Hans Van Plujim Ajiuzulu


ameshatangaza kujiuzulu na barua kauandikia uongozi taari.
 
Yanga wehu sasa kocha yule ana shida gani, tukiweka pembeni ushabiki, Yanga ina kikosi kikali sana,duuuuuuh wabongo kweli vichaa

Kosa la kocha ni kushindwa kumfunga Simba pamoja na mbeleko za refa, ponjoro kachukia fedha za kutengeza matokeo katoa na bado timu imeshindwa kuifunga Simba, inamaana bila kutoa hela kuhonga waamuzi na baadhi ya wachezaji hali ingekuwa mbaya zaidi. hicho ndicho kinachomuuma zaidi ponjoro.
 
Be consistent. Umesema Yanga kama .....'wasingekuwa na washambuliaji wazuri kwa kiwango cha Tanzania wangefungwa ila Kagera walishambuliwa sana kiasi cha .....'. Halafu kwenye maelezo hayohayo unasema '....... kama walivyoihujumu Kagera juzi.....'. Tushike lipi kati ya mawili haya yanayotofautiana?
 
Watu wanajiandaa kimataifa uwezo wa kocha umefikia mwisho pale
Haiwezekani. Huwezi kumfananisha Pluijm na kocha huyu mpya. Ndio maana Yanga wenyewe hawakuamua kumfukuza Pluijm bali kumpa cheo kikubwa zaidi ya huyo kocha mpya; Mkurugenzi wa Ufundi. Na usifikirie kwamba angepunguziwa mshahara, wala kwamba huyu mpya angekuwa na mshahara sawa au mkubwa zaidi ya wa Pluijm. Walichotaka kufanya Yanga ni kuua ndege wawili kwa jiwe moja. Kuongeza nguvu kwenye mashindano ya Kimataifa kwa kuwa na jopo pana na lenye uweledi zaidi kiufundi huku ikimwondoa Pluijm kwenye kuhusiana moja kwa moja na wachezaji ili uongozi uwe na sauti angalau siku za mechi na Simba. Na ndio maana hawakumwarifu Pluijm mapema kwa kuamini kwamba asingekataa nafasi ya ukurugenzi, bila ya kujua kwamba yeye ni Mzungu. Nia yao ilikuwa njema, ila utashi uliizidi busara. Hata njia ya jehanamu imejaa tele nia njema. Mtaka nyingi nasaba hupatikana mwingi msiba.
 
Sijaelea ulichoandika ulikua unamaanisha nini, ila inaonyesha maneno yaliondolewa hayakuwa na staha, jifunze kuto husisha maneno mabaya, ukijiona una hasira usipende kuchangia changia hizi msda, pili usipende kukaa kwenye makundi ya watu. Ila ni kukumbushe tu, mchezo huu haitaji hasira.
 
Hajajiuzulu bali Katimuliwa!! Hebu Nyoosha Maelezo ! Kuwa Muwazi Likocha Lenu Limepigwa Na Chini!!! Chaneta FC mutamuajiri Hata Gurdiola Msimu huu lakini Simba Hakamatiki Kaeni Mukijua..
 
Samahani kama umekwazika na maelezo yangu. Lakini mbona naona maneno yote niliyoyatumia ni ya Kiswahili na ya kawaida sana! Maneno pekee yasiyo ya Kiswahili niliyotumia ni 'be consistent'. Ninakuhakikishia kwamba hayo si matusi. Ila kwa sababu yamekukwaza, sitayatumia tena hayo wala mengine ya lugha hiyo kwako.
 
Siajelewa management ya Yanga kwann inamtoa Plujim wakati timu ya Yanga iko vzr sana.

Je, kocha anatolewa kipindi timu ikiwa vizuri au ikiwa vibaya?
 
Umeanza vizuri ila umevuruga mwishoni. Hii ishu ya Yanga kuhujumu mechi kwanini msiipeleke mahali husika? Kama mnaona TFF hamtasikilizwa ipelekeni FIFA ili hawa wanaonunu mechi waadhibiwe.. Vinginevyo itakua ni taarabu tu kama taarabu nyingine..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…