Hamna watu wanaotapelika kirahisi kama waumini wa dini hii

Eti ungali hai unakatazwa usitumie pombe na usiwe mzinzi, lakini cha ajabu ukishakata umeme unaruhusiwa kutumia vyote, inabidi uzimie uzinduke kama mara trilioni hivi ndipo utaweza kuelewa huo mstari [emoji1787]
Makatazo yanatokana na athari zake kwenye maisha ya dunia,angalia athari za pombe na zinaa duniani,maisha ya akhera ni tofauti na duniani,ukilewa akhera hutoendesha gari hovyo na kusababisha ajali kwa kuwa hakuna gari huko Wala fly over,hakuna uzazi huko kwamba utasababidha watoto wa mitaani,

Mambo yanayokatazwa kwenye dini Yana athari kwa jamii hayakatazwi tu kumkomoa binadam
 
hili sio suala la dini mkuu ni suala la watu kuwa wepesi wa kuaminishwa kutokana na maswahibu wanayokutana nayo kwenye maisha.

Watu wanapitia mengi haswa changamoto za kipato na magonjwa, ni katika hizi dini watu wanapata sehemu ya kupumulia wakipewa afuheni kupitia miujiza na maneno matamu ya kuwapa matumaini ya kuendelea kuishi tena

ni katika haya makanisa watu wanapatiwa watu wa kuwalaumu kutokana na matatizo yao huku wakiepuka mchango wao kwa yanayowakuta hivyo, kuwapa afuheni kihisia "umerogwa na mama yako lakini usijali tutakusaidia"

Ni nadra kukuta matajiri, wanaume wanaotumia zaidi logic kutatua matatizo yao kuliko hisia au watu wanaopata msaada sahihi haswa wa mental issues wakilowea huku

zamani watu wengi walikimbilia kwa waganga na sasa wanakimbilia kwenye haya makanisa
 
Wewe unamzidi Shekhe Kipozeo kwa Ilmu ya dini?

Mwanazuoni mbobevu Alhaji Kipozeo ametuhakikishia tutapewa BIKRA 72 na nguvu za kula wanawake 100 kwa siku.

Wewe ni nani hata upinge hayo?
 
Rahisi kutapeliwa ni wanawake na graduates
 
Mwamnani wa pale kawe ana waisilamu wengi sana pale huyo ni mfano tu

Manabii wote wa mchongo wana waisilamu kibao

Lakini wakristo wanatapeliwa kirahisi kivipi

Wakati wao ndiyo matapeli hayo mathehebu ya kitapeli hayana mfungamano na ukristo kwa sababu hizo ni fursa watu wameziona na kisheria ni halali basi kila mtu anajifanyia anavyojiskia
 
Wewe unamzidi Shekhe Kipozeo kwa Ilmu ya dini?
Mwanazuoni mbobevu Alhaji Kipozeo ametuhakikishia tutapewa BIKRA 72 na nguvu za kula wanawake 100 kwa siku.
Wewe ni nani hata upinge hayo?
Kumbe unamsikiliza Kipozeo na kwako wewe ndiyo unamuona mbobevu?

Huku sisi huwa hatumsikilizi mtu bali rejea kwenye vitabu.

Sio kama nyie vitabu hamsomi bali unakichukua kama kilivyo kisa Gwajima kasema
 
Wewe unamzidi Shekhe Kipozeo kwa Ilmu ya dini?
Mwanazuoni mbobevu Alhaji Kipozeo ametuhakikishia tutapewa BIKRA 72 na nguvu za kula wanawake 100 kwa siku.
Wewe ni nani hata upinge hayo?
Kumbe unamsikiliza Kipozeo na kwako wewe ndiyo unamuona mbobevu?

Huku sisi huwa hatumsikilizi mtu bali rejea kwenye vitabu.

Sio kama nyie vitabu hamsomi Bali unakichukua kama kilivyo kisa Gwajima
 
Mkristo akiingia msikitini tayari wote waliopo pale wnajulikana ni dini flani kinyume chake.

Kwa sababu hayo yanatambulika ni makanisa
 
Tatizo wanawaamini watu wanaacha kusoma muongozo wao ambao ni biblia.
 
Kumbe unamsikiliza Kipozeo na kwako wewe ndiyo unamuona mbobevu? Huku sisi huwa hatumsikilizi mtu bali rejea kwenye vitabu. Sio kama nyie vitabu hamsomi Bali unakichukua kama kilivyo kisa Gwajima
Kwahiyo anaweza toa maneno yake ya Tandale kwa tumbo kwenye mhadhara na maulamaa wakakaa kimya tu?

Ngoja nikuletee aya na hadithi shekhe
 
Aise Buji Buji ahsante sana kwa kuleta mada hii.Ninachowashangaa wakristo pengine tunaweza kusema ndio waliosoma elimu dunia kuliko waislam lakini mkristo kumuingiza mkenge ni rahisi sana kuliko muislam.

Waislam si wongo sio watu wa kuwaingiza mkenge pamoja na kwamba tunadai hawana elimu dunia kubwa kwa wingi.

Je ulishasikia muislam anajiita nabii? au mtume nadhani akitokea kichwa na shingo yake itagombewa kama mpira wa kona.Uislam nimegundua sio dini ya kinafiki .Ona babu wa Loliondo marehemu RIP alivopagawisha watu.

Buji Buji wanawake ndio wahanga wa hili tatizo imefikia mahali nina mpango wa kumpa talaka mke wangu nikimpa matumizi pesa zote anapeleka huko.Nyumba yangu imegeuzwa kanisa na makelele.

Nilimpa uhuru wa kuabudu lakini unanitokea puani.
 
Kwahiyo anaweza toa maneno yake ya Tandale kwa tumbo kwenye mhadhara na maulamaa wakakaa kimya tu?
Ngoja nikuletee aya na hadithi shekhe
Nasubiria. Nyie mnadanganywa mbinguni kutakuwa na kuimba na kucheza tu.

Mtu akiomba aya kwenye biblia mnaingilia huku mnatokea kule.

Hiyo ya mvinyo nadhani haukuwahi kuisoma kwenye biblia kama mbinguni kuna vyombo.
 
QURAN 6: 93

93. "Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, au anaye sema: Mimi nimeletewa ufunuo; na hali hakuletewa ufunuo wowote. Na yule anaye sema: Nitateremsha kama alivyo teremsha Mwenyezi Mungu.(Na hali anasema uongo?)

Na lau ungeli waona madhalimu wanavyo kuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono wakiwambia: Zitoeni roho zenu!

Leo mtalipwa adhabu ya fedheha kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyasema juu ya Mwenyezi Mungu yasiyo ya haki, na mlivyo kuwa mkizifanyia kiburi Ishara zake. "
 
Si kila Mkristo ni Mkristo.

Sent from my VF-795 using JamiiForums mobile app
 
Tatizo imani dhaifu na kujifanya wana elimu sana kumbe zero

Unatoa mchango huku anaefaidika mmoja tu

Maskini huwasaidii ila unampa anaekuombea kwanini usijiombee mwenyewe

Unaombewa na tapeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…