Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Umesahau na watoza ushuru & waangalizi wa usafi sokoni.
Ngongo,
Nimekujibuni vyema, kwa adabu na taadhima.
Lakini nyie ndugu zanguni kwenu uungwana ni kitu adimu na ghali kwenu.

Jibu naliweka hapo chini na hili ni kutoka kwenye blog yangu:
Mohamed Said: KUTOKA JF: MWALIMU NYERERE NA MCHEZO WA BAO

KUTOKA JF: MWALIMU NYERERE NA MCHEZO WA BAO
Mkuu usitegemee upate historia
Nzuri kwa maalim muddy zaidi ya majina ya wacheza bao na wauza Samaki tu ndivyo utapata kwake

Nyerere_bao_butiama.jpg

Wembeee,
Kwani ndugu yangu mtu ikiwa kazi yake ni kuuza samaki ndiyo
hairuhusiwi kuandika makubwa aliyochangia katika jamii?

Au mtu akiwa anacheza bao ndiyo yeye keshapoteza heshima
yake na hastahili kutajwa?

Mwalimu Nyerere alipokuwa mtoto mdogo siku moja chifu wa
jirani alimtembelea Chief Burito akamkuta Nyerere yuko nje
anacheza bao.

Yule chifu akamwambia Nyerere hebu cheza na mimi.
Hii ilikuwa katika njia ya mtu mzima kufanya maskhara na mtoto.

Yule chifu alipata mshtuko.
Mwalimu Nyerere alimfunga.

Alipokuwa faragha na Chief Burito Nyerere akamwambia huyu
mtoto hebu mpeleke shule akasome kwani ana akili sana kanifunga
bao hapo nje.

Hizi habari ziko katika kitabu cha Morlon (2015).
Kinapatikana Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.

Kama wapendavyo kusema Waingereza, ''The rest is history.''
Nyerere alikuwa mcheza bao maisha yake yote.

Babu yangu aikuwa mcheza bao maisha yake yote na wazee wangu
wengine wengi tu walikuwa wacheza bao.

Mwanzoni nilidhani wewe ni muungwana na kijana ulieleka sawa kumbe
nilikosea.

Prof. Juma Kapuya alikwenda Butiama akamkuta Mwalimu Nyerere
kwenye bao.

Mwalimu akanyanyua kichwa chake akamwambia Kapuya, ''Kaa hapo
nikufunge kama mtoto mdogo.''

Kapuya hakuthubutu.

Dar es Salaam Mtaa wa Mafia na Kongo karibu na nyumba ya Mzee Maneno
Kilongora
kulikuwa na barza kubwa ya bao.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Tabora
alikuwa akenda pale kushindana na mabingwa wenzake.

Bao ni moja ya mila zetu.
Kama ilivyo kwenu kwenda kilabuni kunywa pombe za kienyeji.

Msome babu yangu ''Mcheza Bao,'' hapo chini uone nini alifanya katika
historia ya Tanganyika:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
 
Walimpeleka kwa nini, na kwann hawakwenda wao!

Jibu ni raisi, kwa sababu ya upeo wao mdogo, wasingeweza kuzungumza chochote
Unataka kujua tukujuze au unataka kuleta kibri tu kitoto kifupi tu hyo hotuba aliyoenda kusoma mwalim nyerere UNO imeandikwa na hao wenyewe upeo mdogo km unavyowaita kwa ukosefu wako wa adabu hotuba iliandikwa na mashujaa kina sheikh hassan bin Amir abdulwahid nk walimpaleka mwalim na kumuweka mwalim mbele kuhepusha kuonekana wao ni wadini maana asilimia 99 walikuwa ni waislam
 
Unafikir MWALIMU, aliyekuwa na DEGREE ya Makerere by then, angeweza kuandikiwa hotuba na hao waungwana!?
 
Mbona ameandikiwa na kufanyiwa mengi sna pamoja hyo DEGREE yke tatizo lako kubwa unaleta ubishi uku ukiwa mvivu wakusoma hta hivyo vitabu alivyoandika mwalim nyerere mwenyewe
6657a1b74cfcf11996ea3fbce896da71.jpg
mmoja wa watu wa mwanzo kuitangaza TANU wakt mwalim nyerere akiwa musoma na muandishi hotuba zake mwalim nyerere ktk majukwaa ya kisiasa Bi TITI MOHAMED
 
ahsante mzee mohamedi kwa simulizi nzuri ,natafuta historia ya mangi kisarika picha zao pamoja na simulizi za kazi zao Enzi hizo .ahsante
 
Unafikir MWALIMU, aliyekuwa na DEGREE ya Makerere by then, angeweza kuandikiwa hotuba na hao waungwana!?
Ndalikawe,
Hili suala la hotuba ya UNO kiasi cha miaka miwili nyuma ilizua
mjadala mkali sana.

