waheshimiwa,
mimi ndiyo kwanza nimejiunga. nimefanya ziara ya baadhi ya majukwaa na kuchungulia mijadala michache. Nilipoingia kwenye lile jukwaa la siasa heartbeat zangu ziliongeza kasi kwa sababu inaonekana watu wengi kule wana hasira sana.
Nilipokwenda International kidogo siyo mbaya, hata hayo majukwaa mengine.
Lakini nimeona nianzie hapa kwa sababu baada ya kuchungulia kwenye hili jukwaa heartbeat zangu zikarudi normal tena. angalau kuna life, na urafiki.
Nimeona pengine nianze tu na observation yangu hii. Kuna watu wamenifurahisha sana mijadala yao lakini kwa kuwa sijawasoma wote sitaki nifanye makosa ya kutaja baadhi na kuacha wengine. Pengine kadri navyozoea basi nitawataja walionifurahisha zaidi.
usiku mwema