Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya


Ukiisoma vizuri historia ya kweli ya harakati za Uhuru wa Tanganyika utakuta ilifikia mahala mpaka Nyerere akifungishwa swaum na wazee wa Kiislam wana harakati.

Unanikumbusha Darwesh maarufu sana kama "Sharrif Kibendera" enzi za Nyerere, alikuwa akishatowa daawa pale mnazi mmoja anaanza kuomba Dua, na moja ya dua zake akisema "tumuombee Nyerere asilimu bila ya hivyo hana kheri yoyote. Eeh Mwenye Mungu mtowe Nyerere katika kiza kikubwa kilichomgubika na kumuingiza kwenye nuru ya milele eeh Mwenyezi Mungu nisameh kwa kumwombea Nyerere kama ulivyomsameh Mtume Muhammad kwa kumwombea Abu Jahil..."

Hakika ni dua nzito sana kwa mwenye uelewa.
 
Vema hilo la kufunga swaumu vyema alilizungumza yeye mwenyewe Nyerere, vinginevyo yangeanza marumbano na mabishano mpaka mwisho wa dunia.
 

OK, Sheikh!
My apologies to your late father. Nilikosea kuandikakuwa ni baba yako ndio aliwekwa kizuizini, I should have written Babu yako.

Sasa endelea.
 
Mkuu Nguruvi3 mnakasha umefika mahali patamu sana jambo moja lililowazi kabisa usitegemee kupata majibu stahiki kutoka kundi la Ustaadhi Mohamed Said na kundi lake.

Ushauri mzuri sana, huyu Mzee ni mbishi sana japo simlaumu yeye. Ni kwasababu Jamii yake nzima inayopenda kusikia ya kwake inampa kichwa. Huyu mzee anapenda kujisifia na kusifiwa lakini hajui wamsifuo ni wale wasiojua chochote na wanaomeza kama yalivyo ilimladi yametoka kwake au kwa mwenzao.
 

Kama u mkweli hebu tuwekee nukuu zake zenye kukufanya umuite "mbishi".
 
Ilimladi = ilimradi
 
OK, Sheikh!
My apologies to your late father. Nilikosea kuandikakuwa ni baba yako ndio aliwekwa kizuizini, I should have written Babu yako.

Sasa endelea.

Unapaswa kuomba msamaha kwa kosa ulilolitunga la uongo la sababu ya kuwekwa kizuizini. Unajifanya huelewi au ni punguani wa ukweli?
 

Hahahaaaaa, mzee Mohammed Said umenifurahisha sana. Hakuna anayekupinga kwamba wazee walikuwa Dar es Salam walipigania uhuru wa Tanganyika bila mafanikio hadi walipomkaribisha msomi, Julius mjukuu wa Burito aliyepewa jina la Kambarange siku ya Kuzaliwa kwake! Wazee hao wa Dar es Salaam ni lazima walikuwa waislam kwa sababu ya namna waislam walivyokuwa wame itawala pwani yote na kufanikiwa kuwabadili hao wazee wako kutoka dini zao za jadi kuja Uislam! Kitu kimoja mzee wangu unachotakiwa kufaham, ni makosa makubwa sana kuelezea historia ya TANU kwa mtazamo wa dini! Hizi dini ni zao la ukoloni!! Hivi hata hili hulijui!? Kwanini bado unafunga akili yako ndani ya huo ukoloni wa kiarabu!? Labda ni kwambie tu, kuna watu wanaona mbali na huyo Nyerere ni mmoja wao! Kutowapa heshima hao Wazee wako ndani ya Serikali huenda ni kutokana na kuona mbali kitu ambacho kingetokea mbele ya safari! Hivi unadhani uko sahihi namna unavyoelezea hii historia yako!? Akija mwingine anaandika historia kwa mtazamo wa kusema Sykes alikuwa Msuni hivyo wapigania uhuru wa mwanzo walikuwa wasuni na walipeana kadi kwenye mabalaza ya kisuni au Akija akasema alikuwa mshia, n. k, Watu tunapinga kuandika historia kwa mtazamo wa dini fulani kwasababu bado huko naweza sema nikuandika historia ndani ya ukoloni wa kifikra.
 
So sad.

Tungeyajuwaje yote haya kwa historia ya kivukoni!?

Hilo swali ni kwa Nguruvi3 And company.

Hapo ndo uwezo wa kupambanua mambo unapotofautiana na nyie wenzetu, hivi mlitegemea baada ya uhuru Nyerere aanze kuhudumia familia za watu au ahudumia nchi!? Nchi ingeendeshwaje kwa kusubiri hisani!? Mtu amelazwa hospitalini sehemu sahihi kabisa, mlitaka aache shughuli nyingine za kujenga nchi aende hispitali!?
 

