Hans Poppe aunga mkono kutafutwa Kocha mpya Simba SC, asema timu haijawa na muunganiko mzuri

Kopunovic au Milovan ndio makocha wanaopaswa kuifundisha Simba hii. Huyu hana mbinu nyingi.
 
Timu hizi za SIMBA NA YANGA zitaishia hivyo hivyo kwa mambo yasiyona maana...hivi TIMU INAONGOZA LIGI..imecheza mechi 5....imeshinda 3.....ime draw 2....Bado timu mbovu?timu hizi hazitoendelea kamwe hadi hao WAZEE wanaojiita MAKOMANDOO wa timu waondoke....timu ilihangaika miaka 4 haijashiriki Mashindano ya kimataifa....lakini OMOG kafanikiwa hilo na badala ya mwaka huu kuelekeza nguvu za ubingwa mnaanza zengwe.....
 
Kikosi cha bilioni 1.3

Hoping for the best, expecting worse
 
Hizi timu bhana ni pasua kichwa tu tayar mtibwa katumia udhaifu huo
 
Hiv Nyie mnaoshabikia afukuzwe mnasema with facts au ushabik maandazi tu
Msimu uliopita kawapa ubingwa wa FA Plus kushika nafas ya Pili
Msimu huu mmesajili Team nzima kuanzia Golikipa mpka mshambuliaj wa mwisho unategemea ile chemistry ya hawa wachezaji wapya na wazaman itakuja ndan ya mechi tatu tu za ligi
 
kama haijawa na muunganiko mzuri kubadilisha kocha ndio suluhisho la kudumu?
Ni moja ya options katika kusuluhisha tatizo, au hujui??

Kama kocha anashindwa kupanga timu na kufanya sub zenye impact, anahitaji kukaa pembeni kidogo.
 
Hicho sio kigezo cha kutokubadilisha kocha. Unaweza kuwa CEO wa kampuni na ukaifanikisha sana mpaka ikanunuliwa na kampuni nyingine, then kwa level iliyopo kampuni ukaonekana huna tena uwezo wa kwenda juu ya hapo. Hiyo ni kawaida sana.
 
!
!
Mimi nadhani apatikane Kocha mzalendo tu wa hapa hapa. Huwa sionagi tofauti timu zetu zinapofundishwa na Kocha mgeni.
>Mpira ni butubutu vilevile
>Unaweza ukajua Uwanja, kila Mara mpira unatoka nje ama wa kurushwa au goal kick
>Wachezaji wakipiga pasi tano kwenye nusu ya Wapinzani wao bila mpira huo kuharibika ni swala ambalo haliwezekani.
>Mpira kama ngoma kila saa filimbi.
 
Hicho sio kigezo cha kutokubadilisha kocha. Unaweza kuwa CEO wa kampuni na ukaifanikisha sana mpaka ikanunuliwa na kampuni nyingine, then kwa level iliyopo kampuni ukaonekana huna tena uwezo wa kwenda juu ya hapo. Hiyo ni kawaida sana.
Hivi kwani nani anaongoza ligi?
 
Hivi kwani nani anaongoza ligi?
Target inatakiwa kuwa bingwa sio kuongoza ligi, mwaka jana tuliongoza ligi kwa mbali sana lakini hatukuwa mabingwa. Simba wanaunderperform given the investment ya wachezaji msimu huu na huo ni ukweli usiobishaniwa kwa wanaojua footwork.
 
badala ya kutafuta mganga mzuri wanapoteza muda kutafuta kocha.shida ya samba ni bado hawajapata mzee mzuri wa power benki he he
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…