Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Wanajamvi
Kama mtakumbuka niliweka sauti ya Mohamed Said akizungumza na Radio
Niliwaomba musikilize kwa umakini sana maana kuna mambo ya upotoshaji

ni hii https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Sikiliza dakika 51-53 , ambapo Mohamed Said anamwambia Mtanganzaji kuwa kabala ya mwaka 1952 hakuna kiongozi wa TAA aliyemjua Mwalimu Nyerere

Hili si mara maoja, katika majadiliano haya Mohmaed amethibitisha kuwa Nyerere alianza siasa baada ya kupokelewa na Abdul Mwaka 1952.
Na mara zote amesema Nyerere aliingia Dar katika siasa mwaka 1952

Tumekuwa tunauliza sana kuhusu ushiriki wa Nyerere kama katibu wa tawi Tabora na kuhudhuria mkutano mkuu mwaka 1948. Tulisema haiwezekani katibu wa tawi kubwa Tabora asiwe Introduced kwa viongozi wa HQ.

Sasa naomba musikilize video hiyo katika dakika 51-54 halafu musome maneno ya Juma Mwapachu hapo chini yaliyoletwa na Mohamed Said mwenyewe

Msikilize Juma Mwapachu , anasema wazi kuwa Hamza Mwapachu ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA makao makuu kabla ya kuondoka kwenda Edinburgh kwa masomo

Hili ni tofauti kabisa na habari za Mohamed Said kuwa aliyemleta Nyerere mzobe mzobe ni Kasela Bantu na kumu introduce kwa Abdul Sykes na kwamba kabla ya hapo hakuna aliyewahi kumsikia au kumjua Nyerere! Fallacy ! Urongo mkubwa.

Kama huu si urongo Mohamed Said aje akanushe maneno ya Juma Mwapachu aliyoyaleta mwenyewe .

Hivyo tuna ushahidi mwingine kuwa TAA HQ walijua habari za Nyerere na si kuwa mtu wa kwanza alikuwa Abdul Sykes

Hapa unawezaona Mohamed alivyojitahidi kuficha sifa za Nyerere kwa gharama ya Abdul.

Haelezi ushiriki wa Nyerere kuanzia miaka ya nyuma, anachokifanya ni kumfanya Nyerere ni parasite aliyedondoka tu na kuwa kiongozi i.e ad hominem !

Mnaweza kuona jinsi gani sisi vichekesho tunasoma between the lines na kugundua makosa.

Kwa maneno mengine , si kuwa Mohamed hajui ukweli kuhusu Nyerere, anachotaka ni kumdhalilisha kwanza kwa gharama ya Abdul Sykes.

Hapa tunasema hapana si kweli na ushahidi ni huo hapo juu

Utashangaa Mohamed atakuja hapa na hadithi na picha, anachotakiwa ni kuomba radhi kwa kusema redion Nyerere hakuwahi kusika HQ kabla ya 1952 au akanushe maandiko ya Juma Mwapachu kuwa Hamza haku mu introduce Nyerere HQ
 
Asanteh Mkuu Nguruvi3 ... Ukosoaji wako ni wa kiwango cha lami...
 
Na walisaidia vipi harakati za uhuru hao wazee wako? Tumeona jinsi wazee wa Mohamed Said walivyompokea Nyerere, wakamuweka kwao.

Hao wako jee uliowataja?
 
Nguruvi3,
Soma kwa utulivi na nisikilize kwa utulivu.

Hili la kwanza.
Jambo la pili.

Maelezo ya Juma Mwapachu yana makubwa katika historia ya TANU.

Hivi yote hayo aliyoeleza na mimi kusherehesha kuhusu Ally Mwinyi
Tambwe
ulichoona wewe ni hilo la Nyerere kutofahamika New Street?

Hutaki kujua athari ya ''mole,'' wa serikali ya Kiiingereza ndani ya TANU?
Hutaki kujua wanaharakati wangapi waliponzeka na usaliti wa Mwinyi
Tambwe.

Ngoja nikufahamishe.

