Pole sana ndugu yangu.Kwanza inaonekana kuwa umeshakuteka,uko chini ya himaya yake.Maana kwa kawaida wanawake wapenda kucontrol,hivyo umeshajiingiza kwenye controling yake.Mmeishi kama mume na mke wakati hujakamilisha zoezi kama kujitambulisha na yeye kuweza kukubalika kwenu.Jaribu kumweka na dada zako au mama yako mzazi halafu usikilize comment zao.Ikiwa na wao wataona uonavyo wewe achana naye tafuta wa kaliba yako hamtaweza kuishi pamoja kwa maisha yenu yote.
Ikiwa ni mkristo usiingie mkenge kwa kujaribu ukifikiri atabadilika baadaye.Huo ndio utakuwa mwisho wa ndoto zako.USIINGIZE HURUMA kwenye suala nyeti kama hili.