Mzee Mohammed, wewe ni mtu mzima bana hebu shirikisha akili na busara za ukubwa japo kidogo. Achana na ushabiki bana!! Hivi kweli na wewe unaandika haya!?! Kwa hiyo ulitka Nyerere aache shughuli za kujenga nchi yenye watu maelfu kwa maelfu aende kumuhudumiwa huyu mzee wetu hospitali!? Hapakuwa na madaktari pale!? Nyerere angeenda au angejulishwa angeweza kuzuia Mungu asimuite huyu mzee wetu!? Hapa ndo watu wanapoanza kuchallenge hicho unachoita historia ya kweli!
 
Unapaswa kuomba msamaha kwa kosa ulilolitunga la uongo la sababu ya kuwekwa kizuizini. Unajifanya huelewi au ni punguani wa ukweli?

Hakika Faiza kichwa chako kimejaa pumba cz mkuu hapo juu kaomba msamaha lkn wwe jinsi ulivyokua punguani unamtaka aombe msahama tena Ficha uzembe wako
 
Wanajamvi msione mzee wetu amepoteza uelekeo anasema hovyo, tumemshika pabaya, tumethibitisha urongo na tunazidi kuonyesha kile tunachosema historia yake ni hisia juu ya Nyerere.

Kuna sauti yake na maandishi ya J.Mwapachu yanayoeleza kwa uzuri kabisa kuhusu hili. Kisha yakafuata maswali 7 aliyoshindwa kujibu

Anasema anazungumza ugenini kwa wasio na background hapa hawezi kujibu hoja. Mvumilieni mzee mkiona anapoteza network na kualika akina Faiza waje kumuokoa kwa matusi. Msiende huko kwa Faiza, tubaki na mzee wetu

Anaposema anasimama ugenini na kujibu maswali, ana maana anasimama ulaya! dalili njema za inferiority complex.

Mohamed tulia maana ndio kwanza kazi inaanza na msiumari zaidi yaja.
 
Mkuu Nguruvi3 mnakasha umefika mahali patamu sana jambo moja lililowazi kabisa usitegemee kupata majibu stahiki kutoka kundi la Ustaadhi Mohamed Said na kundi lake.
Amesubiri akina Faiza wakamsaidia kutukana amekwepa maswali.

Ni hivi, katika radio Nur Alama Mohamed amesema wazi Nyerere hakusikika wala kujulikana kwa uongozi wa TAA kabla ya mwaka 1952.

Huyu alikuwa hewani na mwandishi alimuuliza vizuri. Alikuwa anatoa darsa

Jana bila kutegemea na kwa rehma za mwenyezi mungu katuletea kile alichoita zawadi kutoka kwa Juma Mwapachu.

Hakika imegeuka kuwa zawadi maana Juma anasema ' Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA (TAA leadership) kabla ya kuondoka

Mzee kakwama leo anarudi kusema ni kweli alitambulishwa kwa Platan

Tunamuomba aomber radio Nur Radhi kwa kupotosha wasikilizaji kwa habari hiyo.

Kama anaona yupo sahihi atumei fursa hii kukanusha maneno ya Juma Mwapachu

Hatuhitaji hadithi za 'hujui, najua , nilikuwa ulaya n.k.'

Tunamtaka aombe radhi kwa kusamabaza uongo kwa heshima yake kitaaluma na kiumri.

Nitawashangaa sana Prof Shivji na Prof Saida H. Othaman kama watachakua maneno ya huyu mzee bila kuyachuja. Wanaweza ishia mahali pabaya sana

Mohamed Said, njia rahisi ni kuomba radhi ili twende mbele

Huna katiba uliyosema aliandika Abdul Sykes
Huna evidence ya mkutano/ Mkusanyiko aliotumia neno TANU kabla ya Nyerere

Sasa umekiri kwa kauli kuwa Nyerere alijulikana TAA kabla ya 1952.

Ulijitahidi kumfuta Cecil Matola tukakataa
Ukajitahidi kufuta historia ya Nyerere , Juma Mwapachu kaja na kusema urongo

Kaa mkao mzuri, narudisha kile chuma !
 
Kwa wasomaji mliokuta Mohamed Said anaokolewa na matusi ya akina Faiza, haya ndiyo yaliyopo mbele yetu. Mkiona mzee anahangaika, anasema hovyo, anatukuna basi baadhi ya sababu ni hizi hapa chini



1. Tunasubiri Mohamed Said atuletee nakala ya draft(rasimu) au katiba ya kuandika au kukopi iliyokuwepo, andikwa au tumiwa na Abdul Sykes kabla ya katiba iliyoandikwa/kopiwa na Nyerere.