Ile hotuba hakuandikiwa Nyerere wala hakikumkusudia yeye.

Yote yale yalikuwa katika Constitutional Development Committee
ya Gavana Edward Twining ambayo hata hivyo mapendekezo
hayo serikali yake iliyakataa.

Mapendekezo haya yaliandikwa mwaka wa 1950 na TAA Political
Subcommittee ambayo wajumbe wake walikuwa Sheikh Hassan
bin Amir, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo,
Stephen Mhando
na John Rupia.

Mapendekezo haya yalijadiliwa mwaka wa 1954 kwenye mkutano
wa kuunda TANU.

Habari zaidi ya waraka huu unaweza ukazipata kwa Listowel (1965)
na Pratt (1976).

Lakini ukitaka habari za ndani kabisa kuhusu hotuba hiyo ya UNO itabidi
umsome mwenyewe Abdul Sykes (1951).

Abdul atakueleza vipi alimleta Earle Seaton katika kamati ile ya TAA ili
asaidie katika mambo ya sheria yaliyokuwa yakiwakabili wao kama
Mandate Territory.

Kwenye kitabu cha Abdul haya yote nimeyaeleza kwa kirefu sana.
Naelewa taharuki na mshtuko uliokufika.

Wewe si wa kwanza.

Mwalimu wangu Prof. Haroub yeye aliumia sana na alikwenda hadi kwa
Mwalimu kutafuta ukweli wa yale niliyoandika katika kitabu cha Abdul
Sykes
.

Mwenyezi Mungu ana njia za ajabu sana.

Katika uhai wake wote baada ya uhuru kupatikana na akisikia TAA inakashfiwa
kuwa kilikuwa chama cha starehe na nini...

Abdul hakuwa anasema kitu hadi anaingia kaburini.
Leo Abdul Sykes anazungumza na sisi kutoka kaburini.
 
Mbona ameandikiwa na kufanyiwa mengi sna pamoja hyo DEGREE yke tatizo lako kubwa unaleta ubishi uku ukiwa mvivu wakusoma hta hivyo vitabu alivyoandika mwalim nyerere mwenyewe
6657a1b74cfcf11996ea3fbce896da71.jpg
mmoja wa watu wa mwanzo kuitangaza TANU wakt mwalim nyerere akiwa musoma na muandishi hotuba zake mwalim nyerere ktk majukwaa ya kisiasa Bi TITI MOHAMED
Rubawa,
TANU ilikuwa na wazungumzaji wakuu watatu katika siku za mwanzo.
Mwalimu Nyerere, Bi. Titi Mohamed na Sheikh Suleiman Takadir.

Baada ya Sheikh Suleiman Takadir kugombana na Nyerere mwaka wa
1958 na kufukuzwa chama wazungumzaji wakabaki wawili Nyerere na
Titi.

Wote hawa wawili walikuwa ''brilliant orators,'' wazungumzaji wazuri sana.

Mimi nimemfanyia mahojiano Bi. Titi na nimesikia katika mazungumzo
ya kawaida.

Mwalimu alikuwa akiishiwa maneno wakati mwingine.
Mwalimu alikuwa akipewa maneno ya kusema na Bi. Titi.
 
Asalaam Aleykum Maalim wangu Mohamed Said,
Ahsante kwa darsa nami kila nikipata nafasi hupitia kwenye huu Uzi maana najifunza Mambo mapya mengi shukuran. Maalim naomba niweke link hapa ya UZI nimeukuta humu jamvini kwa kweli nimeshangazwa na hilo bandiko.

