Hapa patulivu, panaliwaza, kuna afya

Hapa patulivu, panaliwaza, kuna afya

muhosni

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
1,108
Reaction score
152
waheshimiwa,

mimi ndiyo kwanza nimejiunga. nimefanya ziara ya baadhi ya majukwaa na kuchungulia mijadala michache. Nilipoingia kwenye lile jukwaa la siasa heartbeat zangu ziliongeza kasi kwa sababu inaonekana watu wengi kule wana hasira sana.

Nilipokwenda International kidogo siyo mbaya, hata hayo majukwaa mengine.

Lakini nimeona nianzie hapa kwa sababu baada ya kuchungulia kwenye hili jukwaa heartbeat zangu zikarudi normal tena. angalau kuna life, na urafiki.

Nimeona pengine nianze tu na observation yangu hii. Kuna watu wamenifurahisha sana mijadala yao lakini kwa kuwa sijawasoma wote sitaki nifanye makosa ya kutaja baadhi na kuacha wengine. Pengine kadri navyozoea basi nitawataja walionifurahisha zaidi.

usiku mwema
Jamani naona siku inakaribia kwisha na ninataka kuwatakia happy valentine wote ambao mnatembelea hii thread. Niwataje lakini wachache wenu ambao mmenikaribisha na kunishauri na wengine tume chat kidogo kwenye hii thread.

Lizzy,
Ukwaju,
Remmy
Jaluo Nyeupe
Gaga
Chwechwe
Bigirita
VoiceofReason
Kaizer
LD
Firstlady
Michelle
BlueFace
Gurudumu
Bubu ataka Kusema
Mukoyo
Katavi
Desidii
Mkare
Chetuntu

Happy Valentine all!!!!!:clap2::coffee:
 
waheshimiwa,

mimi ndiyo kwanza nimejiunga. nimefanya ziara ya baadhi ya majukwaa na kuchungulia mijadala michache. Nilipoingia kwenye lile jukwaa la siasa heartbeat zangu ziliongeza kasi kwa sababu inaonekana watu wengi kule wana hasira sana.

Nilipokwenda International kidogo siyo mbaya, hata hayo majukwaa mengine.

Lakini nimeona nianzie hapa kwa sababu baada ya kuchungulia kwenye hili jukwaa heartbeat zangu zikarudi normal tena. angalau kuna life, na urafiki.

Nimeona pengine nianze tu na observation yangu hii. Kuna watu wamenifurahisha sana mijadala yao lakini kwa kuwa sijawasoma wote sitaki nifanye makosa ya kutaja baadhi na kuacha wengine. Pengine kadri navyozoea basi nitawataja walionifurahisha zaidi.

usiku mwema

karibu sana, ila hujasema kipi kimekuvutia huku jukwaa pendwa.
 
Asante Lizzy, ukweli wewe ni mojawapo ya watu walionivutia. michango yako haina papara, inafurahisha na kuliwaza at times

Asante sana na wewe utufurahishe!Umeshajifunza kugonga Thanks lakini?Usiwe mchoyo!
 
Asante kunifundisha, nilikuwa sijui, nimekugongea. Nilivyoona kuna baadhi ya watu wana muda mwingi zaidi kujadili jambo hapa. tatizo langu litakuwa muda ingawa naona nitaenjoy sana mara moja moja nikiwa na stress za kazi nakuja huku
 
Hahahahahaa karibu muhosni njoo huku MMU uondoe stress kule kwenye siasa kutakuhosni bure kama una roho ndogo!
 
karibu sana, ila hujasema kipi kimekuvutia huku jukwaa pendwa.

Lizzy amenifundisha kugonga thanks na tayari nimekupatia. kilichonifurahisha ni kwamba jukwaa hili watu wanaongea kama marafiki siyo maadui wanaohasimiana. kisha watu wanataniana wanabezana kidogo, na kuchekesha. mawazo mengi ni ya maisha ya kawaida kama vile watu mko mahali tu mnapiga soga. yaani kuna majukwaa mengine huko ni professional and serious talk. hii nayo ni nzuri lakini kwa mgeni kama mimi nilishutuka kidogo watu wanavyojibizana kwa ukali na kupingana
 
Hahahahahaa karibu muhosni njoo huku MMU uondoe stress kule kwenye siasa kutakuhosni bure kama una roho ndogo!

Yaani usipime. utadhani watu wanaonana na wameshikiana bastola? Ingawa mengine ya maana
 
Hivyo vinanihi vya kugonga thanks mbona sivioni tena?
 
Asante kunifundisha, nilikuwa sijui, nimekugongea. Nilivyoona kuna baadhi ya watu wana muda mwingi zaidi kujadili jambo hapa. tatizo langu litakuwa muda ingawa naona nitaenjoy sana mara moja moja nikiwa na stress za kazi nakuja huku
Karibu!Wala muda usikutishe...hata sisi tulianza hivyo hivyo!
 
Nimekugongea, lakini kwani usipoipata unajisikiaje? na mimi mbona hamnigongei
Unamgongea mtu unapoona umeridhishwa na point yake !Yani either umejifunza kitu..umekubaliana nae au umefurahia mchango wake!Kwahiyo inamfanya mtu ajisikie pouwaa!
 
Lizzy nakushukuru sana. Umenisaidia sana na najisikia umekuwa mwenyeji wangu hapa. Lakini sasa mimi nataka kulala, tutaonana kesho usiku mwema
 
Kama nilivyofanya hapo kwa lizzy.
 
Lizzy nakushukuru sana. Umenisaidia sana na najisikia umekuwa mwenyeji wangu hapa. Lakini sasa mimi nataka kulala, tutaonana kesho usiku mwema

Karibu sana hosni mubarak......karibu, huu ni msimu wa mapera
 
Back
Top Bottom