Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Hamza Mwapachu, Abdulwahid Sykes na Chief Michael Lukumbuzya

Mohamed kwa nini wewe unamchukia Sana Nyerere?
Afrodenzi,
Kusahihisha historia ya wazee wengu ndiyo imekuwa kumchukia Nyerere?

Hivi ningeacha kukuelezeni yale yote ambayo amkuwa mnayajua ndiyo kweli
ningekuwa nampenda Nyerere?
 
Mohamed kwa nini wewe unamchukia Sana Nyerere?

Ikiwa Alama Mohamed Said anamchukia Nyerere kwa kuandika historia ya waasisi wa harakati za kudai kujitawala na waasisi wa TANU walioachwa kuandikwa na historia ya Kigamboni amma kwa makusudi kabisa amma kwa kushinikizwa amma kwa bahati nzuri, jee huyu nae anaesemekana amemtusi Nyerere tena "live" bungeni unamuongeleaje? :

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!

Cc wembeee, Ngongo, Nanren, Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Pasco, Uncle Jei Jei and company.
 
Afrodenzi,
Kusahihisha historia ya wazee wengu ndiyo imekuwa kumchukia Nyerere?

Hivi ningeacha kukuelezeni yale yote ambayo amkuwa mnayajua ndiyo kweli
ningekuwa nampenda Nyerere?
Kila kitu kina pande mbili.
Ni sawa kwa wewe kuandika na kutuambia story za wazee wako.
Zinaweza kuwa za kweli ama la. Lakini kwenye maandiko yako Nyerere huwa
ni kama mtu fulani tu hivi ambae aliwadhulumu watu . Yaani nasubiri siku utatoa story upande wa nyerere.
 
Ikiwa Alama Mohamed Said anamchukia Nyerere kwa kuandika historia ya waasisi wa harakati za kudai kujitawala na waasisi wa TANU walioachwa kuandikwa na historia ya Kigamboni amma kwa makusudi kabisa amma kwa kushinikizwa amma kwa bahati nzuri, jee huyu nae anaesemekana amemtusi Nyerere tena "live" bungeni unamuongeleaje? :

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!

Cc wembeee, Ngongo, Nanren, Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Pasco, Uncle Jei Jei and company.
Huyo nae hana heshima.
 
Huyo nae hana heshima.

Ukijisoma vizuri hapo juu kidogo suala lilikuwa kumchukia Nyerere, nnaona hilo umelisahau na umerukia "heshima".

Nnaomba jibu swali langu, kama umelisahau kanisome tena. Hilo la heshima ni mtazamo wako, mimi nadhani angekuwa hana heshima asingeitwa Mheshimiwa Tundu Lissu.
 
Na yeye Mheshimiwa tundu Lissu inaonyesha anamchukia Nyerere.
Jibu lako hilo.
 
Ni historia tu au kuna kaudini ndani yake yakhe? Mi nasema kuusu nyerere Allah alimpanga yeye ndo atutoe kule... Na hakutaka hao wengine kwasababu angewataka angewafanya...
 
Ni historia tu au kuna kaudini ndani yake yakhe? Mi nasema kuusu nyerere Allah alimpanga yeye ndo atutoe kule... Na hakutaka hao wengine kwasababu angewataka angewafanya...
Mkuu usitegemee upate historia
Nzuri kwa maalim muddy zaidi ya majina ya wacheza bao na wauza Samaki tu ndivyo utapata kwake
 
Si alikuwa na mpango wa kuandika kitabu kumjibu Mudeer, hicho kitabu ndiyo utakuta habari za Mwanamama Cecil Matola.
Hapa kuna jambo linaleta shida kidogo. Mbona marejeo yote ya vitabu yanamtaja Mwalimu Cecil Matola ni mwanaume? Au waandishi wa vitabu vya historia walikosea?
 
OTE="FaizaFoxy, post: 16655041, member: 43551"]Ikiwa Alama Mohamed Said anamchukia Nyerere kwa kuandika historia ya waasisi wa harakati za kudai kujitawala na waasisi wa TANU walioachwa kuandikwa na historia ya Kigamboni amma kwa makusudi kabisa amma kwa kushinikizwa amma kwa bahati nzuri, jee huyu nae anaesemekana amemtusi Nyerere tena "live" bungeni unamuongeleaje? :

Tundu Lissu: Mwl. Nyerere alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu!