Kuna kuvamiwa kwa Rashid Ali Meli kwa kutoa fedha kusaidia safari ya
Nyerere ya kwanza UNO.

Halikadhali kuna kukamatwa kwa Idd Faiz Mafongo alipokwenda kuchukua
fedha za kumpeleka Nyerere UNO kutoka kwa Mwalimu Kihere Tanga.

Nakuwekea picha ya Idd Faiz Mafongo ni huyo wa kwanza kushoto, Sheikh
Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro
na Haruna
Taratibu
Dodoma miaka ya mwanzo ya kujenga TANU.

Yote haya si muhimu kwako ila la Nyerere basi?

Hutaki kujua Brendon Grimshaw alisema nini kuhusu Abdul Sykes baada
ya kuona magazeti ya TANU hawakuandika taazia yoyote katika kifo cha
Abdul Sykes?

Hutaki kujua mswada wa historia ya TANU ulioandikwa na Abdul Sykes na
Dr. Kleruu uko wapi na nini Abdul aliandika katika historia ile na kwa nini
ulikataliwa?

Hutaki kujua kwa nini gazeti la Africa Events lililomtaja Abdul kama muasisi
wa TANU lilikusanywa.

Hutaki kujua kwa nini baada ya miaka hiyo yote na haya yote mwishowe
Abdul na mdogo wake Ally wakatambuliwa kuwa ni katika wazalendo waliotoa
mchango mkubwa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa kuwa humjui Abdul mara kadhaa umekuwa ukiuliza kuhusu elimu yake.
Abdul alikuwa ''super bright student.''

Baba yangu ananambia kuwa yeye n Abdul waliaanza shule pamoja na darasa
moja Al Jamiatul Islamiyya Muslim School Dar es Salaam.

Anasema walianza kusoma Qur'an siku moja lakini Abdul alihitimu kabla ya wao
wote na ikiwa mwalimu wa Qur'an hakuja Abdul ndiye akiwasomesha wenzake.

Mwaka wa 1942 alitokea namba moja mtihani wa Cambridge na kupata nafasi ya
kuingia Makerere akiwa na miaka 18.

Waingereza wakamchukua, ''conscription,'' kwenda kusaidia kile walichokiita ''war
effort,'' akapelekwa Burma Vita Vya Pili Vya Dunia.

Rafiki yake Earle Seaton alimsukuma sana Abdul kurejea shule na mwaka wa 1953
alipata nafasi Princeton University Marekani lakini hakwenda.

Kuna barua kutoka kwa Seaton akimwandikia Abdul 1953 baada ya kupata nafasi
ambayo Seaton anamwambia Abdul kuwa atakapokuwa New Jersey awe anakwenda
UNO, New York kusikiliza, ''deliberations,'' kuhusu ''Mandate Territories.''

Kwa kuwa unakereka na picha zangu nataka ukereke zaidi nakuwekea picha nikiwa
New Jersey ujue kuwa mie si mtafiti uchwara:

Kutoka New New Jersey hadi New York Manhattan ilipo UN ni kama
unatoka Ubungo unakuja Mtaa wa Kipata.

Tutaendelea na mjadala In Shaallah.
 
Wanajamvi

Mnakasha umefikia mahali patamu sana.

1. Tunasubiri Mohamed Said atuletee nakala ya draft(rasimu) au katiba ya kuandika au kukopi iliyokuwepo, andikwa au tumiwa na Abdul Sykes kabla ya katiba iliyoandikwa/kopiwa na Nyerere.

2. Tunasubiri Mohamed Said atueleze kabla ya kutangazwa kwa TANU mwaka 1954, jina la TANU lilitumika katika mkutano au mkusanyiko gani ambao Adul Sykes au mwingine nje ya Nyerere

3. Halafu kuna sauti hii ya Mohamed Said katika dakika 51-53 akimueleza mtangazaji wa radio kuwa kabla ya mwaka 1952 hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere. Sikiliza hapa

https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Kisha usome maneno haya ya Juma Mwapachu aliyempa Mohamed Said atueletee kama zawadi. Lengo lilikuwa kuonyesha sisi 'vichekesho' hatujui na wala hatuna mawasiliano na watu wakubwa kama akina Mwapachu.

