Handeni, Tanga: Leo ndo hatma Polisi wanaotuhumiwa kudhalilisha Wanawake

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,126
Reaction score
5,068
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema litatoa taarifa ndani ya saa 24 kuhusu sakata la baadhi ya askari wilayani hapa kutuhumiwa kuwashika sehemu za miili wasichana na kuwalazimisha mapenzi.

Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda alisema ni kweli jambo hilo limefika mezani kwake na tayari ameunda timu kufuatilia sakata hilo wapate ukweli halisi ni upi.

Alisema tayari uchunguzi umeanza kujua ukweli kwa jinsi lilivyoripotiwa na ndani ya saa 24 atatoa majibu ya suala hilo.

“Ni kweli suala hili lipo mezani kwangu na nimeunda timu kufuatilia waliohusika ni akina nani, wamefanyia wapi, imekuwaje na baadaye nitatoa majibu kama sio leo (jana) basi ni Ijumaa (kesho) wakikamilisha uchunguzi wa suala hilo nitaongea na waandishi,” alisema Kamanda Chatanda.

Sakata hilo limekuja baada ya Hawa Mokiwa kueleza kwenye kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Siriel Mchembe kuwa baadhi ya askari wamekuwa na tabia ya kuwashika maungo bila ridhaa yao na kuwalazimisha kufanya mapenzi.

Alisema askari hao wanalazimisha uhusiano na kama msichana akimkataa anamtafutiwa sababu na kwenda kumlaza rumande.

“Mkuu wa wilaya, tunapenda kulalamika kweli kuna askari wakija humu ndani wanakushika bila ridhaa yako, ukikataa wanakukamata,” alisema Hawa.

Kauli ya Hawa iliungwa mkono na Zulfa Zidadi, akisema suala hilo lipo na kumtaja mdaiwa wa tukio hilo.

Baadaye mkuu huyo wa wilaya, alisema Serikali haiwezi kunyamazia vitendo hivyo kwa kuwa ni makosa kisheria kumshika mtu maungo yake ya mwili bila ruhusa yake.

“Suala la udhalilishaji wa kijinsia halikubaliki, ni marufuku kwa mwanamume kutumia cheo chake, nguvu zake au kwa namna yoyote ile kumshika mwanamke kifua chake au makalio bila idhini yake, hayo ni makosa na haikubaliki,” alisema Siriel Mchembe

Mkazi wa Handeni, Mohamed Abdallah alisema japo hajawahi kusikia tukio hilo, ila kitendo kinachodaiwa kufanywa na askari hao ni makosa
 
Hao polisi wakijichunguza wenyewe watasema hao wasichana Ni machangudoa.
Kumbuka majibu kuhusu uchunguzi wa Hamza kaitwa gaidi mfia dini.
Kwenye hiyo team ya uchunguzi inabidi wawepo na madiwani 2-3 wa eneo la chanika.

Kama wawakilishi upande wa wananchi.
 
Wakimaliza huko waende Malawi kuna polis wamepigwa na gari kuharibiwa vibaya
 
Hao polisi wakijichunguza wenyewe watasema hao wasichana Ni machangudoa.
Kumbuka majibu kuhusu uchunguzi wa Hamza kaitwa gaidi mfia dini.
Wewe dar hapa ushawahi sikia polisi wanarukia mademu za watu disco!!

Haya mambo ya habari za upande mmoja hayafai kuhitimisha jambo.
 
Polisi imekula kwao maana wanatumia vyeo vyao,,, lakini huo mkoa ni tabia yao tu kupenda sex all the time,,,, hata muda wa kaz... Hasa wanaanza na watoto wadogo... Serikali inatakiwa ifatilie sana haya mambo na sio kuchukua kiki kwa hao askari tu, hii mikoa ya pwani ni ya kipu#"*vu sana.. Unakauta kazee kana wake watatu na wawili ni vitoto vya sec
Shwaaaain kabisa
 
Mrejesho wa Kamati ya uchunguzi Mbona wananchi hatupewagi jamani?!
 
Vipi hali ya sasa ya kiutendaji ikoje?

Je imeimarika?

Je wananchi wahaonewi tena?

Je hakuna hila zozote zinazoendelea chini kwa chini za kuchomekea wananchi makosa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…