Uncle...
Inawezekana ukaona kosa kuandika historia ya Waislam wa Tanganyika.
Ndiyo ubinadamu ulivyo, ''one man's meat is another man's poison.''
Mimi kwangu si kosa na ndiyo maana nikakujibu kuwa soma anuani ya
kitabu changu.
Inawezekana wewe hujui lakini kuna vitabu vingi tu vilivyoandika historia
na mengi ya Waislam wa Tanganyika.
Katika vitabu maarufu ni hiki cha Augustus Nimitz: Islam and Politics in
East Africa.
Kipo pia kitabu cha P van Bergen: Religion and Development in Tanzania.
Kipo kitabu kinachoeleza habari za Kanisa Katoliki cha John Sivalon: Kanisa
Katoliki na Siasa ya Tanzania Bara 1953 Hadi 1985.
Hapana ubaya kuandika historia kama niliyoandika mimi kwani ni jambo la
kawaida katika usomi.
Asikutishe mtu.
Hayo mengine sitoyagusa kwa kuwa unaandika kitu usichokijua.
Muulize Dr. Mkanachi kuhusu historia hii.
Wakati alipokuwa anaandika tasnifu yake alikuja kujadiliana na mimi.
Mengine itapendeza yatoke kinywani kwake.
Salaam Mzee wangu Mohamed Said
Naomba nichangie kidogo kwenye hii post yako.
Mimi nakubaliana sana na wewe kwenye kuandika Historia mbalimbali, iwe ya Wa Kristo, Waislaaam, wachaga, wakurya kama Mimi etc.
Nachokiona hapa inakuwa nongwa kwa wewe kuandika Historia ya Tanganyika na ukai link na wazee wetu wa Dar es Salaam au ukai link na waislaam katika mchango wao kwenye kupigania uhuru. Kwangu Mimi hilo sio Tatizo.
Vijana na wasomi wengine, historia ni swala pana sana, Vijana tungetakiwa kujifunza kupitia wewe Mzee Mohamed Said na watu wanaweza kuandika Historia mbali mbali za Tanganyika na Zanzibar yetu. Na hapo watu mbalimbali wengekuja ku kufanya constructive critics kwenye hizo historia mpya.
Shida ya wengi ni kutotaka kujifunza na kubaki kuwa wabishi tu. Kuna mtu anaitwa Nguruvi3, yeye anasema mbona mzee Mohamed Said hujamtaja Cecil Matola, sasa Mzee Said Mohamed anamweleza, mimi sina information za kutosha za kuweza kuandika Historia ya huyo mtu kwa hiyo siwezi kumsemelea vizuri, lakini kama wewe Nguruvi3 unazo information zake basi sio vibaya ukaweka hapa hili tujadili, lakini Nguruvi3 anazidi tu kuwa mbishi.
Jamani kama kuna mtu ana history ya wachaga juu ya kutafuta uhuru sio vibaya akaandika history, hakuna tatizo hapo. Au kama kuna mtu anajua mchango wa watu wa mbeya si aandike?
Kwa mfano Mimi ni mkurya, lakini Sijui history ya wakurya katika kupigania uhuru, lakini akitokea mtu akaandika, natumaini utakuwa mjadala mzuri sana Pia.
Au kama kuna mtu anajua historia ya Abdul Sykes sio vibaya akaandika. Kupitia hapo ndio wasomi anaweza fanya mdahalo. Sasa Mzee Mohamed Said ameandika historia ya Abdul Sykes kadiri alivyojaliwa kumfahamu. Sasa kama kuna mtu mwingine anafahamu historia mbadala ya Abdul Sykes anaruhusiwa kuiweka hapa na tukaijadili, lakini si jambo la busara ubaki unabisha tu bila kuleta "new history ya Abdul Sykes"
Nadhani tuwe tunamkosoa mzee Mohamed Said with new evidences. Na hivi ndivyo wasomi wanavyofanya book review. Nina kosoa kitabu cha Mzee Mohamed Said kwa kutoa references and evidences. Lakini unapobakia kuleta unabisha tu kwa maneno bila evidence inakuwa haina maana kabisa, bora ukae kimya tu.