Hapana Uchawi kwa Walokole kindakindaki. Haina haja ya ndumba

nipo online

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2022
Posts
1,039
Reaction score
2,657
Hapa siwazungumziii walokole wa kusali bora liende la hasha. Kwa wale walio badilishwa maisha yao na kumfata YESU KRISTO na kumwamini ushirikina hauwezi kufua dafu hapana nazungumia hirizi, kuvunjiwa nazi mlangoni, kuchinjiwa ndege sijui vyote hivi haviwapati kamwe.
 
Hakuna uchawi popote nje ya dhana za kiimani tu.
 
Hapa siwazungumziii walokole wa kusali bora liende la hasha. Kwa wale walio badilishwa maisha yao na kumfata YESU KRISTO na kumwamini ushirikina hauwezi kufua dafu hapana nazungumia hirizi, kuvunjiwa nazi mlangoni, kuchinjiwa ndege sijui vyote hivi haviwapati kamwe.
Amen, Glory be to GOD
 
Usirahishishe mkuu ukiwa uko mwepes mwepes unalipuliwa nje ndani na kusali kwako.
Wewe ndiye unarahisisha kufikiri mimi nasali.

Mimi atheist. Siamini uwapo wa Mungu. Siamini uwapo wa uchawi. Siamini katika kusali.

Sasa habari za kusali unaniletea vipi mimi Mnyambisi?
 
Utajua wewe
 
Nitajua mimi wakati wewe ndiye ushanipangia?

Nakwambia hivii, hakuna uchawi.

Hizo habari za uchawi ni imani za watu wajinga tu.

Ushaelewa hilo somo?
Wachawi wapo ukibisha unapaswa upelekwe mirembe
 
Hapa siwazungumziii walokole wa kusali bora liende la hasha. Kwa wale walio badilishwa maisha yao na kumfata YESU KRISTO na kumwamini ushirikina hauwezi kufua dafu hapana nazungumia hirizi, kuvunjiwa nazi mlangoni, kuchinjiwa ndege sijui vyote hivi haviwapati kamwe.
thibitisha kama kuna uchawi
 
Wachawi wapo ukibisha unapaswa upelekwe mirembe
Tuanze mwanzo kabisa.

Uchawi ni nini? Na ukiona kitu unachofikiri ni uchawi, utajuaje huu ni uchawi kweli, na si kitu tofauti usichokielewa wewe tu?

Kwa mfano, ukimfufua babu aliyefariki miaka 200 iliyopita aje aione dunia ya leo, ma TV, internet, magari, ndege, silaha, na kadhalika, ataona vyote hivi ni kama uchawi tu.

Wakati hakuna supernatural power inayotumika hapo popote. Ni natural power ya technology tu.

Vyote hivi si uchawi, ni teknolojia tu asiyoijua.

Sasa, na wewe ukiona kitu ukasema hiki ni uchawi, utajuaje huu ni uchawi kweli na si teknolojia tu ambayo bado hujaielewa?
 
Hapa siwazungumziii walokole wa kusali bora liende la hasha. Kwa wale walio badilishwa maisha yao na kumfata YESU KRISTO na kumwamini ushirikina hauwezi kufua dafu hapana nazungumia hirizi, kuvunjiwa nazi mlangoni, kuchinjiwa ndege sijui vyote hivi haviwapati kamwe.
Very poor mindset. Hizi ndio zile akili unakuta anatembea amefumba macho akijikwaa anaanza kukemea pepo limeshika njia 😆😆😆😆
 
Tuanze mwanzo kabisa.

Uchawi ni nini? Na ukiona kitu unachofikiri ni uchawi, utajuaje huu ni uchawi kweli, na si kitu tofauti usichokielewa wewe tu?

Kwa mfano, ukimfufua babu aliyefariki miaka 200 iliyopita aje aione dunia ya leo, ma TV, internet, magari, ndege, silaha, na kadhalika, ataona vyote hivi ni kama uchawi tu.

Wakati hakuna supernatural power inayotumika hapo popote. Ni natural power ya technology tu.

Vyote hivi si uchawi, ni teknolojia tu asiyoijua.

Sasa, na wewe ukiona kitu ukasema hiki ni uchawi, utajuaje huu ni uchawi kweli na si teknolojia tu ambayo bado hujaielewa?
Hua unasoma biblia?
 
Back
Top Bottom