Hata hivyo, katika maandishi hayo tunapata habari nyingine ikihusiana na introduction iliyofanywa na Hamza Mwapachu kwa Nyerere katika kile alichosema TAA Leadership

Kumbuka TAA leadership wakati huo ilikuwa chini ya Abdul Sykes, hivyo Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa Abdul Sykes kama sehemu ya TAA leadership.

Soma hapa maneno ya Juma Mwapachu

''I still recall the visit vividly
. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''

Kwa faida ya wasomaji, tunaweka maneno ya Bakari Mwapachu katika tafsiri isiyo rasmi
Tunaomba radhi ikiwa kuna mapungudu yatakayojitokea. Bakari Mwapachu anasema hivi

''Bado nakumbuka kwa uyakinifu. Nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu na pamoja na kaka yangu Bakari tulilala sebuleni kuacha chumba kwa wageni wawili.

Abdulwahidi alikuwa Rais wa TAA na uongozi wa TAA pamoja na wanaharakati wa siasa wengi wao wakiwa waislam walitaka Abdul Sykes abaki kuwa Rais

Abdulwahid alikuwa tayari kumuafiki Hamza katika suala hilo katika ukweli kuwa ni Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA Dar es salaam mwaka 1949 kabla Nyerere hajaondoka kwenda chuo kikuu Edimburgh''

Ndipo tunakuja kutafuta ufafanuzi kwa Mohamed Said katika hoja ya 4 na 5

4. Mohamed Said , je bado unaamini kuwa kabla ya 1952 hakuna yoyote aliyewahi kumsikia Nyerere katika TAA HQ chini ya Abdulwahid Sykes?

5. Je, maneno ya Juma Mwapachu ni uzushi au ni ukweli?

6. MS ikdhihirika kuwa Juma Mwapachu (na amesema kwa ushidi) maneno yake yapo sahihi, je utaliomba radhi jamvi kwa upotoshaji?

Je, utawaomba radhi wasikilizaji uliowapotosha katika redio na lina utafanya hivyo?

7. Kama maneno yako ni nkweli, je utakuwa tayari kukanusha maneno ya Juma Mwapachu hapa jamvini na kutuomba radhi kwa kutuletea habari zisizo na ukweli?

Na mwisho, Mohamed ajibu hoja hizi, hatuwezi kuburuzwa tu tukubali hata upotoshaji eti kwavile tunataka kujua mengine.

Haina maana kujua mengine ikiwa yapo tusiyoyajua kama haya tunayomuuliza

Mohamed Said, tafadhali sana usihamishe mjadala na kukwepa hoja.

Tunataka kusahihisha historia ya kivukoni kwa ukamilifu wake.

Hatutaki kuwaacha vijana wamechanganyikiwa kwa hoja kinzani. Tutaendelea baada ya majibu haya, vinginevyo ukiri makosa kama tunavyokubali ya kivukoni.

Ahsante
 
Nguruvi3,
Hebu jitulize na usome kwa utulivu.
Aloandika habari za Abdul si Bakari Mwapachu ni mdogo wake Juma.

Hivi wewe una nini?
Tulia na usome kwa makini.

Tutafanyaje mjadala wa maana ikiwa kila ukiandika unachanganya mambo?
Nakupa muda ujitulize kisha tuendelee na mnakasha In Shaallah.
 
Hewalaa, ni kweli ni Juma Mwapachu aliyekuletea habari hiyo. Nimefanya editing ya hoja zangu kwa kuondoa jina Bakari na kuweka Juma, Mwapachu ikibaki pale pale,hoja ni hizi hapa chini

Wanajamvi

Mnakasha umefikia mahali patamu sana.

1. Tunasubiri Mohamed Said atuletee nakala ya draft(rasimu) au katiba ya kuandika au kukopi iliyokuwepo, andikwa au tumiwa na Abdul Sykes kabla ya katiba iliyoandikwa/kopiwa na Nyerere.

