Hapa nchini ukipiga namba za dharura wanafika kusaidia?

Hapa nchini ukipiga namba za dharura wanafika kusaidia?

Joined
Aug 5, 2022
Posts
88
Reaction score
119
Ndugu Zangu hii kitu naiwazaga Sana. Kuna huduma zinatakiwa zitolewe Kwa uharaka mkubwa na Kwa nchi za wenzetu ukifanya hivyo ukapiga hizi namba mfano
Screenshot_20220809-085336.jpg

Ukapiga mamlaka mengine za huduma za dharula haichukui dakika washaamsha safari Kwa Kasi ya kubwa. Hapa bongo vipi???

Najua pia tupo wengi ambao hatukuwahi kufanya hivi japo wenzetu maulaya huko.. ukiona hata Mtu anakuangalia Sana, anakukodolea mimacho, unatoa taarifa polisi. Huku kwetu kama ni mwanaume mwanamke anakukodolea unaona yes katepeta. Anyway tuachane na hiyo.

Tujuzane hivi tunapopata matatizo common Sana mfano bongo vibaka na kajirani hawatoki kusaidia ukipigia hawa jamaa wanafika?? Hii Elimu bongo haipo kabisa MTU anapambania kivyake.

Ukiona sehemu Kuna watu kichakani unaachia tu.
 
Huku Tanzania ni 112 wapigie uongee nao kwanz uje utupe experience [emoji23]
 
Magari mengi ya dharura ya serikali huwa hayana mafuta, piga simu polisi utapata jibu.
 
Tz ukipiga simu ya dharura watakuja muda ambao dharura imeisha muda mrefu.
 
Mkuu kama mazingira yako yanahitaji msaada wa haraka Tunza namba personal za watu wa dharura hiyo ndio njia ya uhakika ya kupata msaada.
 
HAWAJI

Jaribu kuwapigia TAKUKURU, Polisi au wengineo
 
Huku kwetu hata nyumba ikiungua Zimamoto wanakuja muda ambao nyumba imeshateketea!
Polisi wanajitahidi kwa sehemu, na penyewe mpaka waje wafike kwenye tukio mambo yameshaharibika!
Nadhani hayo mambo mengine usiseme!
 
Back
Top Bottom