Hangary: Hatutoafikiana na EU kuweka vikwazo dhidi ya mafuta na gesi ya Russia, 90% ya waHungary watapata dhiki kubwa na uchumi wetu utaanguka

Sikirimimimasikini

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2019
Posts
2,926
Reaction score
15,634
Waziri Mkuu wa Hungary, Viktor Orban, ametangaza kuwa nchi yake (Hungary) ipo dhidi ya vikwazo vyovyote vitavyowekwa na umoja wa Ulaya juu ya Russia kuuza mafuta na gas ktk nchi za Umoja huo.

Kufuatia mkutano uliofanyika London uliowahusisha mawaziri wakuu wa nchi kadhaa zikiwemo Hungary, Poland, the Czech Republic, Slovakia na Uingereza, Orban alisema kuwa pamoja na kuwa Hungary imesikitishwa na Russia kuanzisha vita nchini Ukraine, lakini serikali ya Hungary hapo tayari kuruhusu familia za waHungary kufanywa kafara (kuadhibiwa) la vita hiyo (“to be made to pay the price of war”).

Akinoti kuwa vikwazo vinavyoweka dhidi ya Russia vinaziumiza nchi zote za Ulaya, Waziri Mkuu huyo akasema kuongezea vikwazo ktk sekta ya nishati ya Russia (mafuta na gesi asilia) vitaiathiri Hungary vibaya zaidi. Waziri Muu huyo akadokeza kuwa karibia kiasi chote cha mafuta na gesi asilia kinachotumika Hungary hununuliwa toka Russia, na 90% ya familia za waHungary hupasha joto makazi yao kwa kutumia gesi hiyo ya Russia, akaongezea kuwa uchumi wa nchi ya Hungary hauwezi kusimama pasi na mafuta na gesi za Russia.

===========


Hungary will not support sanctions on Russia covering oil, gas imports: Premier

Hungary buys most of its oil and natural gas from Russia, says Viktor Orban​

Mehmet Yılmaz |09.03.2022




BUDAPEST

Hungarian Prime Minister Viktor Orban announced Tuesday that his country is against possible sanctions on Russia that would cover imports of its oil and natural gas.

Following a meeting in London with his counterparts from fellow Visegrad Group countries Poland, the Czech Republic and Slovakia along with British Prime Minister Boris Johnson, Orban said in a statement that Hungary condemns Russia’s launch of a war on Ukraine but would not allow Hungarian families “to be made to pay the price of war.”

He said it is in everyone's interest to end the war as soon as possible and his country will make every effort to do so.

Noting that the sanctions imposed on Russia affect all countries in Europe, he said the expansion of sanctions to Russia’s energy sector will affect Hungary "very seriously."

Orban said Hungary buys most of its oil and natural gas from Russia and 90% of Hungarian families heat their homes with gas, adding the Hungarian economy could not function without oil and gas.

Russia's war on Ukraine, which began on Feb. 24, has drawn international condemnation, led to financial sanctions on Moscow and spurred an exodus of global firms from Russia.

At least 474 civilians have been killed and 861 injured in Ukraine since the beginning of the war, according to the UN, which noted that conditions on the ground make it difficult to verify the true number.
Some 2 million people have also fled to neighboring countries, said the UN Refugee Agency.

 
Marekani ni muhuni sana, lengo lake ni kuidhoofisha Europian Union, alianza na kampeni ya BREXIT akafanikiwa, sasa hivi kawaingiza mkenge kwenye hili sakata la Ukraine nao wakanaingia kichwa kichwa, nashangazwa jinsi Germany na France yalivyokua mandezi badala ya kusimama imara kupambania umoja wao.
 
Kuna maamuzi EU wanafanya sasa hivi hadi mtu unakosa jibu kama wapo timamu au lah? Mfano, uamuzi wa Ujerumani kusitisha nordstream 2 wakati bado wanaingiza gesi kupitia nordstream 1 lakini pia kampuni za ulaya zimewekeza kwenye nordstream 2.

Ulaya kwa sasa wamekuwa watumwa wa Marekani, huu ni ukweli usiopingika.
 
Mimi lawama zangu zote ni kwa ujerumani na mfaransa, hawa ndio nilikua nawaona vichwa vya kusimamia imara muungano na uchumi wa EU, lakini badala yake yamekua ni majitu ya kuburuzwa tu na Marekani pamoja na Muingereza.
 
Mimi lawama zangu zote ni kwa ujerumani na mfaransa, hawa ndio nilikua nawaona vichwa vya kusimamia imara muungano na uchumi wa EU, lakini badala yake yamekua ni majitu ya kuburuzwa tu na Marekani pamoja na Muingereza.
Tangu baada ya vita vya 2 vya dunia wamekuwa watu wa ndio mzee sema kwa sasa udhaifu umezidi. Angela Markel aliikazia Marekani kwenye baadhi ya mambo ila huyu wa sasa hamna kitu kabisa. Macron anataka kushika kijiti cha Markel lakini hana uwezo wa kukaza yeye anaishia kuongea tu. Hata Uingereza ni kibaraka wa Marekani ila kwa sababu ya kiherehere chake cha kuwa wa kwanza kukubali kila wanaloambiwa ndo maana unamuweka kundi moja na Marekani.
 
Hasahasa Germany hivi vikwazo vitamuumiza sana.
Ila wamejitahidi vya kutosha ila wameshindwa.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Uingereza mimi hua namchukulia ni mke halali wa Marekani, yeye yuko bega kwa bega kumsapoti mume wake, ila hawa wengine ndio hua nashindwa kuwaelewa yaani nawafananisha na michepuko isiyokua na misimamo, bwana wao Marekani akiwakazia wanatoa mpaka ndogo.
 
Kwahiyo mkuu unawaona wao ni kama hawafahamu haya ila sisi huku ndo tunayafahamu na kuwaona wajinga?
 
Yaan us anavyofanya saiv ni maumivu makubwa sana kwa ulaya. Huu muungano wa nato inabidi us atoke wabaki wa ulaya tuu la sivyo us ataendelea kuwabuzura sana.
Hungary anazungumzia EU wewe unazungumzia NATO, yaani lengo hapo ni kumsema tu US. Hebu rudi kwenye hoja ya Hungary
 
Hatimaye akili zinaanza kuwakaa sawa

Lkn hiz taarifa huwezi kuzikuta kweny propagandaist media Kama BBC [emoji23][emoji23]
 
Ngoja bei ipae waone maana Aljeria amekataa kuongeza uzalishaji wa gesi kwenda ulaya, alternative ni kununua US ambapo yatakuwa ghali kutokana na umbali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…