Kambaku
JF-Expert Member
- Nov 12, 2011
- 8,332
- 31,306
nachukia sana sms za aina hii manake zinawaadhibu watoto ambao ni safi kabisa.
Mbona serekali inawaadhibu waalimu ambao ni safi kabisa?
Ishu ya waalimu sio ndogo kama unavyoifikiria bi mkubwa, Binadamu yoyote, narudia tena yoyote, huwa anafanyakazi kutokana na matarajio ya ujira. Kweli unategemea waalimu waendelee kuwa na moyo wa kazi katika mazingira haya ya sasa? Na kama hawana moyo ulitegemea nini mrembo?
Serekali ilipotumia ubabe kurudisha waalimu kazini toka kwenye mgomo kweli hawakutegemea hili?
Bimkubwa kama wewe ni mwalimu ni dhahiri hufundishi primari za kijijini au st kayumba sekondari, basi kaa kimya tu usiwashangae wanaotaabika.
Ubarikiwe sana