Hapa tunaishauri Serikali ivunje Katiba kwenye Baadhi ya Mambo. Inachanganyikiwa ifuate lipi na wakati gani

Hapa tunaishauri Serikali ivunje Katiba kwenye Baadhi ya Mambo. Inachanganyikiwa ifuate lipi na wakati gani

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
14,762
Reaction score
32,386
Ukimsikiliza Gwajima Me ana hoja zake na Gwajima Ke ana hoja zake. Kikatiba wapo sawa. Na pia kwa Tamko la Rais. Wapo sawa. Chanjo ni Hiyari. Kwa nini?

Ndio maana Serikali inatujazisha fomu kuwa Chanjwa by your own risk. Ukiwa Ok sawa Shukuru Mungu. Ukiathirika pole maisha yaendelee Haiwajibiki.

Sasa katika hili kikatiba hawa wote wana haki ya kutoa maoni yao. Ni haki yao kuongea kulingana na mitizamo yao.

Nachoshangaa ni kuwa Hata wapinzani wanashauri Serikali imshughulikie Gwajima Me. Kuwa anachosema anapaswa azuiwe,ashtakiwe. Yaani wapinzani wanaichagiza Serikali ivunje Katiba.

Lakini je wapinzani wana hakika haitatokea nao ikaja siku wakapishana kauli na Serikali? Ili pia washughulikiwe?maana watu wanasema tamko alilolitoa Rais halipaswi kupingwa au kupishana nalo.

Nikajiuliza Habari ya ununuzi wa Ndege si aliamua Rais? Si tulisema amevunja katiba au hajazingatia mambo kadhaa? Kwa nini Gwajima kusema yeye hachanjwi na kuwaeleza watu wasiwasi wake iwe Nongwa? Atukanwe,achukiwe na kuhukumiwa?

Serikali imekuwa na Kampeni isiyoisha ya kuwataka watu kutumia Condom. Makanisa na Viongozi wa Dini wamekuwa wakipinga bila kificho. Kuwa kuwataka watu watumie Condom kwanza ni kupingana na kusudi la Mungu la kuzaliana na pia ni kuhalalisha Ngono.

Hivyo watu wanaambiwa wasitumie Condom. Waache kuzini. Hatujawahi sikia wakishambuliwa au kutakiwa kushtakiwa. Hawa wanapoongea hivi maana yake wanachochea maambukizi ya Ukimwi na Mimba zisizotarajiwa. Hatujasikia wakishutumiwa n.k

Suala la chanjo ni jema..watanzania tumechanja chanjo nyingi tu. Lakini suala hili libaki kuwa uamuzi wa mtu binafsi. Kama anayechanjwa anatangaza na asiyechanjwa akitangaza hamkosei mtu.

Tusiishauri kuvunja katiba kwenye suala la Gwajima Kiume (Me) kwa kuwa tunamchukia kwa sababu ya Dini yake,Msimamo wake, Chama chake au sababu nyinginezo.

Mimi nina mambo mengi sikubaliani na Gwajima Me. Lakini hii hainisababishii nishindwe kuona ukweli kuhusu anachozungumza. Au kutaka mpoka haki yake ya Kikatiba ya kuzungumza.

Tusiishauri Serikali mambo ambayo ikishazoea ikatutendea na sisi tutaanza lalamika. Tunataka Serikali iheshimu katiba wakati huo huo tunaishauri imshtaki au kumshughulikia Gwajima kwa kupingana nayo kihalali.

Kesho tutasema Wapinzani wananyamazishwa na Serikali wananyimwa uhuru wa kuzungumza.tutakuwa tunajichanganya.lakini pia si sahihi kumchagukia Gwajima hoja. Kuwa angekuwa wa maana kama angeongelea katiba.

Wakati huo huo kuna watu watakwambia wapinzani mngefanya la maana kuzungumzia Tozo au Ukosefu wa Barabara na si Katiba.

Mtagundua kuwa watu wanachaguliana hata hoja au misimamo. Katiba inasema kila mtu ana haki ya kuamini anachotaka pasipo kuvunja katiba.

Mwacheni Gwajima wa Kiume azungumze. Ajibiwe hoja zake kisayansi ili aonekane hajui kisha apuuzwe...ni rahisi tu.
 
Back
Top Bottom