Hapa Dar ni maduka gani yanauza office shoes original?

Kama unaweza kununua kiatu 400,000/- kwanini usiagize online from US au UK?
Sure; sema wakati mwingine kiatu inabidi ufitishe mguuni

Mimi binafsi kuna viatu 42 navaa, vingine 43 ndo inafiti; shida ya online huna hiyo room kujaribu
 
Karume sehem Gani nipe namba yake ila Kwa kuongezea pia Kuna mwamba karume insta anatumia Mauwezo org nimemvulia shati Kwa viatu vya kijanja toka mambele
Kuna mwamba mmoja yupo pale ilala kwenye spare za magari wanauza mitumba mizuri sana na wengine wapo makumbusho kama unaingia standi wapo vizuri
 
Kuna mwamba mmoja yupo pale ilala kwenye spare za magari wanauza mitumba mizuri sana na wengine wapo makumbusho kama unaingia standi wapo vizuri
kama unaweza bila kusita nifowadie namba zake inbox kama unazo ili niweze wacheki niko mkoani mie mzee ila ugonjwa wangu ni viatu tu
 
Lazima afilisike unakaa na kiatu 2years unategemea angesurvive vipi?
 
Kama unaweza kununua kiatu 400,000/- kwanini usiagize online from US au UK?
Kama anaweza nunua kiatu 400k kwanini asinunue na gari tu! Huyu viatu vinaisha kwakuwa anatembea kwa miguu sana
 
Nunueni magari viatu vitadumu utakuwa unanunua matairi tu
 
Nunueni magari viatu vitadumu utakuwa unanunua matairi tu
Kwani ukiwa na magari ndio viatu haviishi? au unaingia na gari mpaka Mlimani City ndani kabisa. Na vipi kama ni mtu wa mazoezi jogging n.k utatumia gari?

Kuna Rais mmoja wa nchi za Ulaya aliwahi kuvaa kiatu kimeisha sole kidogo upande ina maana nae hana magari. Binadamu pamoja na kuwa na nyenzo zote lakini lazima atembee umbali fulani kwa siku kama hitaji la mwili sio kila kitu unatumia gari tu kwanza parking zenyewe maeneo mengi ni shida mfano umeenda Kariakoo lazima upaki gari utembee kwenda kufanya shopping
 

Nunua Clarks, Piere Cardina, Gucci, Robert


Maduka Mlimani City, Mwenge, Postal,Sunderland Kariakoo
Sunderland vitu vyao fake, siyo original kabisa. Ila kwenye macho it seems kama original. Nadhani woolworth etc, yaani tafuta maduka yaliyopo posta. Mfano pale duka moja la mchaga posta ya zamani opp na tcb (bank ya posta zamani ) ana viatu bomba. Maduka mengine mlimani city. Kariakoo wafanyabiashara wanashirikiana na wachina ku imitate products zifanane na original kwa sababu bei ya kariakoo ni ndogo
 
1. Tembelea jamaa wanaitwa Anand Boot wako mtaa Samora/India St. Pembeni ya ile Garden inayokabiliana na NBC Samora ingawa kwa sasa kdogo wameanza kuchakachukua. Wana reputation ya kuuza viatu OG since 1970s

2. Check jamaa wanaitwa NGOZEE wako at the entrance gate ya MAYFAIR
Pale wana single room factory ambayo inatowa vitu visivyo vya kawaida. Ila jitayarishe kwa bei
Nao wana reputation tangia 1970s

3. Otherwise sweep along Samora Avenue

4. Lenga mtumbani, mwaka 2019 nililenga a German brand inaitwa JOMO for only 15k and it was almost new. Ile kiatu naamini ntadunda nayo mpaka 2025 In Shaa Llah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…