Hapa Kazi Tu (HKT) kiwe chama kipya cha kisiasa Tanzania kitakachoenzi falsafa na maono ya Hayati Dkt. Magufuli na kiwe tegemeo la Watanzania

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2019
Posts
1,521
Reaction score
4,381
Sisi tunaamini kwenye misimamo ya Magufuli ndiyo hasa misingi ya Chama Cha Hapa Kazi Tu... HKT. Kwenye hii misingi tutajenga Tanzania imara sasa na kwaajili ya vizazi vijavyo.

Uhuru wa kiuchumi ni jambo linalowezekena kama tutasimamia vizuri maliasili tulizonazo kwa manufaa ya wote.

Hatutakaa kimya pale tunapohisi rushwa, wizi na upotevu wa rasilimali za nchi unapotokea.
 
Mnakisajili lini?

Isije kuwa gumzo tu la JF.
Tumeanza taratibu maana tunaona CCM tunayoitaka haijirekebishi inarudia tabia za zamani za mikataba ya hovyo hovyo Rais wa nchi anakuwa mtu wa kujipendekeza kwa watu ambao hawakumchagua vyama vingine vya Upinzani vimekuwa matawi ya CCM, na waporaji wa rasilimali zetu tunataka ulinzi imara na kwa wivu wote wa rasilimali za nchi yetu tunawataka viongozi wa nchi wazidishe vita dhidi ya Rushwa kwa vitendo
 
"hapa kazi tu" ni slogan .. tafuta jina sahihi la chama.

pili kama chama kinajengwa arround magufuli.. basi hakifai. maana taasis ndio inatakiwa kuwa imara si mtu fulani.

pili una uwezo wa ku survive nje ya ccm ww? wapo waliojaribu sana lakin hawakudumu muda mrefu.
utaweza survive nje ya ccm?
 
utaweza survive nje ya ccm?lengo

"hapa kazi tu" ni slogan .. tafuta jina sahihi la chama.
pili kama chama kinajengwa arround magufuli.. basi hakifai. maana taasis ndio inatakiwa kuwa imara si mtu fulani.

pili una uwezo wa ku survive nje ya ccm ww? wapo waliojaribu sana lakin hawakudumu muda mrefu.
utaweza survive nje ya ccm?
Lengo la HKT ni kurudisha faraja kwa Watanzania juu ya ulinzi wa Rasilimali zao “Hayati Dk John Magufuli alikuwa mzalendo wa kweli, alikuwa na maono, alijitoa kwa nguvu zote, alikuwa na uthubutu sana, mtu wa vitendo na muumini wa matokeo na kuchukua hatua za papo kwa papo,
 
Tumeanza taratibu maana tunaona CCM tunayoitaka haijirekebishi inarudia tabia za zamani za mikataba ya hovyo hovyo Rais wa nchi anakuwa mtu wa kujipendekeza kwa watu ambao hawakumchagua vyama vingine vya Upinzani vimekuwa matawi ya CCM, na waporaji wa rasilimali zetu tunataka ulinzi imara na kwa wivu wote wa rasilimali za nchi yetu tunawataka viongozi wa nchi wazidishe vita dhidi ya Rushwa kwa vitendo

Siku ukipata usajili tujulishe tujue uko serious na si mtu wa soga tu.

Rais anatakiwa kujali wananchi wote, si waliomchagua tu.

Kwa sababu ni rais wa wananchi wote, si waliomchagua tu.

Unaelewa hilo?

Unaelewa kwamba kama kweli unapiga vita rushwa hutakiwi kumshobokea Magufuli?

Magufuli alihalalisha rushwa akasema ni hela ya traffic kupigia brashi viatu tu.

Magufuli aliwapa mdogo wake na hawara yake nyumba za serikali kinyume na utaratibu.

Huyo ndiye mtu wa kumshobokea katika vita dhidi ya rushwa?
 
Ha ha ha.
Once bitten twice shy...

Tuliwapa...

Hamkuweza....

Mwalimu aliona mbali jameni.
 
Tumeanza taratibu maana tunaona CCM tunayoitaka haijirekebishi inarudia tabia za zamani za mikataba ya hovyo hovyo Rais wa nchi anakuwa mtu wa kujipendekeza kwa watu ambao hawakumchagua vyama vingine vya Upinzani vimekuwa matawi ya CCM, na waporaji wa rasilimali zetu tunataka ulinzi imara na kwa wivu wote wa rasilimali za nchi yetu tunawataka viongozi wa nchi wazidishe vita dhidi ya Rushwa kwa vitendo
Wazo zuri, mtawapata wanyonge ambao ndio wengi.
 
Kwa staili hii tunayoendeleanayo mbereko ya CCM haina mwenyewe 2025. Yuko mtu atabembeleza na mimi niachiwe kama wenzangu ninuse awamu mbili.
 
Siku ukipata usajili tujulishe tujue uko serious na si mtu wa soga tu.

Rais anatakiwa kujali wananchi wote, si waliomchagua tu.

Kwa sababu ni rais wa wananchi wote, si waliomchagua tu.

Unaelewa hilo?

Unaelewa kwamba kama kweli unapiga vita rushwa hutakiwi kumshobokea Magufuli?

Magufuli alihalalisha rushwa akasema ni hela ya traffic kupigia brashi viatu tu.

Magufuli aliwapa mdogo wake na hawara yake nyumba za serikali kinyume na utaratibu.

Huyo ndiye mtu wa kumshobokea katika vita dhidi ya rushwa?
Mkuu namaanisha Rais hatakiwi kujipendekeza kwa wawekezaji wenye tabia za Carl Peter's, simaanishi Watanzania
 
Sisi tunaamini kwenye misimamo ya JPM ndiyo hasa misingi ya Chama Cha Hapa Kazi Tu... HKT. Kwenye hii misingi tutajenga Tanzania imara sasa na kwaajili ya vizazi vijavyo.
Uhuru wa kiuchumi ni jambo linalowezekena kama tutasimamia vizuri maliasili tulizonazo kwa manufaa ya wote.
Hatutakaa kimya pale tunapohisi rushwa, wizi na upotevu wa rasilimali za nchi unapotokea.

Nini msimamo wa chama chenu tarajiwa HKT kuhusiana na katiba mpya?

Funguka mwanakwetu, wanachama waanzilishi mwaweza anza nao tokea kwenye uzi huu huu.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom