Hapo zamani, kujiunga na shule za Sekondari za Serikali ilikuwa ujiko mkubwa sana maana shule hizo zilikuwa na kiwango cha juu ukilinganisha na shule binafsi (ondoa seminari).
Nakumbuka ilinipasa kurudia shule ili niweze kufauli kwa kuchaguliwa kwenda shule ya Seikali. Nilipomaliza mara ya kwanza 1985, sikuchaguliwa ikabidi nirudie na ndiposa nikafaulu na kujiunga na Shule ya Serikali. Ilikuwa Bonge la Ujiko!
Hivi sasa wazazi hawataki watoto wao wajiunge na shule za Serikali hata kama wakifaulu, wenye uwezo huwapeleka shule za private za gharama kubwa maana inasemekana elimu inayotolewa na shule hizo ni ya hali ya juu kuliko inayotolewa na shule za Serikali.