2. Tunasubiri Mohamed Said atueleze kabla ya kutangazwa kwa TANU mwaka 1954, jina la TANU lilitumika katika mkutano au mkusanyiko gani ambao Adul Sykes au mwingine nje ya Nyerere

3. Halafu kuna sauti hii ya Mohamed Said katika dakika 51-53 akimueleza mtangazaji wa radio kuwa kabla ya mwaka 1952 hakuna aliyemsikia au kumjua Nyerere. Sikiliza hapa

https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Kisha usome maneno haya ya Juma Mwapachu aliyempa Mohamed Said atueletee kama zawadi. Lengo lilikuwa kuonyesha sisi 'vichekesho' hatujui na wala hatuna mawasiliano na watu wakubwa kama akina Mwapachu.

Hata hivyo, katika maandishi hayo tunapata habari nyingine ikihusiana na introduction iliyofanywa na Hamza Mwapachu kwa Nyerere katika kile alichosema TAA Leadership

Kumbuka TAA leadership wakati huo ilikuwa chini ya Abdul Sykes, hivyo Hamza Mwapachu alimjulisha Nyerere kwa Abdul Sykes kama sehemu ya TAA leadership.

Soma hapa maneno ya Juma Mwapachu

''I still recall the visit vividly
. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''

Kwa faida ya wasomaji, tunaweka maneno ya Juma Mwapachu katika tafsiri isiyo rasmi
Tunaomba radhi ikiwa kuna mapungufu yatakayojitokeza. Juma Mwapachu anasema hivi


''Bado nakumbuka kwa uyakinifu. Nilikuwa mwanafunzi wa darasa la tatu na pamoja na kaka yangu Bakari tulilala sebuleni kuacha chumba kwa wageni wawili.

Abdulwahidi alikuwa Rais wa TAA na uongozi wa TAA pamoja na wanaharakati wa siasa wengi wao wakiwa waislam walitaka Abdul Sykes abaki kuwa Rais

Abdulwahid alikuwa tayari kumuafiki Hamza katika suala hilo katika ukweli kuwa ni Hamza ndiye aliyemtambulisha Nyerere kwa uongozi wa TAA Dar es salaam mwaka 1949 kabla Nyerere hajaondoka kwenda chuo kikuu Edimburgh''


Ndipo tunakuja kutafuta ufafanuzi kwa Mohamed Said katika hoja ya 4 na 5

4. Mohamed Said , je bado unaamini kuwa kabla ya 1952 hakuna yoyote aliyewahi kumsikia Nyerere katika TAA HQ chini ya Abdulwahid Sykes?

5. Je, maneno ya Juma Mwapachu ni uzushi au ni ukweli?

6. Ikidhihirika J.Mwapachu maneno yake ni sahihi,utaliomba radhi jamvi kwa upotoshaji?

Je, utawaomba radhi wasikilizaji uliowapotosha katika redio na lini utafanya hivyo?

7. Kama maneno yako ni nkweli, je utakuwa tayari kukanusha maneno ya Juma Mwapachu hapa jamvini na kutuomba radhi kwa kutuletea habari zisizo na ukweli?

Na mwisho, Mohamed ajibu hoja hizi, hatuwezi kuburuzwa tu tukubali hata upotoshaji eti kwavile tunataka kujua mengine.

Haina maana kujua mengine ikiwa yapo tusiyoyajua kama haya tunayomuuliza

Mohamed Said, tafadhali sana usihamishe mjadala na kukwepa hoja.

Tunataka kusahihisha historia ya kivukoni kwa ukamilifu wake.

Hatutaki kuwaacha vijana wamechanganyikiwa kwa hoja kinzani.

Tutaendelea baada ya majibu, vinginevyo ukiri makosa kama tunavyokubali ya kivukoni.

Ahsante
 
Sikiliza kwa makini dakika 51-53, Mohamed Said anaunguruma katika radio akisema hakuna aliyewahi kumsikia au kumjua Nyerere TAA kabla ya kujulishwa kwa Abdulwahid Sykes 1952
https://soundcloud.com/mwinyimadi/sheikh-hassan-bin-amir-nur-fm

Hapa chini mtoto wa mzee Mwapachu, Juma Mwapachu anakuja na kusema 'stop Mohamed, muongo mkubwa wewe'' hayo si maneno ya Nguruvi ni ya Juma Mwapachu, msome hapa chini

''I still recall the visit vividly. I was a standard three pupil then and together with my brother Bakari had to sleep in the sitting room leaving our bedroom to the two guests.

Abdul Sykes was then President of TAA and the TAA leadership plus Dar-based political activists who were predominantly Moslems wanted Abdul Sykes to retain the Presidency.

Abdul was eager to secure Hamza's position on the matter given the fact that it was Hamza who introduced Nyerere to the TAA leadership in Dar back in 1949 before Nyerere left for Edinburgh University''


Mohamed Said

Kaombe radio radhi ili nayo iombe wasikilizaji radhi. Ni uungwana

La sivyo mwambie Juma Mwapachu yeye ndiye mrongo

Kama yote mawili ni magumu, fanya jepesi kabisa liombe jamvi radhi
 
Uncle...
Nisome mimi kisha soma hizo ''bana,'' zako utafahamu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…