Hapana: Serikali bado haijampa heshima stahiki Mzee wetu Benjamin Mkapa

1) mauaji ya raia wasio na hatia kule Pemba mwaka 2001

2) mashirika ya umma kuuzwa kwa bei karibu na bure

3) ufisadi wa pesa za EPA kufadhili kampeni za CCM

4) kuanzisha kampuni binafsi ilhali bado ni rais

5) kutuita Watanzania eti malofa
 
Kwakweli uwanja ulipaswa kufurika
Huyu ni Rais wa watu aliyewahi kushika madaraka ya juu Kama Rais wa nchi.Hakupinduliwa Wala hakupindua hivyo anastahili heshima ya kitaifa Wakati wa maziko yake.
Nadhani watarekebisha walau vyuo vyote kesho vihamie uwanja wa UHURU
 
Yeye aliuza makampuni mengi bila kujari ushauri wa watanzania. Ila bado wakamsamehe. Shida ni nini? Tunavuna tuliyopanda.
 
Nchi imeparaganyika wanachi hawana imani na serikali na wala hawana hamasa ya kushirikiana na serikali tena.

Sababu kubwa ni viongozi kushindwa kutenda haki na kila mtu anaonea wanyonge wake.
 
1) mauaji ya raia wasio na hatia kule Pemba mwaka 2001

2) mashirika ya umma kuuzwa kwa bei karibu na bure

3) ufisadi wa pesa za EPA kufadhili kampeni za CCM

4) kuanzisha kampuni binafsi ilhali bado ni rais

5) kutuita Watanzania eti malofa

Manufaa aliyoiletea nchi yanazidi Makosa machache aliyoyatenda.

Mkapa aliifanyia nchi yetu, makubwa baadhi yake ni haya yafuatayo!

1. Kuvuta Maji kutoka Ziwa Victoria kuelekea Kahama.

Kila mtu anafahamu kusitasita kulikokuwa kunakwamisha matumizi ya maji ya Ziwa victoria kutokana na mkataba wa Kinyonyaji wa kikoloni unaoipa Misri Share kubwa ya maji hayo. Benjamin Mkapa akiwa rais, alitoa go ahead ujenzi wa mradi wa kuyatumia maji hayo bila kuiogopa Misri. Kwa hakika nafuu iliyotokana na maji hayo ni kubwa sana

2. Kuboresha Jiji la Dar (Tume ya Keenja).

Mkapa alipoingia madarakani, Jiji la Dar lilikuwa na hali mbaya sana, lilikuwa limechakaa, lilikuwa chafu kwelikweli. Rais Mkapa akaunda tume ya Keenja iliyofanya kazi kubwa yenye kukumbukwa, ikasafisha jiji, na kukarabati majengo mbalimbali ya serikali yaliyokuwa katika jiji hilo, Jiji angalau likaanza kuwa na muonekano mpya. Kabla ya hapo ilikuwa ni kawaida kwenda kwenye mitaa ya posta na kukuta vinyesi pembezoni mwa majengo mbalimbali. Tume ya Keenja ilijitahidi kurekebisha hiyo hali

3. Kuzipa hadhi ofisi za serikali.

Wakati Mkapa anaingia madarakani, ofisi za serikali zilikuwa choka mbaya sana, yaani zilikuwa kuwa kama mabanda fulani hivi yaliyochoka, samani zilikuwa zimechoka, zimepauka, samani mbayambaya. Lakini Mkapa alizipa hadhi ofisi za umma na heshima ya utumishi wa umma ikaanza kurejea taratibu. Kabla ya hapo watu kazi kwenye utumishi wa umma ilikuwa ikibezwa haswa na vijana walioonja utamu wa hela baada ya nchi kufungulia soko huria kipindi cha mzee Mwinyi

4. Mzee Mkapa aliweka mipango ya kugusa maisha ya watu.

Aluanzisha Mpango Maalum wa Elimu ya Msingi MMEM, Akaanzisha mipango ya Kurasimisha Biashara uitwao MKURABITA, alianzisha programmes kama vile TASAF, MEMKWA, Mipango hii ilikuwa na mchango mkubwa kwenye kuboresha maisha ya wananchi.
Pia ni kipindi cha Mkapa huduma za Afya ziliboreka sana, kwa hospitali nyingi za wilaya kuanza kuwa na vifaa muhimu kama vile X-Rays, na madawa pia kupatikana.

