HOJA Hao wanaodaiwa kuwa matapeli wa Mtandaoni wamepataje taarifa za line yangu ya Vodacom?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Natumia Mtandao wa Vodacom, leo asubuhi nilienda kutoa fedha Saa 4:00, ilipofika Saa 7:00 hivi, nilipigiwa simu na mtu aliyekuwa akitumia namba binafsi alijitambulisha kuwa ni mhudumu wa Vodacom.

Nilianza kubishana naye na kumuuliza kwa nini ananipigia kwa kutumia namba binafsi badala ya njia rasmi za mawasiliano za Vodacom. Kilichonishtua zaidi ni kwamba wakati tunaendelea kubishana, huyo mtu alinitajia salio langu lote lililokuwa kwenye akaunti yangu, hadi kiasi cha senti zilizokuwepo, alinitajia taarifa hizo kwa usahihi kabisa.

Jambo hili limenitia hofu kubwa, kwa sababu ninaishi peke yangu na hakuna mtu ninayemjua ambaye anaweza kuwa na access ya simu au taarifa zangu. Nilirekodi mazungumzo hayo, na nina ushahidi unaoonyesha salio lililokuwepo kwenye akaunti yangu wakati tukio hilo linatokea.

Baada ya tukio hilo, nilijaribu kupata majibu kutoka Vodacom kuhusu huyo mtu amepata wapi taarifa za akaunti yangu na amewezaje kujua salio langu kwa usahihi kiasi hicho. Badala ya kupata jibu la moja kwa moja kuhusu chanzo cha taarifa hizo, nimeelezwa kwamba matapeli wana mbinu nyingi.

Pia nilifikisha suala hili TCRA, lakini majibu niliyopewa ni kwamba inawezekana mtu huyo amekuwa akinifuatilia kwa muda mrefu, hata kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivyo, bado sijapata jibu la msingi: mtu huyo alipataje taarifa sahihi za akaunti yangu na salio langu?

Kinachonipa hofu siyo tu suala la kupigiwa simu na mtu anayedai kuwa mhudumu wa Vodacom, bali ni namna alivyoweza kupata taarifa ambazo nilitegemea kuwa ni za siri. Kama kweli taarifa hizo zimetoka kwenye mfumo wa Vodacom, basi najiuliza zimefikiwaje kwa mtu huyo na ni kwa kiwango gani taarifa za wateja ziko salama.

Naomba Vodacom na TCRA walichunguze suala hili kwa kina na wanieleze chanzo cha taarifa hizo. Kama huyo hakuwa mhudumu halali wa Vodacom, nataka kujua aliwezaje kupata taarifa sahihi za akaunti yangu. Kama alikuwa mhudumu, basi ni muhimu kufahamu kwa nini anatumia namba binafsi kuwasiliana na wateja na ana mamlaka gani ya kuona taarifa za salio la mteja.

Naomba pia wataalamu wa masuala ya usalama wa mtandao na taarifa wanisaidie kuelewa jambo hili. Sitaki suala hili liishie kwenye maelezo kwamba “matapeli wana mbinu nyingi”; nataka kujua taarifa zangu zilipatikana wapi, nani aliweza kuzifikia, na ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha hali kama hii haitokei kwa wateja wengine. Tafadhali ficha utambulisho wangu.
 
huko bongo ila kitu dili , wewe unshangaa kupigiwa ukiwa umetoka kutoa hela? wenzio wstaafu ndio wanalizwa kila siku watu wana details zao mpaka check namba na account na mpaka salio lililopo muda huo wanajua, usicheze na nchi iliyojaa njaa ubabaishai, udini,ukabila na uchawa, hizo code zooote wanapewa na hao watumishi wenu feki wa serikali haramu ya mjane, jana naskia kafiw tena na mchepuko. mtajua tu kuwa bongo bahati mbaya.
 
Natumia Mtandao wa Vodacom, leo asubuhi nilienda kutoa fedha Saa 4:00, ilipofika Saa 7:00 hivi, nilipigiwa simu na mtu aliyekuwa akitumia namba binafsi alijitambulisha kuwa ni mhudumu wa Vodacom.

