Hamisi Shaban Taletale aka Babu Tale, fanya hima ujenge kwenu hii nyumba ni aibu kuu

Hamisi Shaban Taletale aka Babu Tale, fanya hima ujenge kwenu hii nyumba ni aibu kuu

Bado unazunguka bila point ya msingi,kwa hiyo mbunge msukuma ndio reference yako wewe.
Two wrongs doesnt make correct.
Hicho ulichokinukuu ndio kinastahili kuwa majibu kwako kulingana na kile ulichokinukuu awali.
.
Mtu kama Tale ambaye ni maarufu masikini wengi wanahitaji kuona anaishi vile wanavyoona na kutaka wao na si anavyotaka yeye aliyepambana akapata hivyo alivyonavyo!
.
Hapo mnapopabeza kama kweli ana nia ya ubunge tayari ameshaupata huo ubunge kwa hayo makazi tu.
nenda leo hii Nyehunge kwa kina Joseph Msukuma ukapaone anazidiwa na nyumba za watu kibao and still anamiliki mabasi mengi na migodi pia.
.
na wakati akiwa mwenyekiti wa CCM Geita alikuwa anatembea na Land cruiser zaidi ya 20 kwenye msafara wake ila kwao pabaya kuliko kwangu changamka wewe
 
sawa kwa hiyo hao uliowataja ndio unawasifia kwa ushujaa wa kutojenga kwao?na ndio reference yako wewe yaani unataka kuwaiga upumbavu walioufanya
Hey kama unataka tutumie kiingereza sema tutakitumia chenyewe tu, usiharibu hii lugja adhimu.
.
Sio Msukuma tu hapo awali nimetaja wengine wawili Mwigulu Nchemba wa Makunda, na Kitila Mkumbo wa mtekente! Kwao ni kubaya kuliko kwa wahadzabe angalau hata Mwigulu kaweka kwao bati la blue!
.
Unataka upajue na kwa kina Ngereja mbunge wa Sengerema ushangae uanguke na ufe wewe?
masikini mna shida sana endeleeni kupangia watu waishi mnavyotaka ninyi
 
Hamtaelewana na hao unaobishana nao. Uelewa wako ni tofauti kabisa. Bora uwaache kama mimi nilivyowaacha. Mawazo ya masikini ni kuvaa vizuri na kula vizuri. Atatamani kujenga kila mkoa japo hana uwezo wa kujenga hata kibanda kimoja. Kwa mawazo hayo, akiona mtu kama Kitila hakujenga kwao, huwa anajisikia kuzimia. Lakini yeye pia akipata pesa nzuri huko mbele, amini usiamini, vipaumbele vyake vitabadilika pia. Ataona kula siyo issue tena, nyumba kila mkoa siyo issue tena...
Hey kama unataka tutumie kiingereza sema tutakitumia chenyewe tu, usiharibu hii lugja adhimu.
.
Sio Msukuma tu hapo awali nimetaja wengine wawili Mwigulu Nchemba wa Makunda, na Kitila Mkumbo wa mtekente! Kwao ni kubaya kuliko kwa wahadzabe angalau hata Mwigulu kaweka kwao bati la blue!
.
Unataka upajue na kwa kina Ngereja mbunge wa Sengerema ushangae uanguke na ufe wewe?
masikini mna shida sana endeleeni kupangia watu waishi mnavyotaka ninyi
 
Tafsiri zinatofautiana. Ndio maana tutaendelea kubishana hapa hata mwaka mzima. Zamani kule kijijini kuna watu niliwaita matajiri, leo nikienda nawaona masikini tu. Wana nyumba ya bati ndogo ambayo imezungukwa na nyumba nyingi za nyasi. Hicho ndio niliona utajiri katika mazingira yangu ya kimasikini wakati huo.

Kuna wengine wananiona mimi tajiri lakini mimi sijihesabu katika matajiri. Kigari na kupeleka watoto English medium school hakuwezi kunifanya niwe tajiri. Wengine wakiniona na gari wanafikiri nina pesa za kumaliza matatizo yao. Wananiona mimi ni tajiri sana. Kwa hiyo kama kwako kujenga nyumba ya ghorofa kijijini kwenu ndio utajiri huo basi jenga. Mwache Babu Tale na maisha yake. Anajua matumizi ya pesa zake mwenyewe. Usimpangie. Panga jinsi ya kutumia pesa zako, siyo za Babu Tale.

Wahindi hapa Dar wana hela za kutupwa. Lakini angalia nyumba wanazo kaa - NHC/Msajiri Uhindini na Upanga. Zimechoka lakini wameridhika. Wanaweka pesa benki. Ukwasi wao unaongezeka toka kizazi hadi kizazi. Wana sehemu za kulala japo ya kupanga, wana kula vizuri, watoto wanakwenda shule nzuri... Mwisho wote tunakufa na kuzikwa.
Kwa tafsiri yako wewe utajiri ni nini?
 
Tafsiri zinatofautiana. Ndio maana tutaendelea kubishana hapa hata mwaka mzima. Zamani kule kijijini kuna watu niliwaita matajiri, leo nikienda nawaona masikini tu. Wana nyumba ya bati ndogo ambayo imezungukwa na nyumba nyingi za nyasi. Kuna wengine wananiona mimi tajiri lakini mimi sijihesabu katika majiri.

Kigari na kupeleka watoto English medium school hakuwezi kunifanya niwe tajiri. Kwa hiyo kama kwako kujenga nyumba ya ghorofa kijijini kwenu ndio utajiri huo basi jenga. Mwache babu Tale na maisha yake. Anajua matumizi ya pesa zake mwenyewe. Usimpangie. Panga jinsi ya kutumia pesa zako, siyo za Babu Tale.

