Handbrake

mkuu kubali tuwa gari yako upande wa mfumo wa handbrake haipo kamili 90% maana usingeweza kuisogeza hata hatua 2 mbele kama ingekuwa nzima. na vile vile uharibifu hapo lazima umetokea hata kam ni kwakiwango kidogo sana.moja kubwa ni kuisha kwa brake pad.then kuchimbika
 
unapoanza kuondoka tu kama gari ni nzima kwenye huo mfumo wa h/break lazma tairi zisote hasa kama upo kwenye barabara ya changarawe.
Nilishajaribugi hilo kwenye toyota isis.
 
Sidhani kama mfumo wako wa gari uko salama. Pamoja na baadhi ya wachangiaji kukupa moyo ila kuihalisia hand brake ikiwa sawa gari haliwezi kutembea kwa umbali mrefu. Ingekuwa ni hivyo pasingekuwa na umuhimu wake. Chukulia gari linamzigo na ni kwenye mlima halafu ukasimama kwa kupitia hand brake, kwa maelezo yako ni kwamba halitasimama sababu tairi hazijabanwa. Wewe kama uliweza kutembelea maana yake za kwako hazijabanwa inavyotakiwa. Je ! Wajua hand brake waweza kuitumia kama brake kwenye hatari? Sasa ikiwa ndiyo nini kitatokea iwapo brake haifanyi kazi
 
Gari yoyo iliosawa upande wa hand break
Haiwezi ku move kama aujatoa hand break
Hua hand brake zinaachia kila mda kama ilivo break ya kawaida
And pia kuna uwezekano aujaivuta mpaka mwisho
 
Gari yoyo iliosawa upande wa hand break
Haiwezi ku move kama aujatoa hand break
Hua hand brake zinaachia kila mda kama ilivo break ya kawaida
And pia kuna uwezekano aujaivuta mpaka mwisho
ni staff handbrake btw
 
Madhara yake...
1. Unatumia mafuta mengi.
2. Unaharibu mfumo wa hand brake, kumbuka mfumo wake upo kwny tairi za nyuma.
3. Endapo handbrake inanguvu afu ukaiburuza hvyo hvyo unaweza kupelekea kuwaka moto kwa tairi za nyuma na hvyo kusababisha gari kuungua.

Kumbuka.
1. Kama system ya hand brake ni nzima na gari ikawa kwny hand brake gari haiwezi itaondoka, ukilazimisha sanaa bac tairi za nyuma zitaburuzwa na sio kuzunguka.
2. Kama system ya hand brake inafanya kazi vizuri na upo kwenye mwendo ukiingiza hand brake bac tairi za nyuma zitazuiwa kuzunguka hvyo kufanya gari ujigeuze kurudi sehemu ilipotoka au eielekee upande mwingine tofauti na ulipokuwa ukielekea.

Mwisho.
Gari yako mpk hapo haina hand brake unayoweza kuitegemea, fanya upeleke kwa fundi mwny uzoefu akairekebishe.
Kigezo chakusema gari ni mpya sio sahihi kwakuwa naamini hiyo gari ni hizi tunazotumia ambazo wenzetu wameshazitumia tayari (second hand cars).
Mawasilisha mkuu.
 
Automatic unaendesha bila shida yoyote ila gari inakua kama nzito hivi
Ukiona gari ipo kwny hand brake na ukiendesha inaondoka vzr icpokuwa ni nzito kdg ni dalili kwamba hand brake tayari inahitaji service, hand brake nzima hairuhusu gari kuzungusha tairi.

Ni wengi sanaa ambao huwa tunafanya service ya kumwaga oil ila ukimuuliza mtu hand brake amewah kuifanyia service atakwambia hajawahi kuigusa, km ameigusa bac ujue lilitokea tatizo ambalo lilimlazimu aifanyie service.
 
thanks bro , ntaifanyia maintenance next service
 
Siku nyingine usifanye hivyo...gari:

1. Matairi yanachakaa mapema
2. Mafuta yanatumika mengi kwa umbali mfupi
3. Hand brake itaharibika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…