoja na wadhamini wa kipindi maana hao huangalia coverage na audience

But all in all, wakati mwingine ni bora kutembea tembea kuliko kukaa sehemu moja. Huko akafanye cha tofauti zaidi ili watu wathibitishe talent yake
Gardner alirudi kwa kukosa ajira huko alikokuwa au alirudishwa kwa dau?
 
Gardner alivyoondoka Jahazi kipindi kilishake sana, wakapita watangazaji kadhaa lakini hakuna aliyeweza kufit, ikaubidi uongozi umwage pesa ndefu ya mshahara kumshawish kurudi tena, so tukubali tu kwamba Team ni kubwa kuliko mchezaji lakini wakati mwingine mchezaji anaweza kuifanya team itetereke
Cha ajabu kuna wajinga humu wanataka kufanya kuwa Gardner aliondoka akarudi as if huko alikokwenda alipoteza kazi akawa hana mchongo. Hawasemi kuwa Clouds ilibidi wamnunue tena.
 
Kwani huyo alohama ni mwanamke au mwanaume na ilikuaje mwenyekiti wa kijiji hajapewa barua ya wito polisi
 
Walisema hvy kwa Hando, B-12 ni moja ya icon ya clouds fm, Kama hamjui.....jamaa yupo pale inakaribia miaka 20 hv tangu enzi za kina marehemu Vivian....so kusepa kwake Kuna impact kubwa kwa XXL,na CMG, jamaa ndy alikuwa mkali kwe interview na hata ku MC matamasha, ana uweledi wa kuuliza maswali, ni mtulivu akiwa kwe Mike na ana exposure ya mmb lukuki.

Kuna mtu kasema Adam ndy kila kitu pale XXL, itakuwa huyu mdau ameanza kufuatilia clouds miaka miwili nyuma. B12 ndy influencer wa watangazaji wote wa afternoon shows, kila mtangazaji wa radio ya kisasa alikuwa anajaribu ku imitate style yake ili aonekane bab kubwa.
The King Of The Afternoon Shows.
 
Kimsingi ni kuwa watangazaji wengi wa clouds walikuwa loyal kwa Ruge kuliko clouds yenyewe.So bila Ruge chochote kinaweza kutokea.Kingine ni kuwa hakuna mtu mwingine wa kufikiria nini cha kufanya kinachovutia kama alivyokuwa akifanya Ruge..Hili litawagharimu sana clouds.
 
Clouds wana kazi kubwa sana. Kwasasa wanapambana bila Ruge ambaye ndiye aliyekuwa key master pale. Ni kosa kuanza kupoteza icon kama B12 (kama kwa Wasafi kumpoteza Jonijoo) wakati bado wanatengeneza future mpya bila Ruge.

Ninachoona Majey anajua kwa kiasi fulani njia za Ruge na ameona gape ambalo ameamua kuli target. Clouds ile ya matamasha imekufa, hawana tena king maker na wabunifu wao uwezo wao ni wa kawaida kama media zingine tofauti na Ruge na Majey hawamuwezi.

Clouds wasipoelewa position yao baada ya Ruge kuondoka na kufikiri mambo yataenda kama kawaida ni kujidanganya, lazima wabuni njia mpya. Kusaga ni mwekezaji tu lakini anategemea brains kama Ruge ndio maana ku spread risk kawekeza sehemu nyingi.

Nani alitegemea Radio one leo kuzidiwa hadi na Times Fm? Clouds wajipange sana sana!
Radio One imezidiwa na Times fm!? Hii hii Times fm inayosikika mikoa miwili sijui mitatu huko? Hii survey yako ulifanya lini!?
 
Nadhani Clouds hakuna mshahara na marupurupu kama wengi wanavyochukulia, ila wanachofanya wao hasa ni kuwahamasisha vijana wao kutumia fursa ya kuwa clouds kuanzisha biashara na mambo yao mengine na wao wanawapa platform ya kutangaza na kupigia promo bure
Hauko sahihi kwenye hili mkuu, clouds kuna mishahara mikubwa kuliko media yoyote upande wa redio nchini ukirudi kwenye marupurupu ndio kabisa na hili Jo aliweka wazi kuna mwezi millad aliingiza pesa nyingi kuliko Kusaga
 
Hivi bado watu wanasikiliza redio? Wanasikilizia wapi?

Kwenye simu ama kwenye gari? Najua tecno ndio zina redio.

Aisee.
Kuna online radio mkuu, kama mimi kwa siku nna vipindi vyangu kwenye radio, kumi nambili kamili nipo radio1 naakiliza bbc, kumi nambili na nusu rfa magazeti, moja kamili r1 habari hadi uchambuzi wa magazeti, hapo nazima nafanya mishe zingine, mbili kamili narudi PB wakimaliza magazeti, hapo ndio siwashi tena radio hadi tatu kamili ucku Sports Xtra
 
Ww una uhakika gani kua amefukuzwa?
Acha vioja. Nime_quote post yako kuwa "Twangana hapa naona hajafikiria kabsa". Ndio maana nikakuuliza wewe una uhakika gani hajafukuzwa? Maana umeandika "hajafikiria kabsa" kuonesha kuwa aliondoka kwa utashi wake.
 
Za chini ya kapeti

- Adam Mchomvu to Efm
- Jeff Lea to Efm
- Barbara Hassan to Efm

Maisha ni kama sifuri unapoanzia kuchora ndipo utakapo malizia....
Tetesi zinasema hali ya kiuchumi sio nzuri sana mjengoni na kuna azimio la kupunguza mishahara ambalo wengine wameona sio poa bora wajiondokee zao. Ndio maana kuna kampeni kubwa ya kutoa promotion ya matangazo.
 
Back
Top Bottom