Kaka
JF-Expert Member
- Nov 22, 2006
- 745
- 372
Kaka Nguruvi3 mimi ninajifunza kwenye barza hii. Kwa wasaa wako, ninaomba utuwekee hapa mchakato aliopitia Mwl. Nyerere katika kuandika katiba ya kwanza "ya kiuweledi" ya Chama cha siasa ili nijifunze zaidi. Ahsante.N sifa nyingine ya mnafiki ni kukcheka aikuchukia. Kusifu akikung'ong'a
Huwezi kumtukana Nyerere ukasema unamheshimu !
Huwezi kuwatukana wazanzibar ukajificha nyuma ya Uislam
Vyovyote iwavyo, Nyerere ni smart. Unawajua wajumbe wa LEGCO?
Historia ya TANU kujulikana ni jambo jema kabisa.
Hata hivyo, historia haiwezi kubadilishwa kama ilivyokuwa.
Nyerere alibadilisha mtazamo wa siasa za Tanganyika.
Aliongoza mapambano dhidi ya mkoloni, alipewa uhuru wa nchi hii na mwingereza uwanja wa Taifa. Aliongoza kwa miaka 20
Kuanzia ujana wake alionekana smart,Makerere, Tabora hadi Edinburgh etc
Umahiri wake ulivuka mipaka na kuwagusa watu wengine
Nyerere alikuwa mwenyekiti wa front-line states kupinga ubaguzi na uonevu
Alikuwa kiongozi wa AU na statesman wa Afrika.
Huko UN wanamtambua kwa weledi na misimamo yake thabiti
Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi 6 waliounda kamati ya 'disarmament'
Na alikuwa mjumbe wa South-south commission
Kila siku anatajwa katika jamii na ni reference ya uongozi na viongozi
Anajulikana kila kona ya nchi hii licha ya kuwa kaburini miaka zaidi ya 10
Anajulikana Afrika na duniani kwa heshima zake, si kupakwa mafuta ya lazima
Pazia lake halifungwi kwa historia ya mtu mwingine. Na hakuna anayewekwa katika mizani ya siasa za nchi hii katika miaka ya 1900 na Nyerere.Hakuna
Pazia la Nyerere halifungwi na maandishi ya kinafiki! Umma umetambua sasa
Nyerere alikuja, akawaelimisha, akawaongoza!
Akabadili siasa za masoko na chini ya miembe kuwa za kisasa.
Aliandika katiba ya kwanza ya siasa!
Hakuna mwingine aliyewahii kuandika katiba ya chama cha siasa! Hakuna
Ukimlinganisha Nyerere na Abdul unamtafutia dhalili!
Abdul halingani na Nyerere! Nitty gritty
Ni kidonge kichungu huna budi kukimeza
Ahsante
Kaka.