Mimi nilimkubali sana Magufuli, na hata msiba wake ulinigusa mno kana kwamba alikuwa ni baba yangu au ndugu yangu. Nafikiri unaiona avatar yangu hapo juu.
Lakini sasa sijui kwanini hoja yako imeegemea katika kumchafua raisi Samia badala ya muhusika wa kitabu kilichomchafua Magufuli!
Ingekuwa kitabu ni cha Samia na kinaponda utendaji kazi wa Magufuli, hapo ungekuwa na haki ya kuja kulinganisha kile kilichoandikwa na Samia na kile kilichofanywa na Magufuli. Lakini kukimbilia kumnanga Samia na kumuacha muandishi wa kitabu salama inafanya baadhi ya watu tuone kwamba labda wewe unachuki binafsi na serikali ya Samia hivyo hili swala umelitumia kama kichaka cha kuhalalisha kumchafua.
Na kumbuka huyo muandishi ana chuki na Magufuli kabla hata Magu mwenyewe hajafariki. Na ashawahi hadi kumfunga, hivyo Samia hahusiki na chochote katika kitabu hicho, maana muandishi hakuanza kumuandika Magufuli leo wala jana bali alianza toka Magu akiwa hai.
Ni sawa na kumponda mume wa mtu bila sababu kisa unamtaka mkewe, na wakati kama wewe ni mjanja basi ni lazima ujue kwamba kuna njia nyingi unazoweza kuzitumia kumpata huyo mkewe, bila hata ya kumponda Wala kumdhalilisha mumewe.