Pia mzee Mkapa alitumia uwezo wake mkubwa wa kidiplomasia kuiwezesha nchi yetu kufutiwa madeni makubwa sana yaliyokuwa yakituelemea

Lakini pia Rais Mkapa alidhibiti mfumuko wa Bei, Bidhaa zilikuwa zinauzwa kwa bei affordable sana. Mfano mzuri ni nauli ya daladala kipindi cha BWM ilikaa shilingi 150 kwa muda mrefu sana bila kubadirika

5. Mzee Mkapa alikuwa champion wa Mageuzi.

Alianzisha reforms nyingi kama vile namna bora ya kuongeza mapato ya serikali kupitia ukusanyaji wa VAT, Pia alianzisha reforms kwenye mifuko ya pensheni kwa kuanzisha NSSF ambayo baadae ilitoa mchango mkubwa sana kwenye kuchochea maendeleo ya nchi yetu na kuwatumikia vyema wastaafu, Pia aliboresha utendaji kazi wa serikali za Mitaa kwa kuanzisha TAMISEMI

6. Mzee Mkapa alianzisha mifumo mingi ya Kitaasisi tunayonufaika nayo hadi hii leo

Baadhi ya mifano ni vitu kama vile
1. Tume ya vyuo vikuu TCU
2. PSRP
3. Wakala wa Barabara TANROADS, Sote tunajua kazi kubwa ya Ujenzi wa barabara iliyofanywa na TANROADS
4. Uwanja wa mpira wa Taifa
5. Yeye ndiye alianzisha mfumo wa Bima ya Afya NHIF, bima inayonufaisha watu wengi sana
6. Alianzisha Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu LOANSBOARD, kupitia Taasisi hii pamoja na changamoto zake, watu wamekopeshwa mikopo ya elimu ya juu lakini pia wameweza kufatiliwa vizuri walipe deni.
7. Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hii tuliweza kuwa na TV ya Taifa
8. Alijenga Daraja la Mkapa, daraja lililosaidia kupunguza adha kubwa sana ya usafiri kwa watu wa mikoa ya kusini.
9. Yeye ndiye aliyeanzisha Tume ya Taifa ya kupambana na UKIMWI ya TACAIDS
10. REPOA

7. Mkapa aliilea sanaa kwa matendo

Ni katika kipindi cha Utawala wake aliwapa uhuru wasanii kufanya sanaa, na ninaweza kusema Golden age ya muziki wa kizazi kipya ilikuwa mwaka 2000 hadi 2005 katika utawala wa BWM. Hiki ndo kipindi Taifa lilishuhudia vipaji vya Bongo flavor. Wakati ule BASATA ilikuwepo lakini haikuwa na Fungiafungia, zimazima mawazo huru ya kisanii, na ndiyo maana vibao vingi classic vya Bongo Flavor vya watu kama Professor J, Sugu, Juma Nature na wengine vilikuwa ni kipindi cha Mkapa kwa sababu alivumilia Mawazo huru katika ubunifu.

8. Kwenye Misiba mikubwa ya Kitaifa aliliongoza Taifa na kuwapa wahanga heshima inayostahiki

Wengi wetu tunakumbuka ajali ya meli ya MV Bukoba, na jinsi Benjamin Mkapa alivyowapa heshima stahiki marehemu, Tunakumbuka Msiba wa ajali ya Treni jinsi Rais alivyoonysha kuguswa kwelikweli na kuwapa heshima ya Kitaifa kwa dhati kabisa. Sote tunakumbuka jinsi alivyohandle msiba mzito sana wa baba yetu wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

9. Mzee Mkapa alikuwa fair, alijaribu kuupiga vita Udini kwa vitendo

Waislamu walivyomlalamikia kuhusu kuwa Nyuma kwenye elimu, kwamba hawajanufaika vya kutosha kwa matunda ya uhuru kwenye elimu, Aliamua kuwapa Majengo ya TANESCO ili wajenge chuo chao kikuu, Lakini pia akayarudishia Makanisa baadhi ya shule zao zilizochukuliwa na Mwalimu Nyerere mfano shule ya Wakatoliki ya Forodhani.

