Hapiness Magese avishwa pete ya $76,000

Watu wasio na hela utawajua tu. Mnashangaa pete ya dola 76,000.00....teheteheteheeee
 
Jamani siamini kama kweli hiyo pete inathamani hiyo au tarakimu zimekosewa,hembu mtwaambie kama ni kweli hicho kipete tu kiwe na thamani hiyo je mambo mengine yatakuwa na thamani gani,eeh mola wangu waja wake tumurudie jamani kama ni kweli hizo ni kufuru sijui ndugu wa hizo familia mbili wote wako matawi ya juu? Na kwanini watutangazie au ndo kumkoma nyani girani,hebu tuambieni jina la mzazi wa mtoto wa kifisadi kwa maana mtoto wa chatu ni chatu bana
 
Wacha kabisa about 90 Milion TZS pete tu. Tafadhali mkipata picha ya hiyo pete tunaomba kuiona. Sasa inabidi atulie na amwambie ukweli kama anampenda jamaa manake mapenzi sio vitu vya thamani wala pesa ni kitu cha kutoka Moyoni.

Hongera zake.
 
Hivi kila mwenye hela ni fisadi?tuacheni kuwa na roho za kimasikini.
 
Watu wasio na hela utawajua tu. Mnashangaa pete ya dola 76,000.00....teheteheteheeee

Sina hela kweli kibanda changu ninachoishi ndio kinaweza kufikia hiyo thamani lazima nishangae. Na pia ni mshahara wangu wa miaka 10 kwa mahesabu ya haraka.
We mwenye mihela tukopeshe tuendeleze jamiiforums basi.
 
Julius yuko wapi?

mambo haya anajua jinsi ya kuyaelezea..siye ambao hatujui mambo ya siku hizi kimya
 
Sina hela kweli kibanda changu ninachoishi ndio kinaweza kufikia hiyo thamani lazima nishangae. Na pia ni mshahara wangu wa miaka 10 kwa mahesabu ya haraka.
We mwenye mihela tukopeshe tuendeleze jamiiforums basi.

Nioneshe niliposema mimi nina mihela...
 
Swali je wewe ungekuwa na hela kama hiyo ungekumbuka kusaidia huko kijijini au ni maneno ya mkosaji?.....Kila mtu anafanya kitu ile roho napenda...kama anacho then kwa nini asimvalishe mchumba wake kitu cha thamani?....na wewe work hard to earn hiyo $76,000 then ukasaidie kijijini...

This is BS!
 
Sina hela kweli kibanda changu ninachoishi ndio kinaweza kufikia hiyo thamani lazima nishangae. Na pia ni mshahara wangu wa miaka 10 kwa mahesabu ya haraka.
We mwenye mihela tukopeshe tuendeleze jamiiforums basi.

Sasa ndugu Minja kwa kuwa tu watu fulani hawana kitu fulani ndio wale wenye nacho waache kukitumia kwa kuwaonea huruma wasiokua nacho? Enzi za ujamaa zimeshaisha, nyakati hizi si zile tena!
 
duuuuuuu hiyo ni kufuru ya kufungulia mwaka, ila dada akumbuke kuwakuna wenzetu wa kilosa wanahitaji mahali pa kulala, vyakula na kama kilosa mbali basi angeenda kutoa msaada hata mbagala maana baadhi ya wale wahanga wa mabom bado wanalala katika mahema
 
Bei ya pete aliyovishwa binti Magese si shughuli yetu, ni yake yeye na familia yake na rafiki zake. What's next, utatuambia kavaa chupi ya bei gani?

Sema huyo fisadi kafisadi wapi na kivipi.Vinginevyo unaweza kuleta gele na chuki za kimasikini tu.

Kuna Watanzania wanafanya kazi za kueleweka kisheria, wako kimya viwanjani wanaweza kabisa kufanya vitu hivi bila ufisadi wala nini.

Kwanza haya mambo ukiyajua vitu hivi vinachukuliwa mortgage tu, it is not like ni lazima ulipe $ 76,000 hapo hapo.
 
