Hamisi Mandi (B 12) rasmi E FM kutoka Clouds FM

Hamisi Mandi (B 12) rasmi E FM kutoka Clouds FM

Hao unaodai wanakuwa kwenye vyombo vya usafiri, wanasikilizishwa redio (kwa maana ya redio ya gari iliyowashwa na dereva) au wanasikiliza wenyewe kutoka kwenye simu zao?
We una onaje mkuu?
 
We una onaje mkuu?
Mimi binafsi naona wanaokuwa kwenye vyombo vya usafiri , hasa wa uma, huwa wanalazimishwa kusikiliza redio ambazo zinakuwa zimefunguliwa. Kwa hiyo hapo si sahihi kusema wanasikiliza.
 
Clouds ipo na itaendelea kuwepo bila hata dozen ukisikiliza XXL anayefanya kipindi kinoge pale ni Mchomvu kina bdozen wamefunikwa na mchomvu na ukifuatilia siku mchomvu asipokuwepo show inapoa sana kwa ubunifu Clouds haitegemei kichwa kimoja Mzee hilo ulielewe ndio maana watangazaji wao wakienda hata media zingine hawashine kama walivyokuwa Clouds; rejea Gadner alivyoenda Times, nenda kwa Ray Mshana na yule mwanamke walivyoenda wasafi njoo kwa Maestro alivyoenda e-fm na wengine wengi BTW chukua hii kila mtangazaji Tanzania hii ndoto yake ni kufanya kazi Clouds media kuanzia salary, fursa na bata la watangazaji pale asikuambie mtu, Kingine bdozen siyo wa kuajiriwa e-fm siyo level zake Elimu yetu imetuathiri sana kutegemea ajira ndio kila kitu jamaa angebase kwenye biashara zake za nguo na kuitangaza zaidi Born to shine, Mwisho kabisa HII NI SAFARI YA KUELEKEA Wasafi media.
Hicho kipande chako cha mwisho kabisa ndio maono yangu pia...hii ngoma kituo kinachofuata ni Wasafi Media...dozen na Mondi ni washkaji sana na ndo maana dakika za mwisho kaona atoe kinyongo rohoni amsifie tu jamaa kwenye ile show ya jeje mtvbase..hlf liwalo na liwe.
 
Radio One imezidiwa na Times fm!? Hii hii Times fm inayosikika mikoa miwili sijui mitatu huko? Hii survey yako ulifanya lini!?
Hivi kusikika sehemu kubwa ndo kuwa bora ee?Basi radio free afrika na tbc taifa ndizo redio bora kabisa
 
Hivi kusikika sehemu kubwa ndo kuwa bora ee?Basi radio free afrika na tbc taifa ndizo redio bora kabisa
Bila ya shaka hapo. Redio binafsi za kibiashara mtaji wao ni kusikika maeneno mengi zaidi ili kuvutia matangazo. Kama haukui kwenda maeneo mengi zaidi ya nchi kulinganisha na umri wa Radio ina maana hauna unachofanya zaidi ya kucheza tu. Yaani uwe na audience ya kutosha halafu usikue!? Haiwezekani hiyo. TBC Taifa, lengo lake kuu kuanzishwa ni biashara!? Je, TBC isipoingiza hata shilingi kumi ya mapato, wafanyakazi wake hawatalipwa!?
 
Boss tukiachana na tbc ambayo ni ya serikali redio binafsi za kisasa zinahitaji kuimarisha brands zao ili ziingize faida both kwa matangazo na kwenye social media.Ili upate matangazo inategemea ukubwa wa brand yako.Kuimarisha brand yako inakubidi uwe na mbinu za kuwafanya watu wengi wakusilize wewe zaidi kuliko redio nyingine.Ili Watu wengi wakusilize sio sana inahitani usikike eneo kubwa.Point yangu ni kuwa coverage yako yaweza kuwa kubwa kama RFA,kwa mfano lakini ukawa huna brand.Redio mpya yaweza kuwa na coverage ndogo lakini ni brand kubwa.Inakuwa na vipindi vinavyofuatiliwa na watu wengi zaidi so inapata matangazo mengi kuliko mwenye coverage kubwa lakini hana wafuatiliaji wa vipindi vyake kwa kuwa havivutii...Mengine nakubaliana na wewe kwa kiasi kikubwaa
 
clouds sasa ndio inaelekea ukingon.....kwel nimeamin kila nabii na zama zake, maana XXL kwisha kazi, Ala za roho kwisha kazi, power breakfast kwishiney imebaki sports extra, wakizingua na iyo bas clouds bye bye
 
Maisha haya,
Enzi nasoma kuna muda nilikuwa natoroka shule hasa vipindi vya dini vya ijumaa ili nikasikilize XXL clouds usiku misele ilikuwa inaanza baada Amplifier ya Millard Ayo,leo miaka kama nane hata sijui kinachoendelea huko redioni,habari nimebaki kuzipata kupitia mitandao tu,TV mpaka weekend napo ni kubahatisha sana utafutaji umetufanya watumwa wa maisha yetu.Na huku ninakoishi redio pekee ninayoweza kusikiliza siku nikibadili life style ya utafutaji ni clouds tu maana ndiyo radio inayosikika hizo Times, Efm,EAradio zote hizo hazisikiki na wala sijawahi hata kuzisikia labda kupitia mitandao ipostiwe clip.
Nachojiuliza hivi haiwezekani kuzaliwa kizazi kingine cha watangazaji ili kupunguza ile kutegemea mtu kiasi kwamba akihama kipindi kinayumba.
 
Wapi upo?
 
Au ile kauli yake ya juzi kuhusu ile performance ya Diamond MTV base ndio imemponza.

Wanajiua wenyewe taratibu kwa vinyongo na beef zisizo na maana ,nimeona Majizzo kaposti kwenye page yake ya Instagram.
Hakuna cha kauli kumponza, alishajua muelekeo wake. Ile kauli ni kutafuta sababu tu
 
Back
Top Bottom