Wahindi hapa Dar wana hela za kutupwa. Lakini angalia nyumba wanazo kaa - NHC/Msajiri Uhindini na Upanga. Zimechoka lakini wameridhika. Wanaweka pesa benki. Ukwasi wao unaongezeka toka kizazi had kizazi. Wana sehemu za kulala japo ya kupanga, wana kula vizuri, watoto wanakwenda shule nzuri... Mwisho wote tunakufa na kuzikwa.
Aliyekudanganya wahindi hawajengi ni nani?Sema hawajengi Tanzania kwa sababu sio kwao huku wapo kiutafutaji tu,na wanatembea nchi nyingi kwenye kutafuta maisha.
Kwa mfano sasa hivi wapo Tanzania ila upepo ukibadilika wanakimbilia Zambia,Angola,Kenya au hata South Africa na pesa wanazopata wanakwenda kujenga kwao India.
Sasa wewe jidanganye uache kujenga kwa kuwaiga wahindi utakuwa juha,kwa sababu hauna kwenu kwingine zaidi ya Tanzania.
 
Wahindi nimesoma nao. Ni marafiki zangu. Nafanya nao biashara. Siwaoni kwenye TV kama wewe. Hiyo ni taarifa. Ujumbe wangu: Usimpangie Babu Tale maisha. Panga yako. Usipindishe mada.

Kwani kuna mtu humu kampangia mtu maisha,tumpangie kwani amekuwa mtoto wetu.
Mtu anapokupa ushauri haimaanishi amekupangia mwisho wa siku muamuzi ni yeye mwenyewe.
Na kuhusu hao wahindi kuwaona kwenye tv futa hayo mawazo,nimeishi nao na kufanya nao kazi.
Tena ni wahindi vichwa na smart,sio hao wahindi mabogus wa kariakoo.
Kwa hiyo wewe kuuza duka kwa nuhindi umeona ni bonge la CV?
Wahindi nimesoma nao. Ni marafiki zangu. Nafanya nao biashara. Siwaoni kwenye TV kama wewe. Hiyo ni taarifa. Ujumbe wangu: Usimpangie Babu Tale maisha. Panga yako. Usipindishe mada.
 
Kama haumpangii Babu Tale. Na mimi pia simpangii basi tumekubaliana. Natafuta pesa. Tusipotezeane muda. Sitokujibu tena.
Kwani kuna mtu humu kampangia mtu maisha,tumpangie kwani amekuwa mtoto wetu.
Mtu anapokupa ushauri haimaanishi amekupangia mwisho wa siku muamuzi ni yeye mwenyewe.
Na kuhusu hao wahindi kuwaona kwenye tv futa hayo mawazo,nimeishi nao na kufanya nao kazi.
Tena ni wahindi vichwa na smart,sio hao wahindi mabogus wa kariakoo.
Kwa hiyo wewe kuuza duka kwa nuhindi umeona ni bonge la CV?
 
Kupotezeana muda kumetoka wapi tena?Kwani kuna mtu amekulazimisha kuingia JF,si umekuja ww mwenyewe,kama unaona unapoteza muda usiingie humu
Kama haumpangii Babu Tale. Na mimi pia simpangii basi tumekubaliana. Natafuta pesa. Tusipotezeane muda. Sitokujibu tena.
 
watanzania tuwe na culture ya kutofuatilia maisha ya mtu na kipato chake....
ni wao wenyewe wanataka wafuatiliwe maisha yao...

kwenye kurasa zao mitandaoni kuna kitufe cha FOLLOW

na umaarufu wao unapimwa kwa wangapi wanafuatilia maisha yako, FOLLOWERS

sasa huwezi kufiwa ukasema leo msini follow maisha yangu...

na kijana wa Tandale mbona simwoni pembeni ya jeneza, hakuja au alikataa kuingia ndani ya hiyo nyumba?
 
Sisi tusio na nyumba Bongo tuna tabu sana. Wengine hawana nyumba lakini wana pesa benki. Wana gari nzuri na nyumba nzuri ya kupanga maeneo mazuri ya mji. Kwani kuna tatizo gani? Mbona watu ambao hajasoma huwa wanashabikia nyumba hivi?

Tangu niko mdogo kijijini, wasomi walipokuwa wanatangulia mbele ya haki na kuja kuzikwa kijijini, mbumbumbu wa kijijini walikuwa wanawaongea vibaya sana eti kwa sababu hawakujenga nyumba kwao!

Nimeishi nje kwenye nchi zilizoendelea, ambako watu wana pesa za kutupa, wala watu hawashobokei nyumba kiasi hiki. Watu wanaweka mapesa benki. Wakitangulia, wanaacha pesa kwa familia.
Maisha ni nyumba ndugu!

Kila mtu asipojenga bali akatunza mapesa benki, Je hao wenye mapesa wangeishi juu ya miti? Wanaishi kwenye nyumba za kupanga, hizo nyumba zimejengwa na watu!

Mungu akikuruzuku pesa jenga ndugu!
 
Kwani kuna mtu humu kampangia mtu maisha,tumpangie kwani amekuwa mtoto wetu.
Mtu anapokupa ushauri haimaanishi amekupangia mwisho wa siku muamuzi ni yeye mwenyewe.
Na kuhusu hao wahindi kuwaona kwenye tv futa hayo mawazo,nimeishi nao na kufanya nao kazi.
Tena ni wahindi vichwa na smart,sio hao wahindi mabogus wa kariakoo.
Kwa hiyo wewe kuuza duka kwa nuhindi umeona ni bonge la CV?
Wewe unaonekana ni mshamba mshamba sana
 
Back
Top Bottom