“Ashakum si matusi" Maalim mleta huo uzi huwa anakuita muongo jee yeye hapa ameandika nini?
Uongo wa Historia ya Afrika na Waafrika itajibiwa na muafrika
eti kaandika kitabu kukujibu amesahau hili bandiko?
Al-Alama Ritz naomba uione
Saidat FaizaFoxy naomba upitie
 
Mtebetini,
Mwaka wa 2003 katika mkutano wa Kimataifa Kampala, Uganda ambao kati ya
waliowasilisha mada alikuwa Prof. Ali Mazrui na Prof. Mohamed Bakari,
Prof. Mohamed Bakari katika kufanya majumuisho ya yale aliyosikia pale
alisema kuwa ni muhimu Waafrika wakaandika historia yao wenyewe kwani
wakiacha historia yao iandikwe na watu wengine wataandika mambo ambayo
wao hawatayapenda.

Prof. Mazrui halikadhalika Prof. Mohamed Bakari wameandika mengi ambayo
yamesaidia sana katika kufahamika mengi katika Afrika.

Lakini hawa walikuwa wasomi waliobobea katika fani zao.

Sasa ukitazama hayo yaliyoandikwa katika uzi ulionielekeza niusome kwa kweli
kuna makosa mengi si tu ya ukweli wa hayo yaliyoandikwa bali hata makosa ya
lugha na kukosekana kwa rejea za kuthibitisha kuwa mwandishi alifanya utafiti.

-mX5LM3GdMqnuDM8en9K3QWJM_z_YoHazcT2AVnkA7Wiu3ExmyEICdpGMEqGmVrRagnPjdxdFDugu_MEVnHCH10Ma97Zj7hooF6PeQGN8SVEqe_gKReKOPVYB1fJCFdFokqFJk-fv8KMebBIki6KQf4_FW464k6aZPSpDaSxuK7LTDrJC7z-y6YJMPbbH_yaqS7vyMhUD4Ad1GpkuI86ESvCzKGyUZ_5PP5WG3NZtLk3IT-m6K8RXRTqQNOwha9Cq5F0hNvxsqgKj9OlWWo9zThZeyDXbCRl-neFmSLL53IxRuPf5523WBQfUmtW-muFZ4t2uclPmZUhn1PvOl29sJizRaynaNO1VfHwCmPSkuMKSVsmnQYsiPzonl3dI1l9TZqebpAo1WTEXmJH73hxKDDYuE88OTWNaAhrq9fsZp6bcrq6lFUe5jS92DTqIGj9zyQJsoPsV96Y3iOmMO0m60bo-N3SDbSQAHx_IDzZPJLNx56E7jtYc6WNBGguTuWU3bykNPKBcF6a_IrfQvGRPRhxZHPnZgt0LDobJKopj3lRgzcCb63xT1EXbZ6UyVa6S8Vsvmen9BuRueyk5vzRa3c-s0xUo7NR=w640-h480-no

Prof. Mohamed Bakari akiwa ofisini kwake Fatih University Istanbul, Turkey na Mwandishi

DSCN0096.JPG

Kulia kwa Prof. Mazrui ni Tamim Faraj Muslim University
of Morogoro (MUM) na kushoto kwake ni Mwandishi
Hilton Hotel, Kampala 2003

Wanamajlis,
Ingieni hapo chini msome dunia inasema nini kuhusu Prof. Ali Mazrui ili muweze
kupima kama kweli kila mtu anaweza kushika kalamu akaandika kuhusu historia
ya Afrika:
Mohamed Said: PROF. ALI MAZRUI MWALIMU WANGU WA MASAFA MAREFU

Ahsante Maalim wangu hakika umenipa maarifa mapya katika darsa lako kwenye huu uzi, ila kwa mimi mwanafunzi kuna swali naomba uniweke sawa kwa jibu lako kuwa kuna makosa ya ukweli na makosa ya lugha iliyoandikwa,Maalim tafadhali hapo naomba ufafanuzi wako kidogo. Mi nilichokibaini na nikacheka kuwa mapinduzi yalifanyika kwa mtoto kumpiga Baba yake ngumi ya pua!!!?
 
Ahsante Maalim wangu hakika umenipa maarifa mapya katika darsa lako kwenye huu uzi, ila kwa mimi mwanafunzi kuna swali naomba uniweke sawa kwa jibu lako kuwa kuna makosa ya ukweli na makosa ya lugha iliyoandikwa,Maalim tafadhali hapo naomba ufafanuzi wako kidogo. Mi nilichokibaini na nikacheka kuwa mapinduzi yalifanyika kwa mtoto kumpiga Baba yake kofi!!!?
Mtebetini,
Angalia kila penye wino ulokoza:

Binafsi nimejipa utaratibu kuwa vitabu vinavyohusu uafrika na waafri sitavitilia mkazo sana vile vilivyoandikwa na wazungu bali vilivyoandikwa na Waafrika wenyewe! Mfano ukisoma historia ya Mkwawa iliyoandikwa na wazungu wanasema mkwawa alijiua kwakujipiga risasi,?

