mkuzi
JF-Expert Member
- Mar 17, 2013
- 1,627
- 1,459
Saruji, mabati, nondo, mafuta kufutiwa kodi
Wakati Spika wa Bunge, Anne Makinda akitangaza Miswada ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT ) na Utawala wa Kodi kusomwa katika kikao cha Bunge lijalo kutokana na kutokamilika kwa sasa, baadhi ya bidhaa zitafutiwa kodi, imefahamika.
Jana Spika alitangaza kuwa kamati husika zinahitaji muda zaidi ili kuweza kuandaa miswada hiyo ya kodi na kwamba haitasomwa katika bunge hili na badala yake itawasilishwa bunge lijalo.
Hata hivyo, akizungumza na NIPASHE jana nje ya bunge baada ya Spika kuahirisha shughuli za bunge, Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, alisema katika muswada huo wanatarajia kufutia kodi baadhi ya bidhaa ambazo alizitaja kuwa ni saruji, nondo, mabati na mafuta.
Alisema wanatarajia muswada huo kuwasilishwa bungeni kabla ya Januari ili uanze kutumika.
"Muswada umeshapita kwa makatibu wakuu nao wamekaa na wataalamu wao hivyo ni wazi wao wanajua kama ni faida kwa taifa au la, sioni sababu ya jambo linalowezekana sasa kwanini lingoje kesho," alisema.
CHANZO: NIPASHE