kuna tetesi kuwa mwenyekiti wa usajili wa club ya simba(mikia) fc amepeleka barua TFF ili aweze kuidhinishwa kuwa msemaji wa club hiyo ili aweze kuwa huru zaidi kuongelea mambo yanayoihusu club yake hiyo na ikibidi naya club zingine hususan YANGA..sasa binafsi najiuliza hivi msemaji wa club ya mambumbumbu fc(mikia fc) ni nani? na iweje aingiliwe majukumu yake? ama hatimizi wajibu wake kama ilivyokusudiwa au ndo ubepari wa huyu jamaa mweupe mweupe mhaini? au ndani ya club ya mabonanza fc katiba ya club inamruhusu kufanya hivyo?? wakuu hebu tujadili hili ni sahihi kwa huyu jamaa kuwa msemaji wa club na wakati huohuo ni mwenyekiti wa usajili wa hiyo timu na je mgawanyo wa madaraka wa vipongozi katika timu upoje ndani ya club au ndo kusema kunawatu wachache wenye nguvu na sauti ya kuamua na kuongelea mambo ya timu pasipokuwa na mipaka yoyote?..Nawasilisha