Ukweli wa historia ya kiafrika wazungu waliona aibu kusema walimshindwa Mkwawa, Mkwawa hakujiua bali aliwatoroka wazungu na kuelekea Songea ambapo alifia milima ya Lukumbulu kwakuliwa na Simba baada ya kuugua akiwa milimani peke yake. Nimpongeze kamanda Edwin Mwesiga huyu ni mtafiti wa mambo ya kiafrika na uafrika wetu.

Ni rahisi sana Vijana wa leo kuwadhalau wazee wanaokutana nao barabarani na kuwaona watu wasio na Elimu wakiaminishwa kuwa elimu ilianzia magharibi, Cha ajabu Ahmed Baba (1556-1627) karne ya 16 aliandika vitabu 60.Ni mingoni mwa wasomi wa Phd katika ufalme wa Mali.

Ni vizuri watu tuyasake maarifa kwakutumia maarifa, na kwakutokujua historia yetu Waafrika tumelidhika Bara letu la Afrika na yale machache tunayoyafahmu, tukidhani wazungu ndio wasomi wa mwanzo duniani kumbe wapo waliofanya mapinduzi makubwa katika Africa,ila wamefichwa na historia za kigeni zinazofundishwa mashuleni.

Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......Pamoja na kwamba 1927 Gavana Sir David Cameron kupiga marufuku mtu mweusi kukanyaga mjini (posta ya leo) hasa kwenye sherehe za wazungu ambazo zilikuwa maranyingi zinafanyikia ukumbi wao pale makao makuu ya NBC leo,

Gavana huyu aliwaundia chama cha kuratibu sherehe za weusi huko pembeni ya mji huko mtaa wa Stanley (leo Lumumba) na kuwapa ofisi mahali leo wanapojiita TANU ilizaliwa. Lakini historia ya Tanganyika haiwataji waasisi wa AA, Rais wa kwanza Mwalimu Cesil Matola (msomi wa mwanzo kabisa enzi za mjerumani kutoka kabila la Wayao), katibu mkuu wa kwanza Klest Sykes (Mzulu mateka wa vita vya kwanza vya dunia toka Afrika Kusini), Mwekahazina Ali Ramadhan (mzaramo na mvuvi maarufu wa pwani la Azania).?

Hao ndio mwaka 1927? waliounda Chama cha kwanza kabisa cha kutetea maslahi ya weusi Tanganyika na shughuli zake zilikuwa ni kuratibu sherehe za waafrika tu.? (Chama cha walevi kwa lugha nyingine).? Mwaka 1933 Mwalimu Cesil Matola alifariki na nafasi yake ikakaimiwa na katibu mkuu wa chama hicho bwana Klest, mpaka ilipofika mwaka 1948? yakatokea mapinduzi yaliyoongozwa na mtoto wa Klest aliyeitwa Abdulwakil Sykes huyu alikuwa ametoka kupigana vita vya pili vya dunia, na aliporudi alikuwa na mawazo ya ujana toka vitani, akampindua baba yake kwa kumpiga ngumi puani. Kisha AA ikabadilishwa jina na kuitwa TAA,? Rais wake wa Kwanza akawa Dr Vedasto Kyaruzi? (Mhaya)huyu ndie dakitari wa binadamu wa kwanza kabisa wa kiafrika Tanganyika, Katibu mkuu akawa Abdulwakil Sykes na Mweka hazina akawa Dosa Azizi?, utawala huo ulienda mpaka mwaka 1953 uchaguzi ulipofanyika na Nyerere akashinda pale kwenye ukumbi wa Anautoglo Mnazimoja leo, mwaka 1954 Nyerere akabadili jina? la chama na kuwa TANU iliyokwenda mpaka mwaka 1977 na kisha kikazaliwa chama kiitwacho CCM ambacho kinalitafuna taifa leo..

Hili ndio chimbuko la AA, TAA, TANU na hii CCM.

Wanamajlis,
Makosa ndiyo hayo hayasemeki kwa wingi wake kwa kuwa muandishi
bado hajafikia kiwango cha kuweza kuandika kitaalamu.

