Hapakuwa na haja ya kuwaondoa wamachinga na kuvunja vibanda pembezoni mwa mji

Nadhani aliyepewa jukumu la kusafisha mji hakuelewa vyema mji unaanzia wapi na kuishia wapi.

Yeye alijua Dar nzima kila mahali ni mji.

Kumbe anayekaa mbagala akitaka kwenda posta anasema nakwenda Mjini, wa mbezi naye hivyo hivyo.

Posta ndio Mjini ak.a Centre Business District na ndiko kulikotakiwa kusafishwa na si kwingineko.
 
Ingewatoa tu katikati ya miji. Huku pembezoni hawana madhara bali wana faida.
Siku gari ikiacha njia ikawazoa hapo barabarani bado mtailaumu serikali sio?

Barabarani sio salama
Na panalet uchafu na msongamano...

Masoko yapo
 
Tatizo watu wabishi sana

Anaangalia urahisi na sio usalama wala usafi nk
 
Kwanza nasapoti 100% kuondolewa kwa machinga maeneo yote ambayo si rasmi na mengine yalikua hatarishi kiusalama barabaran. Pili.. hakunaga utaratib wa hivyo watu wamejaa kando ya barabara kuchuuza bidhaa zao. Imagine pale zakhiem walivyokua wanajaa mpaka magari yanapishana na watembea kwa miguu papo kwa papo. Tatu.. kuwajaza machinga kila sehem ile ilikua kutafuta popularity kisiasa tu hata hayati ni lazima angekuja kuwatimua na kuwatafutia maeneo rasmi. NB: Kikuwa na maeneo rasmi ya kununua nyanya, maembe, viatu, na mahitaj mengineyo tutazoea na tutaenda tu!! Cities planning muhimu na sio kufanya jambo ili ufurahishe umma!!!
 
Unaongelea wamachinga au wafanya biashara ndogondogo. Japo haileti mantiki mtu kuuza majora ya vitambaa, au stationery ukaiita eti ni machinga.
Halafu huu uvivu wa baadhi ya wabongo kuwa muuzaji ndo amfwate mnunuaji barabarani tena stendi ni uwehu tu.
Wakipangiwa maeneo rasmi mbona wateja wanawafuata tu. Kumekuwa na maeneo maarufu kutokana na bidhaa hizo kupatikana huko mfano Mahakama ya ndizi. Wanaohitaji mdizi wanaenda pale na hutowaona wakizifuata goba. Hebu jiongezee kidogo.
 
Cha kusikitisha watu hata hawatoa sababu ya kuwasafisha hadi pembezoni mwa mji.
 
Cha kusikitisha watu hata hawatoa sababu ya kuwasafisha hadi pembezoni mwa mji.
Kwa bahati mbaya tuna viongozi ambao wanapenda kutafuta sifa kwa wakuu wao hawajali nani anaumia mradi yeye kibarua chake kiko salama na mkuu kafurahi.
 
Sijui kulikuwa na logic gani kuwasafisha hadi huku pembeni.
Tumewasafisha ili kuweka usawa na wale wa mjini kati! Huku pembeni walikuwa pia wanapanga bidhaa zao mpaka barabarani! Naiunga mkono serikali katika hili!
 
Banana, Mombasa, Gongo la mboto, Mbagala, Mbezi

Kwa jiji letu la Dar es Salaam, inapendeza na ni salama kuwa Chinga hawatakiwi kuwepo pembezoni mwa barabara zote kuu ktk jiji la Dar es Salaam kama New Bagamoyo, Morogoro Road, Kilwa, Kawawa na barabara zote zinazotumiwa na watu wengi iwe Mwananyamala kwa KomaKoma, Toure Drive , Haile Sellasie, Shekilango, Mandela Express way, Sam Nujoma, Tabata Kimanga, Kinondoni Road, Temeke Wailes, Tandika kwa Kondo n.k
 
South Africa kwa kina Khumbu kulikuwa pia na huu ujinga wa wamachinga kuuza mchicha kwenye lami ya watembea kwa miguu?
 
South Africa kwa kina Khumbu kulikuwa pia na huu ujinga wa wamachinga kuuza mchicha kwenye lami ya watembea kwa miguu?
Durban, Joburg watu wanapanga biashara barabarani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…