Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Mtazama, huu unaitwa ukweli mchungu!. Ukweli una tabia moja kuu, "husimama!."Tatizo la wapinzani ni kukubali hata vitu vya kijinga wakati mwingine ili wasionekane wanapinga kila kitu tu kama wanavyoimbiwa! Mchakato wa Katiba ulikuwa na matatizo toka mwanzo lakini busara mbuzi zisizoakisi mahitaji halisi ya wananchi ndio zinatufikisha hapa tunaishia kulalamika.
CCM wanahaki ya kusimamia maslahi yao ikiwemo serikali mbili ambao ni msimamo wao rasmi hivyo mbinu yoyote watayotumia ni sawia kabisa sijui watu wanalalamika nini! Kwa kifupi tunapoteza muda na huu mchakato kibaya zaidi tunazugana huku 2015 ndio hiyo inafika na utafanyika uchaguzi ktk mazingira haya haya!
CCM itashinda tena uchaguzi wa 2015 tena kirahisi kabisa labda kisambaratike kitu ambacho ni kigumu kwa mazingira ya sasa kama haikuwa hivyo mwaka 2005.Tusubiri masihi mpya asimamie ukombozi wa kweli maana inakatisha tamaa.
Watu humu waliposikia tuu mchakato wa katiba mpya!, wamehamasishwa kuwa na too great expectations kuwa 2015 things will change!. 2015 ni mambo ni yale yale, watu wale wale, mbinu zile zile na chama kile kile, ila akiwa ni "nanii" hata kama ni chama hicho hicho!, things will change for the better!, otherwise, we are doomed!.
Pasco