Hapa Tanzania iundwe mahakama ya michezo ,kuamua makosa ya marefaree uwanjani

Hapa Tanzania iundwe mahakama ya michezo ,kuamua makosa ya marefaree uwanjani

Pain killer

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
14,361
Reaction score
21,680
Habari wakuu

Mimi naona mareferees hapa kwetu wamekuwa na makosa ya maksudi kabisa kwenye maamuzi uwanjani na hii ni kutokana na mihemko / ushabiki/ pesa wanazokuwa wamehongwa kuamua game ,hapa kwetu mareferee wengi hawapati stahiki zao vzuri hivyo basi kuuza match kwa kuweka pesa mezani ni kitu cha kawaida Sana na mbaya zaidi maamuzi yao ndio inakuwa hatima ya timu zote mbili .....haijalishi timu flani imepambana na ilikuwa imemzidi uwezo mpinzani ....

Penalty za hovyo ,magoli kukataliwa ,maamuzi ya wazi kabisa ambayo yanaonesha kuibeba timu flani ...

Mbaya zaidi baada ya mchezo tukirudi kwenye kanuni na Sheria tunakuta referee kakosea na timu flani imenyimwa point zake mhimu za halali ....lakini hakuna kitu cha ziada kinachofanyika baada ya kuona hayo yote kelele zinaishia mitandaoni na blaa blaaa....

Swala la football ni kitu ambacho watu wote wanashuhudia ,Kuna camera ,video zimechukuliwa kama haya yote yanaonesha timu flani imefanyiwa ujinga na referee basi mahakama ichukue mkondo wake ,hapa hakuna haja ya kumpa adhabu mwamuzi ,hapa ni kuhakikisha timu iliyofanyiwa unyama inapewa haki yake ,kama timu hio ilikuwa inastahili point 3 kabisa na referee kajifanya kupendelea haitakiwi iwe maamuzi ya mwisho ....mbona Tp mazembe alishawahi nyanganywa ubingwa kisa huu ujinga wa mareferee ..

Kama timu inaona kabisa imeonewa ,video zipo ,Sheria zipo ,kila mtu kaona ,mashahidi wapo ,basi ni kwenda mahakamani na kudai point 3 haraka sana na kuhakikisha yule mwingine ananyanganywa maana kila kitu kipo wazi ...

Hii itaweza saidia nidhamu kwa mareferee na timu kwa ujumla ...!

Uzi tayari
 
Mahakama ya michezo ni moja tu ya CAS...

Kwingine huku kuna kamati za mashirikisho tu
 
Back
Top Bottom