Hanstone kinachomkwamisha ni kiburi au wanamsingizia na kumuonea?

Hanstone kinachomkwamisha ni kiburi au wanamsingizia na kumuonea?

Watu wako shamba huko wanawaona kwenye tv hawajui ukweli.

Wakina Moni Centrazone na Nuhu mziwanda wanashinda Kijitonyama Kama machokoraa ila ukiwaona Instagram utasema wanaishi ulaya.

Hawa wasanii nawajua na ninajichanganya nao ni wachache Sana wanayaishi Yale maisha ya kwenye mtandao
Yaani mkuu, sometimes ni kukaa kimya Kwasababu hao wasanii wenyewe pia ni wana, tunajua wanavyosota hivyo tunalindiana heshima tu.
 
Mkuu kwani hapa tunalinganisha label za Muziki ??

Mjadala hapa ni maslahi ya wasanii, bora hata kina Mutta wamewadhulumu kina Saida Karoli halafu wamekaa kimya.

Kuliko sasa hivi mtu kujifanya anakusaidia anakusaidia wakati UNAFIKI tu
mm sikatai kuwa maigizo katika uhalisia hamna, hapana nakubali kabisa maisha ya kwenye mitandao hayana uhalisia kwa kiasi kikubwa. Ila kwa hatua wanazopiga wasanii wa wcb na wachache baadhi zinalidhisha ukiangalia na huko nyuma mziki ulipotoka.
 
Na wewe ukaamini?
Nimeamini sababu walipelekana mpaka Basata na WCB walikuwa wakidai chao na sasa kila mtu yupo kivyake baada ya kulipana.

LABDA KAMA WEWE UNA USHAHIDI MWENGINE ,UNAWEZA UKANIAMBIA JF NI JUKWAA HURU.

ENHEE KWA NINI WEWE HUJA
MUAMINI KONDEBOY?
 
mm sikatai kuwa maigizo katika uhalisia hamna, hapana nakubali kabisa maisha ya kwenye mitandao hayana uhalisia kwa kiasi kikubwa. Ila kwa hatua wanazopiga wasanii wa wcb na wachache baadhi zinalidhisha ukiangalia na huko nyuma mziki ulipotoka.
Mkuu hapa No hating.

Ni kweli Muziki wa bongo fleva umeanza kulipa. Ila haulipi kwa wasanii mkuu.

Kuna genge la watu ambalo hata siyo wasanii ndio wanaofaidi matunda ya Muziki.

Huyo Diamond anafaidi kwa kuwa hilo genge limemwona ni fighter na hivyo limeamua kumfanya Partner.

Chain nzima ya burudani bado wana hali tete mnoo: Wasanii, Producers, Directors, Models, Social Media marketers, n.k
 
Lavalava anaishi masaki kwa mshikaji wetu Hana maisha yoyote.

Huyo Rayvanvy alikuwa kapanga tabata ghorofa kashindwa kulipa.

Mboso anaishi Mbweni kapanga ghorofa.

By the way wana maisha kwa level ya mtanzania ni mazuri kiasi. Ila hayaendani n majina Yao.
Kuna waongo na kuna wewe
 
Mkuu hapa No hating.

Ni kweli Muziki wa bongo fleva umeanza kulipa. Ila haulipi kwa wasanii mkuu.

Kuna genge la watu ambalo hata siyo wasanii ndio wanaofaidi matunda ya Muziki.

Huyo Diamond anafaidi kwa kuwa hilo genge limemwona ni fighter na hivyo limeamua kumfanya Partner.

Chain nzima ya burudani bado wana hali tete mnoo: Wasanii, Producers, Directors, Models, Social Media marketers, n.k
Basi hali ni mbaya sana, maana wenzetu wamepiga hatua sana. Wimbo mmoja mtu anatengeneza ukwasi kabisa.
 
Basi hali ni mbaya sana, maana wenzetu wamepiga hatua sana. Wimbo mmoja mtu anatengeneza ukwasi kabisa.
Mkuu muziki una stress sana. Wewe waone tu wasanii hivyo hivyo.

Tena ukipata jina kubwa halafu huna hela, utapata tabu sana. Utakuwa unasalimia kila mtangazaji wa Radio hata kama ni mdogo wako ili akupigie ngoma zako ili upate Show 🤣🤣🤣 ( hapa kina Dozen wameabudiwa sana )
 
😂😂😂😂 dah maisha haya.
 
Tutake tusitake WCB wanajitahd bhana , wasanii wao wapo vizur japo wanatofautiana mana ni ukwel unapata kulingana na unachoingiza eg lava lava huwez mfananisha na Rayvan .... Kuhusu maisha Yao ya social media kuwa tofaut na Uhalisia hlo ni swala la kawaida , hata mtu ukiwa na Ka mshahara Ka laki nne Kwa mwez uwezo wa kufake maisha unao , just kuwa na simu Kali ,unainstal app za Adobe Photoshop na lighting ,na app kibao za kuscan na kuedit picha ,kuwa na vinguo nguo ,na kuvist sehemu nzur nzur mara moja moja .... Mtandaoni unaonekana don

Wasanii wa WCB siyo choka mbaya hyo hata kama mtandaoni wanaonekana smart , nakataa mpak Kesho , huenda ni chuki Tu za watu kuwa-undermine na kujifanya tunawajua....

