Hapa Zari anamaanisha nini?

Hapa Zari anamaanisha nini?

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Screenshot_20180415-190943.png

Aliyekuwa mpenzi wa Diamond Platinumz ambaye ni mama wa watoto wawili wa msanii huyo, Zari The Boss Lady ameshindwa kuficha hasira zake na kumshambulia kwa matusi mtandaoni.

Mashambulizi ya Zari aliyoyatoa kupitia snapchat, muda mfupi kabla hajaelekea kanisani yalionekana yakihusishwa na ujumbe ambao Diamond aliuandika kwenye Instagram kuhusu wanawake akipigia debe tukio linalofywa leo na Zamaradi Mketema.

“Ikiwa Mama yangu alinilea Pekee hadi kufika hapa…Naamini Mwanamke ni Kiongozi bora Mwenye kuweza kuleta Maendeleo na Furaha ya Kweli Ulimwenguni….Please Tag wanake wote Wapambanaji na Wapenda Maendeleo waambie @zamaradimketemaKawaandalia jambo Kesho [leo],” aliandika Diamond.

Dakika chache baadaye, Zari aliweka ujumbe wake uliojaa hasira akitumia maneno makali na kumuita Diamond ‘mjinga’. Ingawa hakumtaja jina, kitendo cha kumkosoa kwa kushindwa kuwaona watoto wake kwa muda mrefu kinaonesha kuwa anayezungumziwa ni baba Tifah.
Baadaye, Zari aliweka picha inayomuonesha akiwa mbele ya kioo na nguo nyingi na kuandika ujumbe kuwa ni muda wa kanisani.

“Some manages need to do quality assurance before their artist alter nonsense for public whatever… when last did you see your kids I believe they forgot all about you dummy… Think before you caption. Idiot. Mxuiiii,” aliandika.

Kwa tafsiri isiyo rasmi, “Mameneja wengine wanapaswa kuhakikisha ubora kabla wasanii wao hawajaweka upuuzi kwenye mitandao ya kijamii kwa kupata kiki kivyovyote… hivi ni lini mara ya mwisho umewaona wanao.. Nina amini wamesahau yote kuhusu wewe mpuuzi…. fikiria kabla ya kuandika kwenye picha. Mjinga.”

Zari alitangaza kuachana na Diamond, akaiachia rasmi funguo za ikulu ya WCB ya Madale na kuhamia nchini Afrika Kusini.
 
Dummy? Dummy dad?😀😀😀😀
 
Kuna upuuzi Dai ameupost umemuumiza bidada na anawashangaa mameneja wake kuuruhusu huo upuuzi upostiwe kwenye public.
Anasema watoto wameshaanza kumsahau baba yao kwani hajawaona muda.
Hahahhh mimi acha nicheke kwanza

Ajiulize labda mzazi mwenzie amekusanya ile vinasaba kwa kuangalia kwa macho watoto akaona vimulimuli

Aliona sawa kuweka maisha yake kwenye social media wakati ule leo anashangazwa na nini kwa anachokifanya mzazi mwenzie
Ukipanda bamia utavuna bamia sio karoti
 
It was all about fame and now it has turned in to a sour taste
 
Huo ni upotoshaji. Man utd kapigwa kimoja na West Brom palepale OT, asitake kutufanya sisi mazuzu.
 
Huwa inaniwia vigumu ku_judge maisha ya couple kama hizi, kwa sababu sijui wamepitia mambo gani.

Lakini kama umeshaachana na mtu, hii kuchunguliana kwenye social networks kuona ex wako ka_post nini inakuhusu nini tena?

Na kama umeamua kulea watoto si ulee tu! vinginevyo nenda kimya kimya kawasilishe malalamiko yako ustawi wa jamii juu ya kutelekezwa kwa watoto.
 
Alikuwaga anamtusi Hamisa huyu dooh....
 
Mwanamke ukimuacha na umezaa naye ni shida tupu, hapo watoto hata uwajali vipi atasema huwajali ili mradi amepata pa kusemea. Hii inanitokea hata mimi na mzazi mwenzangu
 
Back
Top Bottom