Hamna kiwango cha oil chafu kitakachotosha kumchafua Hayati Magufuli

Samia anatajwa kwasababu ukiangalia kwa ndani kabisa ni kama kuna baraka zake kwa hawa wanaomchafua yaani ni kama anaamini kwamba Magu akichafuliwa madhaifu ya huyu bibi yatajificha au hayataonekana.
 
Samia anatajwa kwasababu ukiangalia kwa ndani kabisa ni kama kuna baraka zake kwa hawa wanaomchafua yaani ni kama anaamini kwamba Magu akichafuliwa madhaifu ya huyu bibi yatajificha au hayataonekana.
Sijui una umri gani mkuu. Lakini kwa sisi wakongwe tunafahamu fika kwamba mtu ukiwa madarakani au ukitoka swala la kuchafuliwa ni la kawaida sana, so inategemea na kiongozi ulie madarakani uta react vipi kwa watu wanaochafua.

Wakati wa Mkapa Mwinyi alichafuliwa sana kwa kuonekana kwamba wakati wa utawala wake alilea rushwa na ufisadi hadi serikali yake ikakosa hela za kuwalipa wafanyakazi. Je unataka kusema kwamba ni Mkapa ndo aliekuwa anatuma wamchafue Mwinyi ili iweje? Kumbuka Mkapa na yeye alikuwa kimya wakati Mwinyi akichafuliwa.

Kikwete alipoingia Mkapa alichafuliwa na ufisadi wa Richmond, kubinafsisha bank za Tanzania na mengine kibao. Ikafika kipindi hadi Mkapa akalazimika kufika mahakamani kumtetea waziri wake aliesemekana alipiga mpunga wa maana huku Mkapa mwenyewe akiwa anafahamu kilichoendelea. So ikalazimika Mkapa aitwe mahakamani kutoa maelezo ya hizo shutuma zilizomhusisha waziri wake, na yeye mkuu wa nchi wa kipindi hicho. Je na Mkapa pia alihenyeshwa sababu na Kikwete, kama Mkapa alivyomhenyesha Mwinyi?

Kikwete Mwenyewe alichafuliwa alipokuwa madarakani na mpaka pia alipotoka madarakani kuliko hata watangulizi wake wote. Je na yeye alibariki mwenyewe achafuliwe?

Magu alipoingia nafikiri unakumbuka alivyokuwa anainanga serikali ya Kikwete kwamba ilikuwa ni ya hovyo, iliyolea uzembe nk. Je na yeye Magufuli alikuwa anaichafua serikali ya mtangulizi wake ambapo na yeye alikuwa mmoja wa mawaziri wa serikali hiyo je tuseme na yeye alikuwa anamchafua mtangulizi wake ili ajisafishie njia?

Huyu jamaa alianza kumchafua Magufuli kabla hata Magu mwenyewe hajafa.

Mpaka Magu mwenyewe akaamua kumtupa jamaa ndani. Je wakati ule alipokuwa anamchafua Magu akiwa hai kabla ya Samia kuwa raisi, hizo baraka za kumchafua Magu wakati Magu akiwa hai alizitoa wapi kwa Magu mwenyewe au?
 
Samia anatajwa kwasababu ukiangalia kwa ndani kabisa ni kama kuna baraka zake kwa hawa wanaomchafua yaani ni kama anaamini kwamba Magu akichafuliwa madhaifu ya huyu bibi yatajificha au hayataonekana.
Anadanganywa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…