Hamna kiumbe cha Mungu chochote kilicho haramu, vyote vinaliwa Wala siyo dhambi!! Isipokuwa Usile damu tu!

Hamna kiumbe cha Mungu chochote kilicho haramu, vyote vinaliwa Wala siyo dhambi!! Isipokuwa Usile damu tu!

Reality of heaven

Senior Member
Joined
Nov 2, 2022
Posts
108
Reaction score
353
Habari wakuu!! Leo kuna madhehebu na dini zinadanya watu kuhusu kubagua vyakula mfano nguruwe nk kuwa ukila ni dhambi! Naomba niwatoe hofu kuwa sio dhambi wewe kuleni tu chochote kile kiwekacho mbele yako labda uwe hautumii tu lakini sio kwa maana ya kwamba ukitumia ni dhambi!! Uthibitisho kuwa tumeruhusiwa kula vyitu hivyo ni maandiko haya

1 Wakorintho 10:25
Kila kitu kiuzwacho sokoni kuleni, bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri;

1 Wakorintho 10:26
maana, Dunia ni mali ya Bwana na vyote viijazavyo.

1 Wakorintho 10:27
Na mtu asiyeamini akiwaalika, nanyi mnataka kwenda, kuleni kila kitu kiwekwacho mbele yenu bila kuuliza-uliza, kwa ajili ya dhamiri.
Luka 10:8
Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;

Acha kudanganywa kuwa kuna chakula ukila ni dhambi!!! Viumbe vyote ni vya Mungu!! Hizo sheria walipewa waisrael kipindi hicho lakini Yesu alikuja kufuta mambo hayo!! Karibu kwa mwenye swali

Wakolosai 2:16
Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
 
Back
Top Bottom