Dah hii story is so amazing yan.. Ila mbona zimefichwa jaman.?
Bakar..,
A fascinating and amazing story in deed!
Kisa cha kukataliwa historia ya
Abdul Sykes ni kuwa ikiwa utamleta
Abdul
katika historia ya TANU itabidi urudi nyuma miaka miaka 50 kupata asili yao
ya Kizulu vipi walikuja Tanganyika.
Utakwenda hadi Kwa Likunyi Mozambique ambako
Sykes Mbuwane babu
yake
Abdul alikotokea.
Hiki kijiji kipo Imhambane na ndipo
Von Wissman alipokwenda kuchukua
jeshi la mamluki wa Kizulu kuja Tanganyika kupigana na
Abushiri bin
Salim na
Chief Mkwawa miaka ya mwisho ya 1800.
Ally Sykes mwaka wa 1952 alichukua likizo na akaenda hadi kwao kwa
Likunyi kuona alikotoka babu yake.
Nimeandika kitabu cha maisha ya
Ally Sykes, ''Under the Shadow of British
Colonialism.''
Huu mswada haujachapwa sasa karibu mwaka wa ishirini.
Humo ndimo aliponieleza safari tatu muhimu kwake wakati wa kudai uhuru.
Safari ya kwanza hii ya Mozambique 1952, safari ya pili Ghana kuadhimisha
uhuru wa Ghana 1947 tena hakupanda ndege kenda kwa nchi kavu na safari
nyingine ya Rhodesia 1953 alipokamatwa na Makaburu.
Safari hii TAA ilialikwa Northern Rhodesia na
Kenneth Kaunda raia wa African
National Congress na alifatana na
Denis Phombeah.
Ukielezwa aliyoshuhudia Ally Sykes katika hizi safari utajua nini maana ya ukoloni.
Ikiwa utaeleza haya na mengine mengi ambayo hapa hakuna nafasi ya kuyaeleza
utakuja na sura nyingine kabisa katika historia ya TAA, TANU na harakati za uhuru.
Itabidi ueleze vipi hawa akina
Sykes walijuana na
Kenneth Kaunda, Jomo
Kenyatta,viongozi wa Fabian Society kama
John Hatch kabla hata
Nyerere hajawajua.
Itakubidi pia ueleze vipi baba yao aliasisi African Association (AA) 1929 na
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933.
Vipi aliweza kujenga nyumba hiyo ilipozaliwa TANU na kujenga shule jengo
ambao lipo hadi leo.
Itabidi pia ueleze viongozi wa wakati ule na michango yao katika jamii hasa
machifu kama
Chief Kidaha Makwaia, Chief Abdallah Said Fundikira na
Thomas Marealle ambao wakijuana vyema na akina
Sykes na kustahiana
sana.
Hizi ndizo zilikuwa siasa za nyakati ule.
Haya hayakutakiwa.
Waandishi na watafiti wa Kivukoni College waliona hii itapunguza umuhimu wa
Nyerere katika historia ya TANU.
Tatizo likawa historia ya TANU lazima ianze na
Mwalimu Nyerere.
Hili ndilo likasababisha matatizo mengi katika uandishi wa historia ya TANU.
Hivi ndivyo tulivyofikishwa hapa leo tuko barzani tunajadili na wengine kama
akina
Nguruvi3 wanajadili kwa hamaki wakidai ati
Mwalimu Nyerere
anakashfiwa.
Na ''kashfa,'' yenyewe ni kule kuandika historia ya TANU kama ilivyokuwa.