Tuache hayo ya lugha twende kwenye ''facts'' ukweli wa kilichoandikwa
ambapo nimeweka alama ya kuuliza.

Kleist hakutoka Afrika ya Kusini.
Kleist kazaliwa Pangani mwaka wa 1894.

African Association ilibadilishwa jina kuwa Tanganyika African Association
(TAA) 1948 siyo 1950 hivyo suala la Dr. Kyaruzi kuwa rais wa kwanza wa
TAA halipo.

Nyerere hakubadili jina la TAA kuwa TANU jina hilo lilikuwapo toka 1945.

Yako makosa mengi kama ya Mkwawa ''kuliwa na simba,'' ''ngumi ya pua,''
nk. haya hapo juu yanatosha kuonyesha tatizo alilokuwanalo mwandishi.

Daktari wa kwanza Mwafrika ni Dr. Joseph Mutahangarwa si Dr. Vedasto
Kyaruzi.
 
Huwa nnawasiwasi mkubwa na huyo kijana ajiitae Yericko Nyerere, wasiwasi wangu ni kuwa ana maradhi ya nafsi, ambayo ni mabaya kuliko maradhi ya akili.
 
Maalim MS nimesoma na nimepitia kila nukta ya makosa uliyo ainisha kwa kweli nachelea kusema kuwa Mwandishi ajipange kufanya shughuli ya uandishi,katika fani ya uandishi bado ni "kinda la Shorwe Wanda au Shorwe Bwenzi".
Nimesoma sehemu ya bandiko lake Yeriko Nyerere na ameandika hivi :-

"Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......"

Wanabodi
Maandishi haya ange yaandika Maalim Mohamed Said laaaaahhh pangekuwa hapatoshi!!
 
Maalim MS nimesoma na nimepitia kila nukta ya makosa uliyo ainisha kwa kweli anachelea kusema kuwa Mwandishi ajipange kufanya shughuli ya uandishi,kati fani ya uandishi bado ni "kinda la Shorwe Wanda au Shorwe Bwenzi".
Nimesoma sehemu ya bandiko lake Yeriko Nyerere na ameandika hivi
"Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......"
Wanabodi
Maandishi haya ange yaandika Maalim Mohamed Said laaaaahhh pangekuwa hapatoshi!!
Mtebetini,
Watafiti walioandika kuhusu mwanzo wa siasa Tanganyika kama Iliffe
wametegemea sana nyaraza za akina Sykes.

Katika nyaraza zile ambazo chanzo chake ni mswada wa Kleist alioandika
kabla hajafa mwaka wa 1949 amewataja wazalendo wote walioasisi AA.

Nimeeleza kuasisiwa kwa AA katika kitabu cha Abdul Sykes:

''In 1929 Kleist and some close friends, namely, Mzee bin Sudi, a Manyema
Ibrahim Hamis, a Nubi, Zibe Kidasi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu,
Raikes Kusi, Rawson Watts
and Cecil Matola founded the African Association.

Kleist was the founding secretary. At that time the Governor of Tanganyika
was Sir Donald Cameron who was the administrator of the territory from
1925-1929.

Cameron was a liberal governor. Kleist was known to Cameron. Cameron
established the first Legislative Council and Indirect Rule in Tanganyika.

This liberal attitude of his greatly helped in the formation of the African
Association. But despite of this, the Association was warned not to indulge
in politics.

When the African Association was formed, already there were in existence
European and Asian Associations. In the Legislative Council Africans were
presented by a Catholic priest, Father Gibbons, who did not even live among
Africans but at Minaki Mission outside Dar es Salaam.