Huyo konde boy mnayemtetea nyie haters wa WCB na kumuita mwanaume asingepata mema yote hayo kama WCB ingekuwa na wasanii choka mbaya .....
 
Una miaka mingapi mkuu??

Jiweke mbali na Instagram kidogo akili yako ikurudie urudi katika hali ya kawaida.

Hao wasanii huwajui zaidi ya kuwaona Instagram.

Labda nikwambie kitu, hao Wasafi kabla hawahama Sinza nimeenda sana pale. Kuna msanii ( simtaji ) nilikuwa nampeleka kwa bodaboda. Enzi hizo huyo Qboy bado yupo hapo na alikuwa anavimba balaa. Achana na sasa hivi hata kula shida mpaka anatamani arudi awe anapata hata makombo hapo.

Mengine unayoyaona mitandaoni kuhusu wasanii, tumia na akili yako.

Ingia YouTube, check msanii anaitwa Peace Amorre ( huyo ameimba sana Twanga Pepeta na ni mdogo wake Asha Baraka ) tunakaa kaya moja.

Wasanii wa bongo ni wasanii haswaaaaa.
wasanii wa bongo ni wasanii haswaaaaaa
nimekuelewa sana hapa...
halafu mnaoishi kinondoni mnawafaidi sana hawa wasanii
 
Mkuu hapa No hating.

Ni kweli Muziki wa bongo fleva umeanza kulipa. Ila haulipi kwa wasanii mkuu.

Kuna genge la watu ambalo hata siyo wasanii ndio wanaofaidi matunda ya Muziki.

Huyo Diamond anafaidi kwa kuwa hilo genge limemwona ni fighter na hivyo limeamua kumfanya Partner.

Chain nzima ya burudani bado wana hali tete mnoo: Wasanii, Producers, Directors, Models, Social Media marketers, n.k
mwambie tu ukweli ilo genge ni la wauza unga
 
Huyu kijana wa Banza Stone Hanstone ninaamini ana kipaji kikubwa sana. Ameonesha uwezo mkubwa sana kwenye wimbo wa Iokote alioshirikishwa na Maua Sama, na hatimaye nyimbo zake mbili ailizozitoa hapo baadaye za acha lipite na I miss you mama. Pamoja na kwamba hizo nyimbo mbili alisema hazikuwa rasmi lakini zilituvutia wengi na kuona ni kijana mwenye bright future kwenye muziki.

Basi mambo yakawa mambo akajitoa kwenye management aliyokuwepo ya kina Abbah na Hanscana na kutokomea kusikojulikana. Ni zaidi ya mwaka sasa hajulikani yupo management gani, wapo waliosema yupo kwa S2kizzy na wengine wakasema anaandaliwa kuingia wasafi, wapo pia waliosema yupo chini ya Harmonize. Siku zinakwenda hakuna lililothibitika yeye mwenyewe hasemi yupo wapi amekuwa Kama Yahaya.

Lakini ni nini kilimtoa kwa Abbah na Hanscana ambako mwenzake Marioo ametulia na anafanya vizuri? Ni kiburi? Abbah process anasema Hanstone aliondoka bila kuaga ni pale alipomkemea baada ya kuiba wimbo walioufanya studio na kuuvujisha, baada ya kumsema akanuna akaondoka. Walipomwita kushoot video ya wimbo wa Chibonge akagoma kutokea hali iliyopelekea wakaondoa verse yake na kumweka gnako.

Akihojiwa na media bila kusema kilichomtoa kwa Abbah anawakana kwamba hakuwa ameingia nao mkataba wowote wa maandishi. Sasa mbona walimpora akaunti yake ya Instagram Kama ndiyo hivyo? Yaani bila mkataba wowote wakamshirikisha kwenye Iokote, Chibonge na kumrekodia nyimbo zingine? Mkataba ni lazima uwe umeandikwa?. Kisheria mkataba ambao ni lazima uandikwe ni wa ajira na kuuziana ardhi tu mingine inaweza isiandikwe na ikawa halali ili mradi kukiwa na ushahidi tu. Kwa hapa Kuna ushahidi wa kimazingira kuwa dogo alikuwa chini ya kina Abbah process na Hanscana na ameondoka kwa jeuri na kiburi.

Hanstone unapaswa ujirekebishe maana kwa staili hii hata labels kubwa unazozitegemea Kama Wasafi na Konde gang zitaogopa kukusaini maana jina lako limeshakuwa labelled kuwa ni kijana mwenye kiburi na dharau na asiye ambilika
Hili suala haliongelewi ila ingekuwakwa homeboy wa Tandale mwenzangu Naseeb watu wangetunisha misuli ya shingo kwa kutoa povu la maana
 
Back
Top Bottom