2. Tunasubiri Mohamed Said atueleze kabla ya kutangazwa kwa TANU mwaka 1954, jina la TANU lilitumika katika mkutano au mkusanyiko gani ambao Adul Sykes au mwingine nje ya Nyerere

3. Halafu kuna sauti hii ya Mohamed Said katika dakika 51-53 akimueleza mtangazaji wa radio kuwa kabla ya mwaka 1952 hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere. Sikiliza hapa

https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Kisha usome maneno haya ya Juma Mwapachu aliyempa Mohamed Said atueletee kama zawadi. Lengo lilikuwa kuonyesha sisi 'vichekesho' hatujui na wala hatuna mawasiliano na watu wakubwa kama akina Mwapachu.

Hata hivyo, katika maandishi hayo tunapata habari nyingine ikihusiana na introduction iliyofanywa na Hamza Mwapachu kwa Nyerere katika kile alichosema TAA Leadership

Kumbuka TAA leadership wakati huo ilikuwa chini ya Abdul Sykes, hivyo Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa Abdul Sykes kama sehemu ya TAA leadership.

Soma hapa maneno ya Juma Mwapachu

''I still recall the visit vividly
. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''

Kwa faida ya wasomaji, tunaweka maneno ya Juma Mwapachu katika tafsiri isiyo rasmi
Tunaomba radhi ikiwa kuna mapungufu yatakayojitokeza. Juma Mwapachu anasema hivi

''Bado nakumbuka kwa uyakinifu. Nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu na pamoja na kaka yangu Bakari tulilala sebuleni kuacha chumba kwa wageni wawili.

Abdulwahidi alikuwa Rais wa TAA na uongozi wa TAA pamoja na wanaharakati wa siasa wengi wao wakiwa waislam walitaka Abdul Sykes abaki kuwa Rais

Abdulwahid alikuwa tayari kumuafiki Hamza katika suala hilo katika ukweli kuwa ni Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA Dar es salaam mwaka 1949 kabla Nyerere hajaondoka kwenda chuo kikuu Edimburgh''

Ndipo tunakuja kutafuta ufafanuzi kwa Mohamed Said katika hoja ya 4 na 5

4. Mohamed Said , je bado unaamini kuwa kabla ya 1952 hakuna yoyote aliyewahi kumsikia Nyerere katika TAA HQ chini ya Abdulwahid Sykes?

5. Je, maneno ya Juma Mwapachu ni uzushi au ni ukweli?

6. Ikidhihirika J.Mwapachu maneno yake ni sahihi,utaliomba radhi jamvi kwa upotoshaji?

Je, utawaomba radhi wasikilizaji uliowapotosha katika redio na lini utafanya hivyo?

7. Kama maneno yako ni nkweli, je utakuwa tayari kukanusha maneno ya Juma Mwapachu hapa jamvini na kutuomba radhi kwa kutuletea habari zisizo na ukweli?

Na mwisho, Mohamed ajibu hoja hizi, hatuwezi kuburuzwa tu tukubali hata upotoshaji eti kwavile tunataka kujua mengine.

Haina maana kujua mengine ikiwa yapo tusiyoyajua kama haya tunayomuuliza

Mohamed Said, tafadhali sana usihamishe mjadala na kukwepa hoja.

Tunataka kusahihisha historia ya kivukoni kwa ukamilifu wake.

Hatutaki kuwaacha vijana wamechanganyikiwa kwa hoja kinzani.

Tutaendelea baada ya majibu, vinginevyo ukiri makosa kama tunavyokubali ya kivukoni.

Ahsante

.
 
Nimefurahishwa kwa namna unavyowapa darsa bila khiyana.

Wana mengi sana ya kujifunza na ndiyo maana wanajazana hapa huku wanajidai kuuliza kutokana na yale yale wanayojifunza kutoka kwako.

Nikiwauliza waliwahi kumsoma Mshume Kiyate (my hero) popote kabla ya kumsoma kwako, wanahaha na kuzidi kukatika matumbo.

Hakika darsa linanoga na Alama endelea kutupa darsa, hakuna asiyefaidika na darsa hili adhyim.

