Huyu dogo anaimba sana, hii EP yake ngoma zote ni kali, sijaipenda moja tu ile kaiita Kiberenge.
Nafikiri akikaza atatoboa tu, hao WCB wanaanza kuwa sio relevant hivi karibunu.. So akichanga karata zake vizuri anaenda kuwa the next big thing Tanzania will ever see, anaimba sana mpaka anakera huyu bwana mdogo!
P.S Ni kama vile madogo wamekuja kuwafundisha kaka zao jinsi ya kuimba na sio zile kelele wanazotupigia wao wakidai ni nyimbo. Mfano yule Killy wa Harmonize, anaimba kinoma yule dogo... Ana ngoma inaitwa 'Mwisho' lile pini ni mwisho kweli! Mac Voice wa Rayvanny nmesikiliza EP yake nae anaimba kinoma, EP yake imenyooka kasoro ile Amapiano aliyoweka ni utumbo. Ibrah wa Harmonize ndo hata haina haja ya kusema mengi, huyu janja akitoa ngoma basi kaamua tu. Dogo MeshAmazing mshindi wa BSS 2020 ana ngoma yake nae ile ya kuitwa 'Nakufuata' ni kali mnoo... Pia kuna huyu wa kuitwa Lody Music anaimba kinoma, nilijua amebahatisha ile ngoma yake 'Kubali' ila amekuja kuachia 'Promise' aisee his future kwenye bongoflava industry is soo fvkn promising!