Nilianza kubishana naye na kumuuliza kwa nini ananipigia kwa kutumia namba binafsi badala ya njia rasmi za mawasiliano za Vodacom. Kilichonishtua zaidi ni kwamba wakati tunaendelea kubishana, huyo mtu alinitajia salio langu lote lililokuwa kwenye akaunti yangu, hadi kiasi cha senti zilizokuwepo, alinitajia taarifa hizo kwa usahihi kabisa.

Jambo hili limenitia hofu kubwa, kwa sababu ninaishi peke yangu na hakuna mtu ninayemjua ambaye anaweza kuwa na access ya simu au taarifa zangu. Nilirekodi mazungumzo hayo, na nina ushahidi unaoonyesha salio lililokuwepo kwenye akaunti yangu wakati tukio hilo linatokea.

Baada ya tukio hilo, nilijaribu kupata majibu kutoka Vodacom kuhusu huyo mtu amepata wapi taarifa za akaunti yangu na amewezaje kujua salio langu kwa usahihi kiasi hicho. Badala ya kupata jibu la moja kwa moja kuhusu chanzo cha taarifa hizo, nimeelezwa kwamba matapeli wana mbinu nyingi.

Pia nilifikisha suala hili TCRA, lakini majibu niliyopewa ni kwamba inawezekana mtu huyo amekuwa akinifuatilia kwa muda mrefu, hata kwa kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivyo, bado sijapata jibu la msingi: mtu huyo alipataje taarifa sahihi za akaunti yangu na salio langu?

Kinachonipa hofu siyo tu suala la kupigiwa simu na mtu anayedai kuwa mhudumu wa Vodacom, bali ni namna alivyoweza kupata taarifa ambazo nilitegemea kuwa ni za siri. Kama kweli taarifa hizo zimetoka kwenye mfumo wa Vodacom, basi najiuliza zimefikiwaje kwa mtu huyo na ni kwa kiwango gani taarifa za wateja ziko salama.

Naomba Vodacom na TCRA walichunguze suala hili kwa kina na wanieleze chanzo cha taarifa hizo. Kama huyo hakuwa mhudumu halali wa Vodacom, nataka kujua aliwezaje kupata taarifa sahihi za akaunti yangu. Kama alikuwa mhudumu, basi ni muhimu kufahamu kwa nini anatumia namba binafsi kuwasiliana na wateja na ana mamlaka gani ya kuona taarifa za salio la mteja.

Naomba pia wataalamu wa masuala ya usalama wa mtandao na taarifa wanisaidie kuelewa jambo hili. Sitaki suala hili liishie kwenye maelezo kwamba “matapeli wana mbinu nyingi”; nataka kujua taarifa zangu zilipatikana wapi, nani aliweza kuzifikia, na ni hatua gani zinachukuliwa kuhakikisha hali kama hii haitokei kwa wateja wengine. Tafadhali ficha utambulisho wangu.

Jibu la uhakika ni hili.

Wafanyakazi wa Mitandao ya simu. Wamevuta taarifa za wateja wao nje. Na kuzitoa kwa hao wapigaji.

mara nying inakuwa ni siku 1 au mbili nyuma. Sasa wamekuta ww salio halijaongezeka/kupungua ndan ya hizo siku 2 na ndio maana wakapatia. Na ww ukahisi labda ni mtoa huduma kwa wateja anangalia salio kwa wakat huo huo.

Pia TCRA pamoja na Polisi wanafanyiaga uchunguzi haya masuala.
Nina ndugu yangu yuko Polisi wiki ya Pili sasa kwasababu ya ishu kama hii.
Ni mfanyakazi wa vodacom.

Kwahiyo taarifa zinatolewa nje na wafanyakaz wa mitandao husika. Na TCRA pamoja na Polisi huwa wanawachukulia hatua hao wafanyakazi kama taarifa ikarepotiwa vizur.
Kama alivyofanya mtoa mada.
 
Hizi branch ndogo ndogo za mitandao ya simu , Wana access limitation ya ku view only na taarifa za mteja.
So Kuna baadhi ambao sio waaminifu
 
Wanaovujisha ni wafanyakazi makao makuu.

Kitengo cha Mpesa.
Wana access nying ya kuona na kuvuta taarifa za wateja wengi kwa wakat mmoja.