Wanaokuja na matusi na lugha chafu kama za huyu anayejiita Yericko Nyerere wana mengi sana ya kujifunza lakini uhasidi umewajaa...
 
Umekula uppercut moja mpaka umekiri kuwa hujui kitu, unababiababia tu. Nimecheka sana ulipokiri kuwa huna ulijualo (ki aina yako) mpaka imekubidi ukafute maandiko yako na kuweka sawa baada ya Alama Mohamed Said kukufunda.

Keep it up Alama Mohamed Said zinawaingia na wanazipokea wakipenda wasipende.
 
Faiza Fox sikujibu kwasababu nia yako ni 'kuokoa jahazi' ili tuingie katika malumbano yasiyo na maana uzi usonge na hoja zife. Hapana huko utabaki mwenyewe

Hoja kwa Mohamed Said zinabaki pale pale na ni hizi hapa chini

Nguruvi3,
Ama ingekuwa si kwa kuwa naburudika kufanya mjadala na wewe
mie muda mrefu ningelikwisha nyanyua mikono juu lakini nastarehe
kuongea na wewe.

Allah amekupa kipaji cha aina yake.

Majibu nimekupa kuhusu katiba ya TAA Political Subcommittee kuwa
nyaraka na microfilm zote hazionekani Maktaba ya CCM Ddodoma
na TNA.

Sikuishia hapo nimekueleza kuwa kabla yangu katiba hiyo ilitajwa na
Listowel mwaka wa 1965 na Pratt 1976.

Bado unataka nikuletee hiyo document.
Kama wewe hodari sana mbona huwauliza CCM nyaraka hizo zilipo?

Lakini ninastarehe katika mnakasha huu kwa kuwa natoa darsa na
wengi wansoma historia ambapo hawakupatapo kuisikia hata kwa
mbali.

Ndiyo maana narudi hapa tena na tena na tena.
Nakushukuru sana kwa hili.

Sasa nisikikize kwa makini na tuliza ubingo wako nikufunze mbinu
za ''critical analysis'' na kujifunza kusoma katikati ya mistari.

Sitakujibu hayo yote uliyoandika nitakujibu hayo tu ambayo umeweka
rangi nyekundu.

Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA 1949.

Akili yako mara moja imekwenda kuwa walikuja hadi New Street na
kuzungumza na Mwalimu Thomas Saudtz Plantan aliyekuwa rais na
Clement Mohamed Mtamila aliyekuwa katiibu wa TAA wakati ule.

Lakini ukweli ni kuwa Mwalimu Thomas Plantan na Clement Mtamila
walikuwa hawajapata kukutana na Nyerere hadi alipokuja kwa Abdul
Sykes
1952.

Inawezekana ujulisho huo ulikuwa wa salam za mdomo au wa barua.

Nakuwekea picha nikifanya mahojiano na Bi. Maunda Thoams Plantan
mtangazaji wa kwanza wa kike Tanganyika Sauti ya Dar es Salaam 1952
na mwalimu wa shule.

Mjukuu wa Affande Plantan na mtoto wa Mwalimu Thomas Saudtz
Plantan
.

Kushoto Bi. Maunda Plantan na Mwandishi

Katika mazungumzo yetu hakupatapo kunambia kuwa baba yake
alipata hata kwa siku moja kuonana na Nyerere.

Nimezungumza pia na Happy Mtamila hata mara moja hajanieleza
kama baba yake alipata kuonana na Nyerere kabla ya 1952.

Kulia Bi. Happy Mtamila na Mwandishi

Ningependa kukufahamisha tu kuwa uamuzi wa Nyerere kuacha kazi
ulifanyika nyumbani kwa Clement Mtamila Mtaa wa Kipata na Sikukuu.

Nyumba hii ilikuja kununuliwa na ukoo wa Baharoon ikavunjwa na
sasa ni ghorofa.

