Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Mambo mengine yanashangaza na mengine yanachukiza. Wapo watu miongoni mwetu ambao wanakasarishwa na wengine wanakerwa kwelikweli kuona CCM inatumia wingi wake Bunge la Katiba kushinikiza misimamo yake. Watu wengine wanakasirika kabisa na wanahamaki wakijiuliza "kwani Katiba inayotaka kupitishwa ni ya CCM au ya Taifa?"; na wengine wanashangaa ati kwanini "CCM haiweki maslahi ya taifa mbele?!" Kweli kabisa wapo watu na wengine ni watu wenye heshima na wazoefu katika siasa za nchi yetu nao wanashangaa ati "CCM imeteka mchakato wa Katiba"
Sasa hawa ndugu zetu hawataki CCM kutumia wingi wake kwenye Bunge la Katiba na wanaisihi ati wasiweke "uvyama" kwanza na badala yake waweke dubwasha moja liitwalo "Utaifa kwanza"! Na hawa si watu nje ya Bunge bali wapo wengine ndani ya hilo Bunge ambao nao wanawasihi wana CCM kuweka "maslahi ya Taifa kwanza"
Kwanini? Kwanini watu hawataki CCM ilioteka ajenda ya Katiba Mpya isitumie wingi wake kupitisha maslahi yake? Kwanini watu hawataki CCM ambayo Mwenyekiti wake alianzisha mchakato wa Katiba Mpya na akawateua wana CCM mashuhuri kuusimamia? Kwanini watu hawataki CCM ambayo ilipitisha Sheria ya Mchakato wa Katiba iliyompa Rais ambaye ni Mwenyekiti wao nguvu kubwa katika mchakato huu wasitumie nafasi hiyo kutimiza maslahi yao?
Watu walikubali ile sheria, wakakubali kushiriki kwenye mchakato na wakakubali kuwa sheria ile ya mchakato imewapa wingi mkubwa wana CCM kwenye Bunge la Katiba. Hivi ndugu zetu walikuwa wanafikiria kuwa mchakato umewekwa kuwajaza wana CCM ilikuwa ni kwa bahati mbaya? Kwamba mchakato mzima unamzunguka RAis na utaongozwa na wana CCM hivi wanafikiri iliandaliwa vile kwa sababu hakukuwa na uchaguzi mwingine (another alternative)? Sasa kama kabla ya kuundwa kwa Bunge la Katiba miaka karibu mitatu nyuma waliambiwa kuwa mchakato huu ni wa ki CCM sasa CCM wanataka kutumia nafasi ya nguvu yao kwanini tunawatakalia?
Kama sera ya CCM ni serikali mbili na hilo limethibitishwa jana na wote tunajua ndio msimamo rasmi wa chama tangu miaka ya 1990s sasa kwanini watu wanafikiria kuwa wanafungwa na mapendekezo ya TUme ya Katiba Mpya? Kwani TUme ya Katiba Mpya ilipiga kura ya maoni au ilikusanya maoni tu? Na nchi haiongozwi na mapendekezo ya Tume inaongozwa na sera za chama kilichoko madarakani na tutake tusitake chama kilichoko madarakani ni CCM; sera zake ndizo zinatakelezwa kuanzia kwenye nishati, maji, elimu, umeme na hata mfumo wa utawala?
Sasa kama CCM msimamo wake ni serikali mbili na kinataka kuhakikisha wanachama wake wana 'toe the line' kwa kuhakikisha kuwa kunakuwa na kura ya wazi kwanini tunataka kuwakatlia? Kwani nani kasema serikali tatu ndilo suluhisho pekee - hata kama limependekezwa na TUme ya Warioba?
Ninachosema ni kuwa kama watu walikubali principle kuwa mchakato huu ni halali na kuwa CCM inaweza kujazana huko ndani sasa kwanini wakatae matokeo ya kujazana huko na nguvu yake hiyo kubwa? Au watu walikuwa wanaombea labda CCM itaacha kuwa CCM na itafuata wengine? Kwamba watu walikuwa wanaombea kuwa CCM itabadilika na kufuata misimamo ya wengine ili kuwaridisha wao na siyo kujiridhisha yenyewe?
Wapinzani na wanamageuzi wengine waliokubali kushiriki mchakato huu na kukubali mfumo huu ulioibeba CCM wawe tayari kula kiburi yao! Wavune walichokubali kipandwe! CCM kwa haki kabisa inatumia sheria na mfumo uliokubaliwa kuhakikisha inapitisha mapendekezo yake na kwa haki kabisa wanaweza kuifumua rasimu ya Katiba kuhakikisha kuwa inatengenezwa kukubali serikali mbili na si tatu kama ilivyo sasa!
Tunaweza tusipende, tunaweza kuchukia, tunaweza kuona kuwa CCM wanaweka uchama mbele n.k lakini ukweli unabakia pale pale; wanafanya kilicho ndani ya uwezo wao. Si tulishawakubali in principle? We have to live with the consequences? Au hatutaki kuishi na matokeo ya maamuzi yetu wenyewe?
Binafsi kwa kweli sijashtuka, sijashangazwa wala sijasikitishwa na yanayofanywa na yatakayofanywa na CCM kwenye hilo Bunge lao. Well, waliliandaa hivyo sasa kwanini tushangae? Watu walikubali wapande mbegu, na tulijua wanapanda mbegu gani tena wanapenda vipi na wapi; sasa leo wanataka kuvunja tunataka kuruka; tunataka viote vingine? Well, imekula kwetu - itakuwepo kura ya wazi na inawezekana serikali mbili ikarudi na wapinzani na wengine hata wakikasirika. Yatakuwa ni maamuzi ya kidemokrasia na yanakubalika kisheria wenye kutaka kugoma Bungeni watagoma, wenye kupiga kelele watapiga na wenye kuzungumza kwa uchungu tutawaona lakini ukweli utabakia kuwa ukweli.
Imekula kwao!
Next time, usikubali ngamia aangize kichwa kwenye hema!
MMM