Bei ya pete aliyovishwa binti Magese si shughuli yetu, ni yake yeye na familia yake na rafiki zake. What's next, utatuambia kavaa chupi ya bei gani?

yaani hapa hata senkisi nakupa maana you Nailed it Mr K.....


Sema huyo fisadi kafisadi wapi na kivipi.Vinginevyo unaweza kuleta gele na chuki za kimasikini tu.

LOL!....Si unajua maneno ya mkosaji!...
 
magese gani?

yuleyule ambaye hata wowowo lake kuliona mpaka uvae miwani?????

kweli wanaume wamedata!!!!!!!!!!!!!!
 
magese gani?

yuleyule ambaye hata wowowo lake kuliona mpaka uvae miwani?????

kweli wanaume wamedata!!!!!!!!!!!!!!

Wewe unafikiri kila mtu anatafuta wowowo kama wewe?

"Wengine wanasema wana usongo
Wengine wanabaki wanapigana madongo
Wabongo, Wabongo, Wabongo, Wabongo
Aaah Yeah"

-Wabongo Mr II
 
Japo hatujawa na uhakika na figure hii ya $ 76,000 naamini kuwa maoni ya watu kwenye hili lazima yawe tofauti kwani inategemea unaangalia suala hili kutokea upande gani.

Kwangu binafsi ninachojua ni kuwa vyanzo vya mapato yetu na jumla ya mapato hayo yanatofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Vile vile matumizi yetu yanatofautiana kutokana na viapumbele ambavyo tunakuwa tumejiwekea.

Mtu mmoja amesema shs. 5000 kununua pete ni ufisadi kwa mtu anayepata pato la shs. 15,000 kwa mwezi ukilinganisha na mtu anayepata mil 500 kwa mwezi kununua pete ya mil 76. Kwa hiyo suala la msingi hapa ni kuwa jamaa ana kipato cha shilingi ngapi na je nini kipaumbele chake cha matumizi.

Ninapopanga kwamba kila baada ya miaka mitatu nitaenda kuwasalimia wazazi na ndugu huko mwisho wa reli na kuwa nitasafiri kwa ndege na familia ya watu sita. Ukifika kijijini Kasulu na baadhi ya wanakijiji wakajua (kwani watoto watasema walipanda ndege toka Arusha mpaka Kigoma), wako wanaoona kuwa nina hela nyingi na kujiuliza kwa nini siwezi kupanga kusafiri na treni au mabasi na hizo hela nikawasaidia kwani wanazihitaji. Kwa upande wao wanaweza kuwa sawa kwa mawazo yao lakini kwa upande wangu ni urahisi na mipangilio ndo inanifanya nitumie usafiri huo na najua kuwa binafsi sina uwezo wa kusaidia matatizo ya kifedha ya ndugu na jamaa zangu wote.

Hata hivyo kuvaa pete ya dola 76,000 kwa mazingira yetu ya kibongo ni kitu cha hatari sana kwani vibaka tunao kila kona na sijui utatembea wapi ambapo hautafuatwa na hawa jamaa wakijua kweli umevaa pete ya thamani hii. Juzi juzi tu mke wangu aliniambia kuwa yuko mtu anataka kumuuzia mkufu wa dola 300; kwa hali tuliyonayo dola 300 tungeweza kununua lakini tukashauriana kuwa kwa nini kuvaa kitu cha dola 300 ambacho kitahatarisha maisha. Tukakubaliana kuacha.

Kwa hiyo cha muhimu hapa nini msukumo wa kutumia the way unavyotumia pesa zako na je ukilinganisha na kipato chako hilo unalotaka kufanya ni matumizi ya kianasa au la? Kumbuka kwa mtu mmoja kununua gari la milioni 100 ni anasa wakati kwa mtu mwingine ni matumizi ya kawaida. Utofauti wetu ni vipato na vipaumbele tulivyonavyo katika kupanga matumizi yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…