Z3c8GTE6bOAvoueqmrCRM8xZU31Onnnti0_1ny2g89ec9k8TyqM6nIAgA1DPp_1yJ56xJGvv5KIiJILedU_bqGBm9WPKQbQ13eWVISS5CFRPqnVDUGUQL4V7igUPseoZ7ejERJPOjKUninxF63OfzrbY9S7q1O1xV1C89QZ09YakQ8WtKEzUgESs9PLUMAkhVIw5HPqK_6pSx9V9i0gp3qH5d1Ut2wkL7gRQzL0DqWKwfBq-tWvZapDacJXx-MzFVqKdPW8VxKbs-mkQdOlgTHJo1plSOloKb0WNrx4AfnqKTEFKC8CoSmDEKkg4iqBS1KxZYUNyXlpG32m8-m6cQwFJZYNRYuGkRYMFQ-vRdw2V-yltv2VguMYTvVimrKhqpcXINIkfg-82t8ETM5rREY4-5sIhk9hysjdjVIn9UwEMQETvJ8XiOIHhsYPHKXoCPxHtSrAksN6Hz50tNMi_0fZ6iikIO4N0LqrYOX4E8lZwbUmgZaTLreWcTPkKaHfC2FgoxHY8eMDpr1DRt-rsqO9NwFostQDfcSdvof6AqFwRLS9iF3EuNHX2GDtIuWEA32vUxqLUjctCi2S-HiQrH-1t8X7baz2g=w800-h600-no

Kulia wa kwanza ni Father Gibbbons akifatiwa na Chief Thomas Marealle

Abdulwahid remembered his father telling him the reasons for forming the
Association:

''At that time there were two Associations existing. There was the European
Association and the Indian Association. Both these were concerned with their
own nationalities.

But the Africans had no such Association to defend them. In the Legislative
Council the Africans were represented by a white missionary named Father
Gibbons
, who worked at Minaki Mission several miles outside Dar es Salaam.

But in reality this European did not establish any connections with the Africans
whom he represented. For that reason the Africans, feeling unrepresented
and having no Association similar to that of the Europeans and Asians for
securing their rights, met and decided to form their own Association.[1]

The initiative to form an association of Africans free from organised religious
and tribal affiliations was a move against the established norms.

Although the Association had the support of Governor Donald Cameron
and was registered as a welfare association, missionaries cautioned Christians
not to involve themselves with the organisation as it would eventually lead to
politics against the state: ‘Christians were often warned by the missionaries
not to get themselves involved in any movements that were challenging
the government’.''

[1] Buruku, op. cit. p.101 (Daisy Abdulwahid Sykes)

Wanamajlis,
Ukimsoma Yericko Nyerere anakuja na majina katika AA sisi wazawa wa Dar
es Salaam hatujapata kuyasikia ya ''Mvuvi wa Azania,'' na ''Mpiga Filimbi
wa Hamelin
,'' si hao wazee wala watoto wao hata kuona nyumba walizoishi.

Mimi binafsi nawajua wajukuu wa Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Said
Mpima
, akina Zibe Kidasi ni ukoo maarufu akina Watts hawa ni kutoka
Tanga na mwanae Dr. Watts alikuwa mganga maarufu Tanga nk.

AA iliasisiwa 1929 na si 1927 na waasisi walikuwa watu maarufu Dar es Salaam
kutoka koo za Kimanyema, Kinubi na Kizaramo na Kizulu.
 
Maalim MS nimesoma na nimepitia kila nukta ya makosa uliyo ainisha kwa kweli nachelea kusema kuwa Mwandishi ajipange kufanya shughuli ya uandishi,katika fani ya uandishi bado ni "kinda la Shorwe Wanda au Shorwe Bwenzi".
Nimesoma sehemu ya bandiko lake Yeriko Nyerere na ameandika hivi :-

"Ukisoma leo historia ya Tanganyika ni aibu, inaanza na Nyerere na kuishia na Nyerere jambo ambalo ni uogo mkubwa......"

Wanabodi
Maandishi haya ange yaandika Maalim Mohamed Said laaaaahhh pangekuwa hapatoshi!!
Watoto wengi tu hassa hawa walio zaliwa miaka ya 80 hawajui au hawataki kujua kupambanua mambo.
Wao hungalia nani kafanya nani kasema hawangalii kilichofanywa au kilicho semwa.
Wana watu wao hata waseme utumbo au wafanye uwovu wao kwao ni mema na mazuri.
Na kuna watu hata weseme nini au wafanye nini madhali si wao basi hawathamini wala hawaamini wakiona tu jina baasi wao wameshotoa hukumu bila kusoma au kuona kilicho fanywa.
Dr Jakaya alisema akili za kuambiwa changanya na zako.
Lakini nadhani hakujua kama wengine hawana hizo za kuchangaya.
Mtu kama Yarico hana alijualo na akiambiwa anakejeli wakuu wake sasa huyu hata ukimuombea dua hatobadilika.
Labda litafutwe chosho la ngombe aingizwe labda atapata akili za kuchanganya.
 
Back
Top Bottom