Pia ilipoundwa Bodi ya Parole iliyojaa Wakiristo watupu, Waislamu walivyoonyesha kutofurahishwa na hatua hiyo, aliivunja hiyo bodi na kuunda nyingine yenye uwakilishi mpana wa makundi ya kijamii.

10. Alipunguza umasikini wa wananchi kwa kiwango kikubwa sana.

Wakati rais Mkapa anaingia madarakani, pato la mtanzania mmoja mmoja kwa mwaka (GNI per Capita) ilikuwa ni takriban dola 170, lakini kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wake alifanikiwa kukikuza mara tatu na kufikia Dola 500 kwa mwaka. Hali hii ilileta unafuu kiasi kikubwa sana sana. Leo hii tunashangilia kuingia katika uchumi wa kati, lakini hutuangalii tumetoka wapi kama nchi, Wahenga walisema, Usione vyaelea viliundwa!

Hitimisho:

Hayo ni baadhi ya mambo makubwa ambayo Mkapa aliifanyia nchi hii, yapo mengi sana lakini hayo ni machache.

Binafsi naweza kusema kuwa, Taifa letu lina bahati sana kuwahi kuongoxwa na mheshimiwa Benjamin William Mkapa.

Rais Mkapa alikuwa ni tough kwa muonekano wa nje lakini alikuwa ni mtu mwema sana

Kiukweli Tutaendelea kumuenzi mwana huyu wa Afrika, aliyeifanyia nchi yetu makubwa kwenye ujenzi wa mifumo

Pumzika kwa Amani mzee wetu Benjamin William Mkapa
 
Hivi who cares about haya maccm?

Jitu linaita wananchi wake "malofa" eti kisa hawaamini anachoamini yeye?

Akafie huko,akafie mbali kama wengine tunavyokufa huku!
 
ndugu yangu naona unaipongeza ATM yako mwenyewe!!
 
Hizi ndio zilikuwa shughuli za Bashite sasa.. Angepiga tukio la hatari mno
 
Akili za jiwe na jeshi lake Zimeganda wanajiandaa kwa ujio wa Tundu Lissu mchana huu kweli yutaona mengi awamu hii.
 
Kuupa heshima stahiki msiba huu mzito hauzuii maisha kuendelea mbele!
Tatizo wanaosema humu wameenda au wana mpango huo? Haya mambo ya kujazana barabarani yanaitikiwa zaidi na wanyonge. Tumewafikia je? Labda maisha yamewachanganya.
 
Nashauri mzee wetu apelekwe kwa njia ya barabara hadi nyumbani Masasi ili watu wa kusini tupate nafasi ya kumpa heshima za mwisho japo kwa kumpungia barabarani, bila yeye hakuna daraja la Mkapa alilolijenga na kuturahisishia usafiri Wana kusini.
Hivi Daraja la Mkapa halijajengwa JPM? Maana mara nyingi tunaambiwa kuwa JPM pekee ndo kaleta Maendeleo tunayaona hivi sasa. Kumbe misifa mingi ya JPM ni fake!
 
Hata vidole havilingani ukichanganya na Covid-19, bado watu wanachukuwa tahadhari.

Kifo cha Mwl.Nyerere bila kuhamasisha watu,walifurika kwa wingi barabarani haijapata kutokea.
 
Watu wa Magufuli wanataka mtu wao aenziwe, lakini JPM hakuupa msiba wa Mkapa heshima ya kutosha.
 
Back
Top Bottom