Tetesi: Hamisi Mgeja mbioni kurejea CCM

Tetesi: Hamisi Mgeja mbioni kurejea CCM

mbona wajitia aibu sana wao ndio wanaitwa ng'ombe wasio na mkia dah wabongo noma
 
Ng'ombe aliye katwa mkia lazima afahamike tuu huwez uficha mkia ulio katwa
 
Hatuwapi cheo tena wakafie mbali huko
 
Afadhali warudi Ccm , chama chenye kila aina fursa , uko chadema ni kutiana umaskini tu
 
Kila la heri kwao,hata hivyo kura zao na za wafuasi wao zilitusaidia sana na walichangia sana kuijeruhi CCM kwenye uchaguzi mkuu.
 
Hali ndani ya Chadema kwa waliomfuata Lowasa imekuwa ngumu baada ya kukiridhisha kuwa chama walichoenda hakina nafasi kwa wageni. Hivyo wamegundua njia muafaka ni kurejea CCM ambako kuna uhuru wa kidemokrasia ikiambatana na fursa tele za kushiriki katika ujenzi wa Taifa. Kinachowaondoa CDM ni utaratibu wa chama kuwakumbatia wenye nacho badala ya kutoa nafasi sawa kwa wanachama wote kutoa maoni na kushiriki katika kufikia maamuzi yahususiyo maendeleo ya chama. Ufinyu wa demeokrasia ndani ya CDM unachangia aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, ndugu Hamisi Mgeja kufikia uamuzi wa kurudi nyumbani, CCM kuliko demokrasia ya uhakika na ushiriki mpana wa wanachama kuchangia maendeleo ya chama. Wakati wowote Ndugu Mgeja ataita waandishi wa habari na kutangaza kurejea CCM
Sawa arejee kama mwanachama wa kawaida lakini uongozi No no nooooo. Huyu ni nyumbu wa malisho hawezi kua kiongozi. Ameonyesha anaweza kununuliwa na kuuza wanachama kwa hela.
 
It is obvious kule hakuna nyumba za kujiuzia wala mashirika na viwanda. Hakuna escrow, meremeta, green finance wala log me in au hata uniform hewa
 
Ni haki ya kila raia kuamua upande wa kisiasa anaotaka ili mradi havunji sheria.

Hata hivyo, kama ana hamu ya kuitwa majina kama msaliti, mamluki au mwenye njaa kali basi athubutu kufanya hivyo.

Ila nadhani tunahitaji siasa ambazo ni more objective and strategic zaidi ya hizi tunazoziona za kimatukio. CCM ilishakuwa hoi kabisa na ilishaanza kuonekana kukubali kuwa inaweza kuondoka kwenye kushika dola.

Lakini yaliyotokea upande wa upinzani last year kabla ya uchaguzi na yale yanayoendelea kuonekana sasa yanaashiria jambo moja tu....kuimarika kwa CCM na kuporomoka kwa upinzani. Upinzani umelala...na kuishia kulaumu, kubeza na kuishi kwa matukio.

Obviously, kama opposition parties hazibadilika haraka na kuendana na mahitaji ya sasa ya kisiasa, basi chaguzi za 2020 na 2025 zitakuwa very bad news kwa upinzani na tutaendelea kuisikia sana ile slogan ya "kura zetu zimeibiwa"
 
Back
Top Bottom