IsayaMwita
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 1,127
- 140
Kwa jinsi Muungwana anavyo wajibika kwa sasa si ndiyo anazidi kukiruka kiunzi 2010? hatujui tutamrushia madongo yapi, kwani yeye kama yeye hakika anaendelelea kuisafisha ile njia,
Tuangalie tusije tukakosa mshiko, !!!!!
Nadhani zile hoja za kufichua ufisadi tungeanza sasa si mwaka jana, hawa jamaa wanaendelea kujisafisha
Sijaelewa kwamba wanapowapeleka akina Mramba baada ya uchaguzi watawafutia kesi zao ama?
Nimeipenda ile style yao.
Ama nina makengeza?
Toa evidence ya kile alichawajibika nacho. Yaani weka progress report yake tangu day alipochukua madaraka Dec 2005????!!! Baada ya kuweka real progress report yake hapa then utaweza kutuambia kuwa ametupiga bao. Sikubaliani na wewe kabisa. Ninachoona ni viini macho au mazingaombwe tu. We need strict proof kwa post yako. Thanks.
Maane hebu ni evidence gani utahitaji kuona kama jamaa anaweza hata kumsariti hata rafiki yake mpenzi(Rowasa)
Kamsaliti vipi? Kajiuzulu UPM na mafao kalamba huku ikijulikana wazi ni mwizi, mwenzake badala ya kuwa makini anasema 'ajali ya kisiasa', huo ndio unauita usaliti. Prove to us, sio kuja na hoja za kusafisha watu hapa JF, hapa sio mahala pa kuleta kitu kisichokuwa na kichwa wala miguu. Think twice!
mpigafilimbi; Mkuu sipo hapa kwa ajili ya kumsafisha mtu hapa, ila nipo hapa kuelezea hisia zangu, mpigafilimbi; nadhani wewe utakuwa na mawazo mgando yasikubali ukweli wa mambo, pale mtu anapofanya vema ni vizuri akapongezwa.

Naona si tu una makengeza bali huoni kabisa. Kumbuka major objective/goal ya JK alipoingia madarakani (ambapo alikuta hazina imejaa) ni "maisha bora kwa kila mtanzania". Achilia mbali ahadi kibao za kipuuzi alizotoa. Je amefanikiwa nini katika hilo?
1. Inflation rate from 6% (2005) to 13.5% (today)
2. Elimu ya juu, from 100% gvt sponsorship to 80%, 60% and none.
3. Bei ya umeme imepanda sana
4. Consumer Price Index mbaya
5. Aliahidi kuongeza mishahara ameshindwa, ametumia EPA funds kulipa nauli za walimu
6. Kilimo: Bei ya mfuko wa mbolea TZS 15,000 (2005) mpaka TZS 125,000 per bag (today)
etc.
Amefanikiwa nini? Au bado unaangalia ze comedy ya JK?

Hapa tunamukumu bila kuitazama dunia kwa sasa,
Kama ndiyo tuseme nini kuhusu UGHAIBUNI tunaposhuhudia uchumi ukiporomoka?
Kwani hayo si mafanikio? Au mafanikio ni positive tu?
Mheshimiwa anajaribu kujipapatua lakini dawa yake ipo jikoni si ameenda kuchezea Zanzibar basi we wacha tu ,ubabaishaji wake karibu utaanikwa, yaani lazima mikogo itamwondoka na hataweza kuamini kama alivyoanza sivyo alivyo hivi sasa ,na hili limesababishwa na ile heshima aliyopewa na matumaini aliowekewa ukiongezea na ahadi zake ambazo ndizo hizo zitakazomporomosha ,Kikwete kwa kweli hasa mmoja kati ya vviongozi ambao wananchi wengi walikuwa na tamaa juu ya uongozi wake hata wengine kufikia kusema ni Chaguo la Mungu hapo si padogo ,na umma mzima wa WaTanzania ulikuwa na imani nae kuwa Nchi imepata kiongozi imara, naweza kusema mapenzi ya WaTanzania kwake hapo mwanzo yalikaribiana na Moringe Sokoine.
Hapa tulipo naamini kabisa Kikwete anaona bado hali hiyo ipo ya kupendwa na wananchi ,ila kwa taarifa tu hali hiyo imeshaanza kuyeyuka kama mfuko wa plastiki unapouweka kwenye moto ,huwa unajiunguza wenyewe na Mheshimiwa hapo alipo anajiunguza mwenyewe ,mambo na vituko vyake ndivyo vinavyommaliza ,na ikiwa hivi sasa anamalizwa na vituko vyake ,je itakuwaje wapinzani watakapoamua kumkoma nyani ?
Wakuu, mimi ninashangaa sana kusikia kuna mafanikio yoyote kiuchumi, kijamii, kisiasa, kiusalama, kielimu, kiafya, kimiundombinu, ki... tangu tumalize uchaguzi mwaka 2005. Sioni lolote.
Nikiangalia sekta zote muhimu, sioni lolote. Ninachoanza kuhisi ni kuwa CCM sasa imechoka kuongoza nchi, ama inajaribu kuona kama waTanzania wanaweza kuwatosa katika uchaguzi wowote wa Rais, Wabunge na Madiwani. Nasema hivi kwakuwa katika historia ya siasa nchini tangu kuanzishwa kwa vyama vingi, haijawahi kutokea performance ya chini kiasi hiki na bila kuwa na nia ama njia inayoonekana wazi ya ku-improve hali ilivyo.
CCM ikishinda 2010, itakuwa ni kwasababu wapinzani wameamua ishinde, na wapinzani hawatashinda tena hadi siku wote humu tutakapokuwa wazee wa kusagiwa chakula na kulishwa (baada ya meno yote kuisha mdomoni na macho kupoteza maono).
Sisemi hivi kwa kuichukia CCM. Ila nasema hivi kwa kuonyesha ukweli wa hali ilivyo.