Handeni wanakosa soko la mihogo yao

Handeni wanakosa soko la mihogo yao

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Baada ya kuhamasika na kulima zaidi mihogo badala ya mahindi waliyoyazoea kama zao la biashara na chakula. Baada ya mafanikio ya wakulima wa kijiji cha Kwamsisi kupitia mihogo na wengine kuiga sasa ni kilio.
 
kuna project kama likua ihusicse soko la china ....sijui inaendelea au ilikua hamasa tuu
 
Mihogo mikavu inauzika sana rwanda, burund na uganda
 
Aaaah kila mwananchi anasonya tu hivi sasa, wanauzia watoto wadogo wanaokaanga mihogo kwenye visufuria
 
Habari njema hiyo, lakini mwananchi mkulima mdogo wa kaiwaida hawezi kuilewa habari kama hiyo
....kwa kuanzia wangetengeneza unga ilikuilinda mihogo yao halafu wanasafirisha unga na kuja kuuza mjini....kuliko Kusubiri mpk mabosi waje....wao wenyewe wajisogeze
 
Wale Wazigua ngoja wavune "Ujinga wao" wa kuchaguwa Wabunge wasiokuwa na manufaa kwao..,
Mbunge wao ndo amewahamasisha wapande Mihogo maana ametafuta Soko la Zao hilo la Mihogo, matokeo yake hv sasa amewatelekeza!!!
 
Hapana DC Gondwe ndiye aliyewahamasisha kulima Mihogo kwa wingi.
 
Mihogo mikavu inauzika sana rwanda, burund na uganda
We kijana wewe kama wiki mbili hivi zilizopita kigoma walikua wanalalamika sana kuhusu hii mihogo mikavu kilo kuuzwa 200tsh kama soko lingekuepo huko sidhani ingefikia hali hyo mana nadhani mahusiano ya biashara kat ya kigoma na hizo nchi ni yakaribu sana...

Handeni nadhani mkuu wa wilaya aingilie kati na awatafutie soko mana alilazimisha kila kaya kulima mihogo vinginevyo hatua zingechukuliwa na nadhani ilikua kujibu jitihada za mkuu kuwa hatosaidia kwenye njaa. Na kiukweli ni mingi mnooo HANDENI MIHOGO ya 500 n balaa na kila baada ya hatua 10 kuna mama anakaanga mihogo hasa maeneo ya pale mjini.
 
Una uhakika na unacho ongea? Nikupe namba za mteja wa hiyo mihogo mikavu wanaopeleka burundi na rwanda kama unayo
 
Nadhani ukiiweka humu utakua umesaidia sana mana ITV walionesha wamama wakilalamika kuhusu hyo mihogo kigoma so kwa kifupi nina uhakika mana hcho ndicho nilichokiona

Kwa faida ya wengi weka namba huenda ikawa fursa pia.
 
Hapana DC Gondwe ndiye aliyewahamasisha kulima Mihogo kwa wingi.
Mkuu Gondwe alikuwa anafanya vile kutokana na Mbunge kusema ametafuta Wachina ambao watajenga Kiwanda cha kuchakata Mihogo, hivyo Wananchi wahamasishwe kulima Mihogo kwa wingi kwakuwa ni fursa ya kibiashara ikizingatiwa Handeni hakuna Mazao ya Biashara zaidi ya Kilimo cha Mahindi tu..,
 
Una uhakika na unacho ongea? Nikupe namba za mteja wa hiyo mihogo mikavu wanaopeleka burundi na rwanda kama unayo
Kama hiyo ni kweli Nunua wewe Kwa wakulima ukauze huko utajirile
 
Mkuu Gondwe alikuwa anafanya vile kutokana na Mbunge kusema ametafuta Wachina ambao watajenga Kiwanda cha kuchakata Mihogo, hivyo Wananchi wahamasishwe kulima Mihogo kwa wingi kwakuwa ni fursa ya kibiashara ikizingatiwa Handeni hakuna Mazao ya Biashara zaidi ya Kilimo cha Mahindi tu..,
Hiki ndio kipindi kizuri kwa Mbunge kwenda kwa Wakulima.
 
Viongozi wetu wameshikwa na kiwewe na woga, Kiongozi asiposema kitu kwa wananchi kama wanavyofanya wenzake ni hatia na habari mbaya kwake. Hivyo,,,, Lazima aseme chochote kwa wananchi tena mbele ya kamera na nyuma ya vipaza sauti. Matokeo yake ni hasara kwa wananchi au kushuka kwa mapato kutokana na maamuzi ya woga kwa wananchi.

Mbegu za mihogo walizoshauriwa kulima sio zile za asili walizozoea zinazoweza kukaa ardhini kwa muda mrefu kusuribiri ukame/njaa itokee bila kuharibika, hizi za kisasa ni miezi 6-9 tu ardhini, baada ya muda huo kupita hazijauzwa ubora wake unapungua. Ambao hawakulima mihogo wanafurahia rundo la mihogo kwa sh. 500 Tu.
 
Hii ni Meseji niliyotumiwa na Mmoja wa Katibu Kata wa Kata mojawapo iliyopo huko Handeni.

PIA TUWATANGAZIE WANAJAMII NA WAKULIMA WA MHOGO WANAOHITAJI KUFUNGUA AKAUNTI YA BENKI YA NMB AMBAYO HAINA MAKATO YOYOYE,PIA ITAMSAIDIA KUHOFADHI FEDHA ZAKE, WATU WA BANK WAYAKUJA JUMANNE TAR 14.8 .2018 NAOMBA JUMATATU NIPATE TAKWIMU YA WAHITAJI MAANA WATAPITA VIJIJI VYOTE VYA KATA YETU, TAFADHALI TOA TAARIFA KWA WAKATI, VIGEZO NI SH 10,000 NA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA ,AMBAE HANA KITAMBULISHO AJE NA PICHA YA PASPOT SIZE MOJA.

Naona Matatizo yao yanaanza kushughulikiwa.
 
Mwanzo mihogo ilikuwa zaidi inalimwa Kwamsisi lakini sasa imelimwa sana huko. Kuna uhusiano gani wa kuwa na acc ya bank ya nmb na soko la mihogo? taarifa zaidi please!
 
Back
Top Bottom