Hamu ya kununua magazeti imenirejelea ghafla

Hamu ya kununua magazeti imenirejelea ghafla

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,427
Reaction score
4,944
hakuna shaka na itabaki kuwa hivyo. baada ya Mwalimu Nyerere alietusaidia kuupata uhuru wa Tanganyika, Dr. John Joseph Pombe Magufuli anabaki kuwa Rais bora wa wakati wote.

kizuri hakikosi kasoro. agenda yake ya kutaka kufuta upinzani haikuwa nzuri na hilo nilimpinga waziwazi kwa kumnyima kura mara zote alizogombea.

na kuhusu kuweka mbele maslahi ya nchi ikiwa ni pamoja na kulinda rasilimali za nchi, kudhibiti uonevu na rushwa. kutokujipendekeza kwa wazungu. upatikanaji wa uhakika wa maji na umeme. hapa anabaki bora na hana mfano wake.

Mama nae anaupiga-piga. shida ni kuwa nyuma yake kuna genge la wabinafsi ambao hawaoni aibu kula rushwa inapotokea kufanya hivyo. kwa hili ajitafakari.

kuhusu uhuru wa habari naiona nuru. hamu ya kutaka kujuwa kinachojiri nchini sasa inanirejea. nanunua hata magazeti sasa.

Peoples! ✌️
 
Daa umenikumbusha mbali. Nilikuwa kila siku sikosi kununua gazeti la mwananchi na kila wiki lazima nisome Rai ambalo niliachana nalo baada ya kununuliwa na janja janja nikaja kuhamia kwenye Raia Mwema. Lakini kwenye kipindi cha mwanzoni cha mwendazake niliacha kabisa kusoma magazeti yote baada ya kuona upuuzi kwani magazeti yote yalikuwa yanaimba wimbo mmoja wa mapambio na kusifu na wakati mwingine kuabudu kabisa. Kuanzia hapo nikaamua mimi na magazeti basi.

Ni takribani mwaka sasa baada ya mwendazake kuondoka lakini jambo la ajabu ni kuwa mpaka sasa magazeti mengi bado yameathirika ni kama bado yapo kifungoni. Hakuna tena zile habari zenye tija kwa jamii zaidi ya udaku, sifa na mapambio hata pale panapohitijika kuisadia serikali kwa kuikosoa ili iweze kujirekebisha na kuwaletea wananchi maendeleo.

Nasubiri labda Tanzania Daima na Mwanahalisi kama wataweza kurudisha zama zile za habari za kiuchunguzi maana Mwananchi lilijijengea heshima ya hali ya juu sana lakini sijui lilikumbwa na nini kiasi hata habari za kupotea kitatanishi kwa mwandishi wao Azory Gwanda hawakuzipa nafasi kabisa. Na mbaya zaidi hata hawakufanya habari za kiuchunguzi kama kawaida yao kuchunguza mambo mbali mbali yenye utata kwa jamii. Kilichobaki kwao cha maana ni katuni ya Kipanya tu.
 
Magazeti ni Technolojia iliyozeeka
Watu wamehamia kwenye viganja full kuswipe
 
Back
Top Bottom