Hans Poppe aunga mkono kutafutwa Kocha mpya Simba SC, asema timu haijawa na muunganiko mzuri

Hans Poppe aunga mkono kutafutwa Kocha mpya Simba SC, asema timu haijawa na muunganiko mzuri

Mpeni nafasi zaidi, ligi ndio inaanza.
Unajua Omog ana misimu mingapi,kila msimu fowadi butu. Msimu huu kaletewa wachezaji anaowataka tena ni wazuri,ameshindwa kuwaunganisha. Anawapiga madogo bench kwa husda na roho mbaya yake. Akwedreeeeee
 
Timu hizi za SIMBA NA YANGA zitaishia hivyo hivyo kwa mambo yasiyona maana...hivi TIMU INAONGOZA LIGI..imecheza mechi 5....imeshinda 3.....ime draw 2....Bado timu mbovu?timu hizi hazitoendelea kamwe hadi hao WAZEE wanaojiita MAKOMANDOO wa timu waondoke....timu ilihangaika miaka 4 haijashiriki Mashindano ya kimataifa....lakini OMOG kafanikiwa hilo na badala ya mwaka huu kuelekeza nguvu za ubingwa mnaanza zengwe.....
Ni kushindwa kuelewa,watu wanazungumka kutokana kutazama michezo ya timu. Zote Simba na Yanga zinaongoza kutokana na kukutana na timu mbovu zaidi yao. Lakini wataenda kufanya nini kimataifa. Zingatia Simba imetumia mabilioni kusajiri,japo mpira in mchezo lakini huwezi kuilinganisha na kinachofanyika uwanjani
 
Binafsi siungi mkono kumtafuta kocha mkuu mpya.
Ushauri wangu kwa sasa, timu iongezewe kocha msaidizi wa pili ambaye kwa kushirikiana na Mayanja " Mr Mia Mia" watakuwa na nafasi ya kumsaidia chief coach Omog.
Kwa nini mzawa? Naamini huyu mzawa atakuwa kiungo kizuri kati ya wachezaji na benchi la ufundi.
 
Ni kushindwa kuelewa,watu wanazungumka kutokana kutazama michezo ya timu. Zote Simba na Yanga zinaongoza kutokana na kukutana na timu mbovu zaidi yao. Lakini wataenda kufanya nini kimataifa. Zingatia Simba imetumia mabilioni kusajiri,japo mpira in mchezo lakini huwezi kuilinganisha na kinachofanyika uwanjani
Ni lini kipimo cha uwezo wa timu kinafanywa na RAMLI?yaani timu inaongoza. .useme haifanyi vzr...labda ulitaka ishinde SIMBA 23 mtibwa 0 au mlitakaje? Hivi miaka yote timu haimalizi misimu miwili lazima kocha mpya. ...au nambiye ni lini timu ilikuwa na kocha MZURI ? zaidi ya kufukuzwa tu....tubadilike...hapo viongozi wana wachezaji wao hawapangwi...
 
Back
Top Bottom