Cc wembeee, Ngongo, Nanren, Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji, Pasco, Uncle Jei Jei and company.[/QUOTE]
Maalim Faiza,
Allah kakujaalia
Yan ulitegemea Nyerere hakujibu kitabu chako kipindi yuko hai

God forbid
Wembeee,
Ndugu yangu mimi najua mengi sana kuliko unavyodhania.

Kitabu changu kilivuruga watu wengi sana kiasi hata siwezi
kueleza.

Kutokana na hilo nikafahamiana na watu wengi mno katika
duru za kisomi na vyuo vingi duniani.

Unajua Nyerere alikuwa ''giant,'' katika siasa za dunia na pia
ulimwengu wa tatu.

Chochote utakachoandika kuhusu yeye kitasomwa kila chuo.

Mwalimu Nyerere alipanga kujibu na sisi mie peke yake ila
na kumjibu Ali Muhsin Barwani ambae alimfunga jela kwa
miaka 10.

Allah hakumjaalia Mwalimu kutujibu.

Huenda mimi ushanisoma sana unajua fikra zangu lakini nina
hakika hujamsoma Ali Muhsin Barwani.

Kitabu chake ambacho ni kumbukumbu (memoirs) kipo unaweza
kukipata Tanzania Publishig House (TPH) Samora Avenue au
Ibn Hazm Media Centre Bookshop Msikiti wa Mtoro na Manyema,
Soma Bookshop Mikocheni, Elite Bookshop Mbezi Samaki.
Bei shs: 10,000.00 Ibn Hazm kwengine ni shs: 13,000.00.

Ukiwa na subra na ustaarabu na heshima katika huu mjadala
mimi nitakufunza mengi na utajua mengi hivyo kuongeza elimu
yako.

Kama asemavyo Maalim Faiza: Elimu bila khiyana.
 
Mkuu usitegemee upate historia
Nzuri kwa maalim muddy zaidi ya majina ya wacheza bao na wauza Samaki tu ndivyo utapata kwake
Wembeee,
Kwani ndugu yangu mtu ikiwa kazi yake ni kuuza samaki ndiyo
hairuhusiwi kuandika makubwa aliyochangia katika jamii?

Au mtu akiwa anacheza bao ndiyo yeye keshapoteza heshima
yake na hastahili kutajwa?

Mwalimu Nyerere alipokuwa mtoto mdogo siku moja chifu wa
jirani alimtembelea Chief Burito akamkuta Nyerere yuko nje
anacheza bao.

Yule chifu akamwambia Nyerere hebu cheza na mimi.
Hii ilikuwa katika njia ya mtu mzima kufanya maskhara na mtoto.

Yule chifu alipata mshtuko.
Mwalimu Nyerere alimfunga.

Alipokuwa faragha na Chief Burito Nyerere akamwambia huyu
mtoto hebu mpeleke shule akasome kwani ana akili sana kanifunga
bao hapo nje.

Hizi habari ziko katika kitabu cha Morlon (2015).
Kinapatikana Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.

Kama wapendavyo kusema Waingereza, ''The rest is history.''
Nyerere alikuwa mcheza bao maisha yake yote.

Nyerere_bao_butiama.jpg

Babu yangu aikuwa mcheza bao maisha yake yote na wazee wangu
wengine wengi tu walikuwa wacheza bao.

Mwanzoni nilidhani wewe ni muungwana na kijana ulieleka sawa kumbe
nilikosea.

Prof. Juma Kapuya alikwenda Butiama akamkuta Mwalimu Nyerere
kwenye bao.

Mwalimu akanyanyua kichwa chake akamwambia Kapuya, ''Kaa hapo
nikufunge kama mtoto mdogo.''

Kapuya hakuthubutu.

Dar es Salaam Mtaa wa Mafia na Kongo karibu na nyumba ya Mzee Maneno
Kilongora
kulikuwa na barza kubwa ya bao.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa kila akija Dar es Salaam kutoka Tabora
alikuwa akenda pale kushindana na mabingwa wenzake.

Bao ni moja ya mila zetu.
Kama ilivyo kwenu kwenda kilabuni kunywa pombe za kienyeji.

Msome babu yangu ''Mcheza Bao,'' hapo chini uone nini alifanya katika
historia ya Tanganyika:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH
 
kila ninachosoma kutoka kwake .
Afrodenzi,
Ukisema kila kitu hatutoweza kuwa na mjadala wowote.

Lete hata sentensi tatu katika hicho unachosoma kutoka
kwangu.

Itatosheleza.
Ikiwa hutoweza basi kaa ukijua unanisingizia uongo.
 
Back
Top Bottom