Anaweza akapull labda wateja wa Dodoma. Wenye salio juu ya 1 Mill . Mpesa. Na dk 0. Report inakuwa in excel.

Anaisave kwa desktop yake. Anaingia na whatsapp web. Anaiiaccess report na kumtumia mpigaji.
Very simple. Ni jambo la dk 0.
Sema sasa lazima log zionekane.

Sasa mtu akireport polisi na TCRA. Na wakaenda kuangalia akaunti ya huyo mteja ni access ya nani iliigusa na kwanini uliigusa. wakat mteja hakuomba wala kuhitaji huduma ambayo ilibidi uichungulie akaunt yake.

Kwahiyo mfanyakazi wa Vodacom anafahamika kwa namna hiyo.
 
Voda wapo very strong, nadhani watalifanyia kazi.ni Moja ya mtandao Bora ambao mifumo Yao ipo vzr
Wahuni wako kila mtandao.

Kuna mtu anaweza akawa yuko royal leo. Na akawa na info za wateja wengi. Akazitunza. Na siku akipata kazi sehem nyingne.
Atazitoa hizo info kwa wapigaji.

Kwa mfano kuna wateja miaka na miaka . Line zao huwa zinapitisha na kuhifadhi hela. Na wao wanazijua.

Siku huyu mfanyakazi ambaye anayo excel ya akaunti elfu 1 za namna hii. Akiacha kazi na baadae akaamua kuwapa mapigaji.
Ni hatari. Na hili ndilo linafanyika sana tu kwenye hii mitandao.

Na kutambua ni nan kavujusha kwa scenerio hii ni ngumu.

Sasa huu ni mfano tu. Namna ya kutoa info ziko nying na wafanyakaz wa mitandao wanaweza wasifahamike.
 
Jibu la uhakika ni hili.

Wafanyakazi wa Mitandao ya simu. Wamevuta taarifa za wateja wao nje. Na kuzitoa kwa hao wapigaji.

mara nying inakuwa ni siku 1 au mbili nyuma. Sasa wamekuta ww salio halijaongezeka/kupungua ndan ya hizo siku 2 na ndio maana wakapatia. Na ww ukahisi labda ni mtoa huduma kwa wateja anangalia salio kwa wakat huo huo.

Pia TCRA pamoja na Polisi wanafanyiaga uchunguzi haya masuala.
Nina ndugu yangu yuko Polisi wiki ya Pili sasa kwasababu ya ishu kama hii.
Ni mfanyakazi wa vodacom.

Kwahiyo taarifa zinatolewa nje na wafanyakaz wa mitandao husika. Na TCRA pamoja na Polisi huwa wanawachukulia hatua hao wafanyakazi kama taarifa ikarepotiwa vizur.
Kama alivyofanya mtoa mada.
watu wengi wanalizwa halafu nahisi kuna age group wanalitarget wayu wenye umri kuanzia miaka 55 kuendelea juu wanaibiwa sana pesa
 
Wanaovujisha ni wafanyakazi makao makuu.

Kitengo cha Mpesa.
Wana access nying ya kuona na kuvuta taarifa za wateja wengi kwa wakat mmoja.

Anaweza akapull labda wateja wa Dodoma. Wenye salio juu ya 1 Mill . Mpesa. Na dk 0. Report inakuwa in excel.

Anaisave kwa desktop yake. Anaingia na whatsapp web. Anaiiaccess report na kumtumia mpigaji.
Very simple. Ni jambo la dk 0.
Sema sasa lazima log zionekane.

Sasa mtu akireport polisi na TCRA. Na wakaenda kuangalia akaunti ya huyo mteja ni access ya nani iliigusa na kwanini uliigusa. wakat mteja hakuomba wala kuhitaji huduma ambayo ilibidi uichungulie akaunt yake.

Kwahiyo mfanyakazi wa Vodacom anafahamika kwa namna hiyo.
nikiweka pesa kuanzia milioni 5 kwenye simu huwa napata calls nyingi za matapeli ambao wengi wanatumia lines za halotel na TTCL pia sms kibao za matapeli. Ila kuna rule nimejiwekea huwa sipokei namba nisiyoifahamu.
 
Back
Top Bottom