Nguruvi3,
Hivi ndivyo unavyonisaidia kupata fikra na kuiimarisha blog yangu:
Mohamed Said: WATOTO WA WAPIGANIA UHURU BI. MAUNDA PLANTAN, JUMA MWAPACHU, HAPPY MTAMILA NA KLEIST SYKES WANAPOWAKUMBUKA WAZEE WAO
 
Faiza Fox sikujibu kwasababu nia yako ni 'kuokoa jahazi' ili tuingie katika malumbano yasiyo na maana uzi usonge na hoja zife. Hapana huko utabaki mwenyewe

Hoja kwa Mohamed Said zinabaki pale pale na ni hizi hapa chini
Nguruvi3,
Ngoja nikueleze.

Mimi nasimama na wajuzi niko ugenini katika chuo na hadhira yote ngeni.

Napokea maswali na nayajibu sijatafuta mtu wa kuniokoa.
Maalim Faiza kaingia kukuelekeza wewe.

Huna moja ulijualo katika historia ya TANU na wala sikucheki kwani Allah
hakujaalia wewe uzaliwe na watu hawa.

Kuwa wazee wako walikuwa watazamaji wa harakati za kuunda TANU
hawakuomba iwe hivyo.
 
Maalim Faiza,
Kisa cha Mshume Kiyate ni cha kusikitisha sana.

Mzee Mshume yuko mahututi kalazwa Muhimbili anamuuliza mwanae
Kiyate Mshume, ''Mmemfahamisha Nyerere kuwa mimi nimelazwa?''

Amekufa Mshume Kiyate TANU haina habari.
Kazikwa nyumbani kwa nduguye aliyekuwa mpiga adhana wa Shadhli.

Hadi leo wamekataa kubadili jina la mtaa kwa heshima yake.
Lakini sisi hatutawasahau wazee wetu waliopigani uhuru wa Tanganyika.

Tutaendelea kuwarehemu kama hivi tufanyavyo juu ya kuwa Mshume
anakejeliwa na Nguruvi3 ati alikuwa ''muuza ng'onda.''

Kweli Mzee Mshume alikuwa muuza samaki lakini hizo fedha za samaki
ndizo alizokuwa akipeleka TANU kusaidia harakati.

Hao walioukuwa na kazi za kalamu na kuvaa stocking walifanya nini?
 
Faiza Fox sikujibu kwasababu nia yako ni 'kuokoa jahazi' ili tuingie katika malumbano yasiyo na maana uzi usonge na hoja zife. Hapana huko utabaki mwenyewe

Hoja kwa Mohamed Said zinabaki pale pale na ni hizi hapa chini

Niokowe jahazi wakati ni wewe uliyeomba poo na kurudi kufuta maandishi yako baada ya kufundwa na Alama Mohamed Said?

Unanchekesha.
 
Mkuu Nguruvi3 mnakasha umefika mahali patamu sana jambo moja lililowazi kabisa usitegemee kupata majibu stahiki kutoka kundi la Ustaadhi Mohamed Said na kundi lake.
 
So sad.

Tungeyajuwaje yote haya kwa historia ya kivukoni!?

Hilo swali ni kwa Nguruvi3 And company.
 
Mkuu Nguruvi3 fikiria mtu anaendesha siasa za misikitini halafu akichukuliwa hatua unasema huo ni uonevu ebo hawa watu Mwl Nyerere angewaendekeza Tanzania ingekuwa nchi vipande vipande.Kati ya makosa makubwa Mwl Nyerere aliyowahi kufanya ni kutokuchukua mkondo wa Karume.
 
Ngongo,
Tatizo lenu hamuijui historia ya TANU.
Uhuru wa Tanganyika ulipiganiwa misikitini.

Sasa cha ajabu kipi hata unashangaa?
Sheikh Hassan bin Amir anadarsisha huku kadi za TANU anazo pembeni.

Au huyajui haya?

Mtoro Rehani kakatiwa kadi ya TANU ndani ya msikiti na Sheikh Hassan bin
Amir.

Hivi ndivyo wazee wetu walivyomtoa mkoloni Tanganyika.
Ikiwa historia hii hamuifahamu ulizeni mtaelezwa.

Hayo ya Karume yanahitaji uzi wa kujitegemea ufungue In Shaallah nitakuja
kusomesha.

Chembelecho Maalim Faiza: Elimu bila khiyana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…