Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Unachoambiwa una udini ni kuona kwamba Waislam wanaonewa japo walipigania uhuru wa Tanganyika pengine kuliko dini zingine. Hutaki kuona sababu za ndani zinazorudisha nyuma harakati za Waislam kupiga hatua ambazo zinatokana na wao wenyewe!
Mkuu waislam wameonewa tokea mkoloni mreno mjerumani na muengereza.
Ndio maana ktk harakati za kupigania uhuru wa tanganyika waislam walijitokeza kwa wingi sana na hawakusita kufanya siasa miskitini na kushirikisha mamufti na mashekhe ktk mbio hizo.
Utengano wetu ni wa kihistoria na kimfumo.
Labda tulifanikiwa kumuondowa mkoloni lakini mfumo bado unatutesa.
Lakini chakufurahisha ni hii changamoto muayo tupa ya kutukebehi hii itatufanya tujiweke sawa na kuondowa mfumo kama tulivyo muondowa muasisi wa mfumo mkoloni.
 
Kuna barabara yake.
 
Je? Familia hii ya mzee wetu na mwanaharakti Abdulwahid sykes ndo hii hii na huyu msanii wa sasa aitwae dully sykes?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa walikuwa ni matajiri wa miaka hiyo pamoja na kuujenga mfumo walisaidia Sana Mambo yasikwame kifedha .magari .na sehemu za kulala kwa wageni .pia baada ya kufanikisha walibaki kwenye biashara zao .
 
Kwasababu wenzetu wanaweka kumbukumbu. Hata Ulaya historia kubwa tulipiga hamu baada ya Roman Empire kwani ndiyo ilisambaza ustaarabu wa kusoma na kuandika.
 
Kwasababu wenzetu wanaweka kumbukumbu. Hata Ulaya historia kubwa tulipiga hamu baada ya Roman Empire kwani ndiyo ilisambaza ustaarabu wa kusoma na kuandika.
Kweli kabisa, Roman Empire ilisambaza "ustaarabu" (Arabs influence).

Naunga mkono hoja.
 
Kweli kabisa, Roman Empire ilisambaza "ustaarabu" (Arabs influence).

Naunga mkono hoja.
Ni kweli literacy iliannza kwa Wagiriki, Waarabu walianza number lakini Romans walisambaza elimu kote walikotawala.
 
Ni kweli literacy iliannza kwa Wagiriki, Waarabu walianza number lakini Romans walisambaza elimu kote walikotawala.
Umebadili kauli yako ya mwanzo kuwa Roman Empire walisambaza "ustaarabu"?

Soma kidogo historia ya kwenu hapa useme lugha ipi ya kusoma na kuandika ilifika hapa kwa mababu zako kwanza? Tukipata na kukubaliana hilo halafu tuhamie huko kwa Warumi.

Kuna post leo nimeisoma kuna wageni wa kizungu walikuja wakawashangaa Watanzania, wamewakuta wanaijuwa historia ya Ulaya kuliko ya kwao. Wewe unayakinisha.
 
Historia ya Mohamed Said kuhusu Abdul Sykes na Nyerere ina matobo mengi sana.
 
Historia ya Mohamed Said kuhusu Abdul Sykes na Nyerere ina matobo mengi sana.
Yoda,
Usitumie neno, "kususa."
Ikiwa unaona matundu katika historia ya Abdul Sykes kama nilivyoieleza siwezi kukuzuia.

Kwa nini hujiulizi iweje kafutwa katika historia ya TANU?
Ukiwa na jibu tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…